UNASIKIA NINI?
“ kama wakisikia na
kunitumikia, watapisha siku zao katika kufanikiwa na miaka yao katika furaha”
Ayubu 36:11
Ikiwa neno
la Mungu(biblia) limetoa kipaumbele sana katika kusikia kama chanzo cha ustawi
na ubora wetu basi hakuna shaka jambo hili ni muhimu sana na linatakiwa lipewe
nafasi ya kutosha sana ili tuweze kuona matunda yake.
►Swali?
Unasikia
nini? Na uko na nani? Na huyo ni nani? Yaani anajua nini? Na anafanya nini? Na
anapenda nini? Na kwanini uko karibu yake? Na unapenda kitu gani kutoka kwake?
Na unafikiri ni sahihi katika kutumia muda wako kuwa nae!
Utendaji wa
mwanadamu moja inabebwa na kuchukuliwa katika kiasi kikubwa ni kusikia mtu
awezi kuwa tofauti kama ajambiwa maneno ya tofauti na basi utakuwa wa kawaida
kama tu ukiambiwa maneno ya kawaida na ukayapokea kuona wewe ni sehemu wa hayo
maneno.
Kikawaida
mtu upenda kusikia jambo ambalo masikio yake yatapenda kusikia na hatimae
kuleta kuleta furaha katika moyo wake na jambo hilo hata liwe linamgharimu
kiasi gani kama kipo kwenye uwezo wake basi hata tumia njia yeyote ili mradi tu
aisikie hiyo habari.
Kusikia ni
jambo zuri ila inategemea nini unasikia na kwa nani? Unasikia kwakua matokeo
yake yanaweza kuwa makubwa hata ukashindwa kuelewa kwanini nilifanya vile au
niliamua vile lakini kwa vile ulivyosikia na kuamini.
Naamini
maamuzi yako katika kusikia yanategemea sana upeo wa ufahamu wako katika jambo
hilo ikiwa huna upeo wowote kuhusu jambo hilo unakuwa na shauku ya kujua zaidi
na utekelezaji wake pasipo kujua hili ni jambo sahihi kwa mimi kuwa katika
kufikia hatua hii.
Ningependa
ujue kuwa jambo lolote unalolisikia jua lina nafasi katika maisha yako kwa
kadili kila siku unavyosikia na ndivyo inavyozidi kujijenga na kama nyumba
kadili unavyojenga basi unaongeza hatua katika kukamilisha nyumba hiyo na
utakavyoendelea basi hapana shaka kunakipindi utafikia lile hitimisho.
Watu wengi
wamejikuta katika matatizo makubwa kutokana na kusikia sehemu (chanzo) kisicho
sahihi na hatimae kujikuta katika mazingira magumu kama kufiwa, kuachwa na hata
kuteseka maisha yake…. Ni kweli kama unataka kulinda afya yako basi hauna budi
kuwa makini sana na kile unachokisia kwani kinaweza kukuongezea hofu au mashaka
na hatimae kujikita kudumbukia katika shimo ambalo litaleta majuto katika maisha
yako.
Watu wengi
waliofanikiwa walikuwa wangalifu sana na jinsi walivyosikia katika kusikia
kunakuwa na nguvu ya utendaji na hata walishundwa kufanikiwa walichangiwa sana
na namna walivyosikia na hatua waliochukua.
Wako watu
walikuwa watu wazuri sana lakini kutoka na kusikia kusiko na chanzo sahihi basi
wamejikuta wakiuchukua maamuzi ambayo mwisho wamekuwa wakilia mathalani
mwanafunzi alikuwa na tabia nzuri lakini baada ya kukutana na marafiki zake wakampa habari isiyo sahihi nae
akajikuta anadumbikia huko na hatimae anaishia kupata ukimwi au mimba. Pia wako
watu walio kuwa wakifanya kazi pamoja lakini kutokana na ushirika na wenzake
akajikuta kusikiliza sana na kuwaamini wenzake hatimae akajikuta anakosa kazi
na wenzake wanaendelea na kazi.
Sio mbaya kusikia
lakini nini unasikia ni muhimu sana na kwa nani unasikia nalo ni muhimu zaidi…….
Kwakua tendo lolote unaloliamua linamchango katika maisha yako katika upande wa
faida na upande wa hasara.
Unapomsikiliza
mtu na kukuacha njia ya panda uwa nafasi ya kutengeneza hawezi kukusaidia zaidi
sana anaweza kukuona wewe ni mjinga usio jitambua! Hivyo aibu inakuwa kwako na
familia yako na yeye anakuwa na maisha yake.
Kuna watu
wanashangaza sana unakuta mtu anashawishika na kukubaliana na kufanya jambo
hilohilo na kuona madhara yake baadae unakuta tena amejikuta
palapale…………mathalani mabinti unakuta kapata mimba ya kwanza kwa kudanganywa na
baada ya muda kidogo unakuta ana mimba nyingine.
UPEO WA
UFAHAMU ndio kinga tosha katika kukuepusha na jambo lolote unalo lisikia katika
kulipa nafasi katika utendaji katika maisha yako.
Kama
unajipenda sana basi haun budi kuongeza upeo wa kuyaelewa mambo katika fahamu
zako ili uwe salama na sio kuishia
kuupendezesha mwili na kujikuta ukidumbukia katika mtego hulehule wa siku zote
katika maisha yako.
►UNAJIPENDEZA MWILI NA KUUTUNZA BASI HAKIKISHA PIA UFAHAMU WAKO UNAPENDEZA
NA KUNG’AA KATIKA KUKUPA USHINDI KATIKA CHANGAMOTO ZINAZO KUKABILI.
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson………………………………………………0764 018535