Jumamosi, 6 Septemba 2014

ILI KUPATA LAZIMA UPOTEZE



ILI KUPATA LAZIMA UPOTEZE!!!





I wakorintho 9:24-25

…………na kila ashindanaye katika mchezo hujizuia katika yote.

I wakorintho 9:26-27
…………bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe nikiisha kuwahubiri wengine; mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Katika dunia tuliyonayo mambo mengi tunayoyaona kuna watu wamepoteza vitu vingi sana na wewe unafurahia matokeo ya watu kupoteza mathalani wako watu wamepoteza muda wao,uhai wao, nguvu zao na ufahamu wao.

Katika ujumbe huu neno hili kupoteza nimelitua katika mawanda mbalimbali mathalani hali ya kutoa kwa ujumla wake fedha, nguvu na muda katika lililo jema, matendo ya kujigharimu kwa ajili ya wengine katika hali njema.

Ni jambo la kushangaza sana watu wengi wanapenda kupata sana lakini hawako tayari kupoteza pasipo kujua wakati mwingi msingi wa kupata ni kupoteza. Kwa mkristo yeyote aliye wa kweli lazima kanuni hii haiweke katika utendaji wake ilikupata ya rohoni lazima uyapoteze ya mwilini!

Pamoja na hayo lazima ujue kwamba unapoteza nini na kwa namna gani unapoteza haya yote ni muhimu sana ili uweze kufanikisha yale ambayo unatakiwa, na kuna siri kubwa sana katika kupoteza kwani hali hii ni inaashiria kutoa kitu kimoja ili kiingie kitu kingine, na kawaida kinatoka kitu kidogo na kuingia kitu kikubwa.

Ni kweli yako maumivu makubwa sana katika kupoteza(kutoa) lakini hayo maumivu yatazimishwa baada ya kupata(gain) hii ipo wazi hata pindi mkulima anapofanya kazi uwa vitu vingi anavipoteza nguvu, fedha na mangine mengi lakini mwisho anakuwa na furaha kupita ile ya awali baada ya kupata.

Watu wengi ujizuia sana ili wasipoteze hasa kitu ambacho wanachokipenda sana kwakua hawajui nini kitatokea baada ya hapo lakini ni vizuri ujue kwamba kujuzuia kupoteza wakati mwingi ni kujizuia kupata.

Yesu alisema….inanibidi mimi niondoke ili aje huyu Roho mtakatifu atakaye wafundisha na kuwa kukumbusha yote!

Japo yesu alikuwepo duniani katika lengo la ukombozi na pindi alipomaliza ili mlazimu aondoke japo watu wengine wanamwitaji azidi kuwa nao, lakini yeye alitambua kuwa ni vizuri yeye aondoke aje huyo Roho atakayekamilisha.

Lazima akili yako ikubaliane kuwa kuna mambo mengine ni muhimu kupoteza ili uweze kuwa katika namna nyingine hata kama itakugharimu kwa muda fulani kwani ni muhimu ugharimike leo kwa pumziko la kesho kuliko kinyume chake.

Kupoteza ni tabia ya Mungu mwenyewe yesu alisema….nautoa uhai wangu kisha nita utwaa tena na baada ya kutoa uhai wake na kurejea tena hawezi kuwa vilevile alivyokuwa vile alivyokuwa awali.

Usitegemee kuwa mkubwa sana kama ukiwa hauna tabia ya kupoteza(kutoa na kusahau) kwakua vile unavyo jigharimu ndivyo utakavyo stawi ( kujigharimu katika akili njema-maarifa sahihi) na kama hauta weza jambo hili hawezi kuwa sawa na mtu unayemtamani, kwakua ipo siri kubwa katika kupoteza na kusahau kabisa.

Usipendelee kushangaa tu vitu vilivyotokana na watu katika kupoteza na wakawa watofauti bali ata wewe unaweza kujiunga nao katika kupoteza kuliko kwema kwa hatua njema ya maisha yako.

Pia katika kupoteza lazima uwe tayari kutoeleweka na watu wengine wanaweza uonekana kama wana kuhurumia sana bali kumbe ndipo wana kuangamiza.




Imeandaliwa na ;
                    
                                Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com                     



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni