NAPENDA
VITA;
Nikiwa najua wazi kuwa katika vita kuna kushinda na
kushindwa lakini pamoja na hayo yote ni seme wazi napenda sana vita, kwakua ni
vita pekee inaweza kunionyesha na kunifuza yale yote ambayo kwa namna ya
kawaida ni singeweza kuyaelewa na hata kuyamudu lakini kupitia vita inanipa
kujielewa sana, kupata ufahamu mwingine katika yale ambayo yananizunguka.
Najua kwa uhalisia kabisa kuwa vita ni mbaya kwani
inaweza kuleta maafa makubwa sana katika jamii yetu….bila shaka utakuwa njia ya
panda lakini sisemi vita ya kutumia vifaa vya moto kama vile bunduki mabomu la
asha bali na zungumzia vita katika mapambano ya kimaisha ya kila siku na
vilevile na zungumzia namna ya kukabili yale yanayotaka kukukabili pasipo
kupepesa macho kwani ukipepesa macho ni wazi utatoa mwanya kwa Yule anaye
kukabili kuona amekushinda.
Lakini niseme wazi kuwa vita hii ya maisha katika
kupambana kutokana na mapungufu tuliyonayo wengine elimu wanatakusoma lakini
uwezeshwaji unakuwa haupo, wengine wanataka kujenga kutokana na kero za nyumba
za kupanga lakini uchumi bado ni changamoto nyingine, mwingine kampata mke au
mme lakini vile alivyotazamia kumbe sivyo na hata vijana kukicha wako katika
mausiano lakini bado kusalitiwa na kutendewa ndivyo sivyo katika ulimwengu wa
kimapenzi nao umeshika kasi uwa watu hawaoni wapi kuna uwafadhali,
Katika vita hii wako watu wanaamua kujinyonga,
kuachana na habari za kimausiano na wengine kuamua kuishi maisha wasiyoyataka
laity wangekuwa na uwezo wangeomba wajengewe dunia ya kwao ili waishi huko
pasipo buguza yoyote hile na wengi wao wanaishi kwakua amua kuwa na kinyongo
katika moyo wao na wale walio tumiwa katika kufanyika kuwa jaka la moyo ndani
yao.
Hautaji kuambiwa na mtu bali nikile kinachoendelea
ndani yako kinachokuweka njia mbili za mkato kati ya kushoto au kulia yote
yanabebwa na wewe na hivyo kusababisha kuwa ni vita kali pamoaja na mashindano
yasiyoisha.
Pamoja na changamoto zote hizo katika vita
unayokukabili bali tambua kuikabili ndio njia pekee katika kukufanikisha kwenda
katika ustawi mwingine lakini tujiulize jambo moja je!inakabili vita katika
maarifa yapi? Katika nguvu ipi? Na katika uimara upi? Mambo yote haya ni ya
muhimu sana kwani katika hayo ndio uweza kukutambulisha pamoja na kukupa
uhakika wa kushinda ua kushindwa.
Ni vizuri kutambua vita ipo kwakusudi lake hivyo
wewe kulitambua kusudi la vita ni moja ya ufahamu wako kuweka katika njia ya
ushindi pasipo udhihirisho katika ulimwengu wa macho yako, lazima utambue vita
imebeba kusudi la Mungu na sio uonevu kama unaweza ukachukulia kirahisi tu.
Bali vyote vimebebwa na kusudi la Mungu haijalishi
katika macho yako yamebeba makusudi gani lakini asili yake imebeba utukufu na
ustawi wako usio elezeka wala usio beba tafsiri ilipata kibali kwa mwanadamu.
Na muhimu uwe mtu katika kujiandaa na vita wakati
wote katika ufahamu wako na wala sio katika mazingira ya hofu bali katika
mazingira yalibeba matumaini na uhakika pasipo kukata tama.
Ni ukweli ulio wazi sio wewe unayepigana bali ni
Mungu mwenyewe anapigana wewe unawakilisha tu lakini vita haipigani kwa ajili
ya kutaka kukumaliza bali ni kutakuua kile kilicho ndani yako ambacho kwa hicho
kina kuwa ni tatizo katika utawala wao, ni seme wazi hautaji kuiogopa vita au
kuikimbia kwakua kazi yako katika vita ni kufuata maelekezo tu na wala sio jambo
jingine………….kwakua yeye MUNGU naujua mwisho wako kabla ya mwanzo kuanza!
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson…………………………………..0764018535