CHAKULA CHAKE NI MAUMIVU YA MUNGU
Sote tunajua kuwa
chakula ni kitu muhimu sana kwani pasipo chakula uhai uweza kutoka hivyo
tunavyokula chakula inasaidia kuustili uhai ambao Mungu ameweka ndani yetu
uzidi kuwepo chakula ni kitu kizuri na
muhimu sana kwani katika hiki tunapata uwezesho
wa kuishi na kuona fahari ya maisha yetu katika kukizi mahitaji ya mwili
(katika hili mwili unakuwa na nguvu) na kujisikia kuwa ni mtu kama watu
wengine!!
Nazungumzia chakula
kama kitu cha msingi katika maisha ya mwanadamu kwani mtu anaweza kukosa
mavazi, malazi akaishi lakini kamwe sio chakula kinachoweza kusababisha viungo
vya mwili kufanya kazi na hata kufanya utendaji wa mwili kuwa mzuri!
Kwa utafiti wangu mdogo
binadamu anaweza kukaa siku nyingi bila nguo akawa salama na kuendelea kuishi
lakini sio kushindwa kula katika siku hizo na kuweza kuendelea kuishi ila yesu pekee ndiye aliyeweza kukaa siku
arobaini bila kula!
Ni kubali wazi kuwa
binadamu hatupo kwa ajili ya chakula ila chakula kipo kwa ajili yetu….hivyo
hatuna budi kukitumia kwa ajili ya kujenga afya njema ya miili yetu.
Kisayansi wanasema
muonekano wa mtu uonyesha au udhihirisha kiwango au ubora wa chakula
anachokula.
Ukweli kwamba mambo
mengi ambayo yanafanyika katika dunia, yawe mambo mema na hata yasiyo mema
mwisho wa yote yanakamilishwa na jambo au kitu kinaitwa chakula kwa ajili ya
kuridhisha mwili katika kuupa matumaini ya kuendelea kuishi!!
Wako watu
wanashughulika katika maisha yao ya kila siku kwa ajili yao na wengine kwa ajili
ya familia zao, na hata kwa ajili ya ndugu na jamaa wanao wangalia…..ukweli ni
seme kuwa katika mambo yanayoweza kuumiza kichwa sana kwa mtu mwenye majukumu
ya kuwa hudumia jamii inayo mzunguka na hasa familia inayo mtegemea ni pale
anapokosa uwezo wa kuwapa chakula!
Mambo mengine yanaweza
yaka simamishwa kwa mtu baada kugundua kwamba uhakika wa chakula haupo au ni
mdogo…..hata mzazi anapotaka kumpeleka mwanae shule jambo ambalo linampa furaha
sana ni kuona kwamba mtoto wake ana uhakika wa kula vizuri tena katika hadhi
anayopaswa!
►Ni seme hili ni jambo muhimu sana lakini katika jamii yetu
imekuwa ni tatizo hasa pindi uwezekano wa chakula hicho kutopatikana na
ijulikane wazi ninapozungumzia chakula rafiki yake mkubwa ni fedha.
Katika kukidhi mahitaji
yake binafsi au familia yake mtu anapokosa kuona uwezekano wa kupata fedha kwa
njia iliyo sahihi na kukidhi mahitaji ya familia yake lolote linaweza fanyika!
Wamekuwa watu wakiuana
kwa ajili ya kupata fedha na kukidhi mahitaji ya familia zao hasa wenye uwezo huo lakini kwa wengine wamekuwa
wakijiingiza katika shughuli zingine kwa ajili ya kupata fedha katika kukizi
mahitaji yake na familia yake kubwa ni chakula moja wapo ya shughuli hizo ni
ujangili, ujambazi, utapeli na hata ukahaba!
Wengi wanaofanya
shughuli hizi sio kama wanapenda bali yote ni katika mbio katika kufanikisha mahitaji
katika familia yake na yeye muhusika.
Watu wamekuwa wakiuuza
miili yao ili wapate fedha kujikimu katika maisha yao watu hawa wanafanyakazi
kama wanapenda lakini ukweli ni mateso katika maisha yake!
Japo wako wengine
wanafanya shughuli hii pasipo kuwa na uhitaji huu hasa hawa si wazungumzii
kwakua hawa wanahitaji kitu kingine ili kiwasaidie lakini katika wale ambalo
hawanauchaguzi hayo yamekuwa maisha yao na zaidi sana yamekuwa ni maumivu ya Mungu!
Katika makusudi ya
Mungu katika kumuumba mwanadamu hajawai kufikiria kusudi la mtu kuuza mwili
wake ili kujikim mahitaji yake na familia yake….bali yote haya kwasababu
mwanadamu ana utashi wa kufanya chochote ila matokeo yake kamwe huwezi
kuyabadili yanakuja sawa na ulivyofanya.
Ni pende kusema kuwa
bado unanafasi ya kufanya vizuri na kuwa bora kwa Mungu kwa mtu ambaye anaye
husika maisha yake katika kuuza mwili wake bado unaweza kuwa bora na kuwa wa
maana hata kuliko unavyofikiri.
Chukua nafasi hii kwa
wewe unayesoma kuwa mwema kwa watu wa jinsi hii kufanya kuwa duniani ni mahali
salama ambapo yeye anahitajika sana na sio kumuonyesha UPENDO tu! Bali aweze
kuona YESU kuwa ndiye mtoshelevu wake na sio kitu kingine!
Mungu
hajawai choka, hata choka na kamwe hawezi kuchoka kwa mtu anayempenda bila
shaka ni wewe!
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson…………………………………..0764
018535
Baraka za Mungu zipo kwa ajili
yako!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni