Jumanne, 28 Julai 2015

JICHO LANGU NDIO MAAMUZI YANGU



JICHO LANGU NDIO MAAMUZI YANGU



 Kile ninachokiona ndicho nitakachoamua sio kile ninakachokisikia!

Hakuna kitu kigumu kama maamuzi na hakuna kitu chepesi kama maamuzi ila inategemea maamuzi haya yamebebwa na nini na yanahusu nini?

Katika uwanda wa mwanadamu kuamua jambo ni dhana pana kuna maamuzi yanatokana na kushawishiwa na maamuzi yanayotokana na busara za mtu husika………..mwisho wa siku yote yanajulikana ni maamuzi yaliyo amliwa na mtu kwa utashi wa mtu husika.

Wako watu wameacha kazi,rafiki,jamaa na hata kugombana na wazazi kwasababu ya kuambiwa maneno na kuyaamini na hatimae kuchukua maamuzi ya kuacha hama kuendelea, maamuzi yanayotokana na kuambiwa yamekuwa na nguvu sana kwakua tunaishi katika dunia ambayo hatujui yote hivyo tunahitaji kusikiliza wengine katika kuchukua maamuzi na tunahitaji kuishi kwa amani na ndugu wanaotuzunguka,

Niseme hata kama wewe mwenyewe  uliwai kuamua maamuzi pasipo kushuhudia mwenyewe ila katika ushawishi wa maneno nikutoe hofu wewe si wa kwanza……hata adam alipoulizwa na Mungu kwanini umekula tunda alisema ni huyu mwanamke uliyenipa…..!!!

Japo matokeo yake yamekuwa ni athari si kwao hata katika ulimwengu sasa na mengi yanatupata kutokana na maamuzi ya hawa watu wawili.

Hakuna kitu kizuri kama kuamua maamuzi yaliyobebwa na ushuhuda wa macho yako na sio ushawishi wa upande wanje! Kwakua maamuzi yanakupa nguvu na kukupa ujasiri katika mwenendo wako, ukweli maamuzi mengi tunayo yafanya kiukweli sio katika maamuzi yaliyobebwa na ushuhuda wa macho yetu. Usipende kuwa na maamuzi yakushinikizwa usio na muono wako binafsi kwamba hivi nasikia au kuambiwa mambo ambayo ya na ushuhuda wenye nguvu katika macho au wakimazingira! Pasipo uhakika wako mwenyewe.

Wako watu waliopoteza Baraka zao na ushindi wao kwa kuambiwa na kushawishika na watu wengine pindi mtu husika anapoamua kumshilikisha mtu jambo lake………….mathalani biashara imeenda vibaya wanaokuzunguka au uliomshirikisha anaweza kusema kuwa uliyenaye sio mwaminifu hivyo vunja nae huo mpango kwani hata kuzidi kukurudisha nyuma maendeleo yako na wewe kutokana na usadifu wa mazingira na nguvu ya ushawishi kwa mtu ukaweza kuamua sasa mimi basi acha niangalia upande mwingine!

Maamuzi yaliyobebwa na macho yako…. kiukweli yanakuwa hayana unafiki wala ushawishi wa mtu au chochote kwakua unakuwa na ushahidi wa kutosha sana ambao moyo wako unakushuhudia kuwa uko salama na sifa kubwa katika maaamuzi haya uwa haya ambatani kabisa na uzushi kwakua kile unachokifanya unakiamini.

Haya ni maamuzi yanakufanya kuwa mkweli na kuwa halisi sana katika kile unachoamua na bila shaka dhamira yako inakuwa haina hatia kwakua kile unachokiamua ni kwa ajili ya kujenga wakati wako katika uzuri.

Nipende kusema kuwa hakuna maendeleo ya kweli kama ukiwa unaamuliwa mambo yako nawe kisha unafuata na kamwe hawezi kwenda mbele japo utaongeza miaka!

Maamuzi ya kuaamliwa yanakuweka katika maisha ya utumwa ambao hutaweza kutoka katika utumwa huo kama utachukua maamuzi bila ya kuheshimu maamuzi yako binafsi kwakua wewe ndio unatakiwa kuonyesha unaijali na kuithamini kesho yako.

Bila shaka ukiwa unaendelea na utumwa wa maamuzi sio rahisi kuungamanishwa na Mungu hata kama ahusiki mkumbuke adamu hata alivyojitahidi kujitetea lakini hakusikizwa tena kwakua Alisha kula tunda ambalo Mungu aliigiza lisiliwe lakini yeye katika ushawishi wa mwanamke ambaye Mungu mwenyewe aliluhusu awe nae.

Mungu amekupa akili akaweka wazo na akakupa kuamua hivyo mtendee haki Mungu kwakuendeleza kile alichokianzisha ndani yako!!!

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni