JICHO LANGU NDIO MAAMUZI YANGU
Kile
ninachokiona ndicho nitakachoamua sio kile ninakachokisikia!
Hakuna kitu kigumu kama
maamuzi na hakuna kitu chepesi kama maamuzi ila inategemea maamuzi haya
yamebebwa na nini na yanahusu nini?
Katika uwanda wa
mwanadamu kuamua jambo ni dhana pana kuna maamuzi yanatokana na kushawishiwa na
maamuzi yanayotokana na busara za mtu husika………..mwisho wa siku yote
yanajulikana ni maamuzi yaliyo amliwa na mtu kwa utashi wa mtu husika.
Wako watu wameacha
kazi,rafiki,jamaa na hata kugombana na wazazi kwasababu ya kuambiwa maneno na
kuyaamini na hatimae kuchukua maamuzi ya kuacha hama kuendelea, maamuzi yanayotokana
na kuambiwa yamekuwa na nguvu sana kwakua tunaishi katika dunia ambayo hatujui
yote hivyo tunahitaji kusikiliza wengine katika kuchukua maamuzi na tunahitaji
kuishi kwa amani na ndugu wanaotuzunguka,
Niseme hata kama wewe mwenyewe uliwai kuamua maamuzi pasipo kushuhudia
mwenyewe ila katika ushawishi wa maneno nikutoe hofu wewe si wa kwanza……hata adam alipoulizwa na Mungu kwanini
umekula tunda alisema ni huyu mwanamke uliyenipa…..!!!
Japo matokeo yake yamekuwa
ni athari si kwao hata katika ulimwengu sasa na mengi yanatupata kutokana na
maamuzi ya hawa watu wawili.
Hakuna kitu kizuri kama
kuamua maamuzi yaliyobebwa na ushuhuda wa macho yako na sio ushawishi wa upande
wanje! Kwakua maamuzi yanakupa nguvu na kukupa ujasiri katika mwenendo wako,
ukweli maamuzi mengi tunayo yafanya kiukweli sio katika maamuzi yaliyobebwa na
ushuhuda wa macho yetu. Usipende kuwa na maamuzi yakushinikizwa usio na muono
wako binafsi kwamba hivi nasikia au kuambiwa mambo ambayo ya na ushuhuda wenye
nguvu katika macho au wakimazingira! Pasipo uhakika wako mwenyewe.
Wako watu waliopoteza
Baraka zao na ushindi wao kwa kuambiwa na kushawishika na watu wengine pindi
mtu husika anapoamua kumshilikisha mtu jambo lake………….mathalani biashara
imeenda vibaya wanaokuzunguka au uliomshirikisha anaweza kusema kuwa uliyenaye
sio mwaminifu hivyo vunja nae huo mpango kwani hata kuzidi kukurudisha nyuma
maendeleo yako na wewe kutokana na usadifu wa mazingira na nguvu ya ushawishi
kwa mtu ukaweza kuamua sasa mimi basi acha niangalia upande mwingine!
Maamuzi yaliyobebwa na
macho yako…. kiukweli yanakuwa hayana unafiki wala ushawishi wa mtu au chochote
kwakua unakuwa na ushahidi wa kutosha sana ambao moyo wako unakushuhudia kuwa
uko salama na sifa kubwa katika maaamuzi haya uwa haya ambatani kabisa na
uzushi kwakua kile unachokifanya unakiamini.
Haya ni maamuzi
yanakufanya kuwa mkweli na kuwa halisi sana katika kile unachoamua na bila
shaka dhamira yako inakuwa haina hatia kwakua kile unachokiamua ni kwa ajili ya
kujenga wakati wako katika uzuri.
Nipende kusema kuwa
hakuna maendeleo ya kweli kama ukiwa unaamuliwa mambo yako nawe kisha unafuata
na kamwe hawezi kwenda mbele japo utaongeza miaka!
Maamuzi ya kuaamliwa
yanakuweka katika maisha ya utumwa ambao hutaweza kutoka katika utumwa huo kama
utachukua maamuzi bila ya kuheshimu maamuzi yako binafsi kwakua wewe ndio
unatakiwa kuonyesha unaijali na kuithamini kesho yako.
Bila shaka ukiwa
unaendelea na utumwa wa maamuzi sio rahisi kuungamanishwa na Mungu hata kama
ahusiki mkumbuke adamu hata alivyojitahidi kujitetea lakini hakusikizwa tena
kwakua Alisha kula tunda ambalo Mungu aliigiza lisiliwe lakini yeye katika
ushawishi wa mwanamke ambaye Mungu mwenyewe aliluhusu awe nae.
Mungu
amekupa akili akaweka wazo na akakupa kuamua hivyo mtendee haki Mungu
kwakuendeleza kile alichokianzisha ndani yako!!!
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson………………………………………..0764
018535