KANUNI
Unapoona mbegu inawekwa
na kuchipua katika ardhi hapo wewe unajifunza nini? Na unapoona yai la kuku na
baadae kutoa kifaranga na hapo unajifunza nini? Na pindi unapoona mchana
unakuwa usiku je! Hapo unajifunza nini? Na pia unapoona bahari ikipungua maji
na baadae yakiongezeka wewe hapo unaelewa nini?..............sina shaka
kichwani mwako kuna majibu mengi ambayo hayana ushawishi wa ulimi katika
kutamkwa kwakua hakuna uthibitisho wa masikio toka nje!
Kiufupi hapo nazungumzia
KANUNI AU UTARATIBU AMBAO MUNGU AMEUWEKA
DUNIANI na kamwe hakuna binadamu anaweza kutengua pasipo idhini yake yani
kufanya tofauti na alivyoamuru yeye.
Unaweza ukachezea vitu
vyote na bado ukawa salama au ukaweza kurekebisha lakini kamwe sio KANUNI na unaweza kuwadanganya watu
maelfu lakini kamwe uwezi kudanganya kanuni au kufanya tofauti na kanuni na
ukapata jibu lililo sahihi…………. hata hesabu ni muhimu uielewe KANUNI na
kuifuata ndipo upate jibu lililo sahihi tofauti na hapo kosa hapo ni haki yako.
Katika dunia kila kitu
kina kanuni yake ili uweze kukipata na kamwe uwezi kuchanganya kanuni na bado
ukategemea kupata kile kilichosawa na kanuni hiyo, na kubaliana kabisa kwamba
kuna kanuni za Mbingu na kuna kanuni za dunia japo kwa kiasi kikubwa yeye
aliyeweka kanuni za Mbingu ndie aliye wapa wanadamu neema ya kuweka kanuni za
duniani.
Kama ilivyo darasani
watu wengi sana wanakosa hususa somo la hesabu kwasababu hawajui kanuni ndivyo
watu wengi wanaangukia sehemu mbaya kutokana na sababu kuu mbili moja hawaijui kanuni au hawaifuati kanuni na
pengine hawajaielewa kanuni. Pia Kanuni inaweza
kuwa ni moja lakini jibu likachelewa kupatika kutokana na wepesi wa ufahamu wa
mtu.
Niseme tu unaweza
kuwashawishi maelfu wawe upande wako lakini kamwe uwezi kuishawishi kanuni
ikafuata upande wako tofauti na asili yake, ni ukweli utafanya lakini utakesha
pasipo matunda yake au sawa na ile nguvu uliyoitumia.
Unaweza ukafanya jambo
watu wote wakakufichia hilo jambo lisijulikane na mtu mwingine zaidi ya wale
waliokuona au walio shiriki lakini kamwe hauwezi kuificha kanuni isifanye kazi
yake mathalani unaweza ukafanya mapenzi na mtu na kwa bahati ukashika
mimba(msichana) lakini utaki watu wajue kuwa ulishiriki ilo tendo na hivyo
ukatumia kila njia ili isijulikane lakini mwisho kanuni ikichukua na nafasi na
mtoto akaanza kuumbika ndani yako bila shaka kwa mtu mwenye akili nzuri ambaye
hata waza mawazo ya kutoa mimba basi itajulikana tu kutokana na muonekano mpya
wa mwili wako.
Niseme kama kuna mtu
ambaye hana huruma kabisa basi huyo anaitwa KANUNI kwani yeye ajui huyu ni adui
wala rafiki bali yeye ufanya sawa inavyotakiwa pasipo kuhofia kitu chochote na
ukitaka kuabika nenda tofauti na kanuni alafu ujifiche katika nafasi uliyo nayo
uone jinsi kanuni itakavyo kukuabisha na
kukuweka hadharani kila kitu pasipo kujali nani anakuheshimu au hakuheshimu.
Unapomwangalia mtumishi
wa Mungu Daudi alipotembea na mke wa mtu alijaribu kuficha kila hali lakini
kanuni haikumuacha ikamfichua na kumgharimu kwa kile alichokifanya pasipo
kujali yeye alikuwa ni chaguo la Mungu au la wanadamu.
Ukitaka kuwa mtu
unayeenda sawa na hali stahiki basi haunabudi kuipenda KANUNI na kuifuata
katika ufahamu ulio sahihi, ukifanya kanuni kuwa ni rafiki yako bila shaka wengi
watakufuata kwakua kanuni ikikuweka mahali fulani kamwe hakuna mtu atakaye
kushusha.
HAKUNA ALIYE MBABE MBELE YA KANUNI
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson……………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni