HATUA YA MWISHO
Mwisho wa safari ndicho chanzo sahihi kwa mtu kuwa na furaha
au huzuni………..na zungumzia mwisho uliobeba hitimisho jema lenye matumaini mema,
unapoangalia kule ulikotoka na kule unakoelekea ndipo panaweza kutoa hali yako
ya furaha au huzuni. Na kuna mambo ambayo unaweza usijue huu ndio mwisho au
ndio mwanzo………mathalani Samson alipoojitoa kwa ajili ya ndugu zake Israel ila
kifo chake akikuwa na tafsiri sahihi katika ufahamu wa ndugu zake ila baada ya
kifo basi tafsiri sahihi ikajitokeza baada ya kuona adui zao hawapo tena.
Ni nguvu na ni faraja ya pekee isiyoweza kufutika katika moyo
wako katika majeraha na mateso katika maisha yako pindi unapoona au kufikia
hitimisho lililobeba ndoto zako katika maisha ya ustawi wako.
Hitimisho nzuri ni kitu pekee kinachoweza kufuta macho yanayolia
ndani moyo wa mtu na ni dawa inayotibu majeraha ya moyo wako. Na ni nguvu
inayokupa fursa ya kuendelea mbele pasipo kuchoka………….!
Hiki ni kipindi ambacho afya ya mwili uweza kurejea katika
maisha yako tena kwa kasi isiyo ya mfano na watu wengi kuanza kurejea tena
kwako tena katika hali ya kuona umuhimu kwa namna nyingine isiyoelezeka………!
Katika hatua hii wako watu wanaweza kufanya jambo ambalo kwa
hakika akuwai kufanya katika maisha yako au kuzidisha katika hali isiyo ya
kawaida matahalani mtu anaweza kusema kwa furaha niliyokuwa nayo leo na amua
kulala nje na haikuwa mzoea yake na wala sio kwa sababu nyingine bali kwa lile
burudiko katika maisha ya mtu husika.
Uwa ni vizuri sana pindi unapoanza safari au jambo huku ukiwa
na furaha lakini hiyo furaha italeta maana kwako na kwa wengine yaani jamii
inayokuzunguka kama mwisho wako utakufanya uwe na furaha mara dufu yaani kuliko
mwanzo lakini pindi mwisho utakuwa ni wa huzuni bila shaka wewe binafsi utaona
kwanini ulikuwa na furaha mwanzo wa safari na hata watu wanokuzunguka hawataona
kwanini wewe ulikuwa unacheka wakati mwisho wa safari umekuweka katika
mazingira mabaya, …….jamii inaweza kuwa na maswali mengi lakini bila shaka wewe
kwako yazidi kwakua kile ulichokitegemea hakikua sawa na ulivyotegemea.
Laiti tungekuwa tunajua mwisho kabla mwanzo basi mambo mengi
tunayofanya kipindi cha mwanzo au cha awali tusingeyafanya kabisa au
kuyapunguza.
Napenda kusema kuwa furaha ya maana sana ni mwisho uliobeba
hatma njema katika maisha yako inayotoa mwanga na matumaini yaliyobeba usalama
wa kesho yako. Siku zote watu wanapenda kuona taabu zao za leo zisiendelee
kesho ndomana wanasema mchumia juani ulia kivulini wakiwa wana maana kabisa
baada ya dhiki ni faraja!!
Hatua ya mwisho ni kipenzi cha watu wengi……..hata katika
stori yoyote mtu anapobaini kuwa mwisho wa hiyo stori hauta furahisha moyo wake
huwa hana haja ya kusikiliza hiyo stori kwakua haivutii kuendelea kusikiliza
baada ya kubaini au kundua mwisho wa hiyo stori hauta ufurahisha moyo wake.
Unaweza kumkuta mtu anavumilia katika mazingira hatari au
magumu na hata kushindwa kujua kwanini mtu anajisumbua kwanini asiache tu
akafanya mambo yenye maana kubwa lakini pamoja na wewe kuona hivyo utakuta mtu
bado anaendelea na uwa anaongeza bidii sana pindi anapoona kuwa mwisho wa jambo
lake au safari yake utakuwa ni matumaini au mwanzo mzuri wa watu wengine.
Hatua ya mwisho ni jambo zuri sana kwani linakuwa ni
hitimisho la mwendo mzima wa maisha yako na ndio kitu pekee kinachoweza kufuta
maumivu yote ya nyuma na kukupa mwanga mwingine katika maisha yako…………niseme
wazi kama kunakitu ambacho kitakufuta machozi na simanzi katika yote uliyopita
ni kuona mwisho wenye ushuhuda au uliobeba ustawi uliojitosheleza katika ubora
na uzuri.
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni