Jumanne, 29 Machi 2016

SAUTI YA MOYO



SAUTI ADIMU


 Kwa tafsiri rahisi pindi unaposikia neno ADIMU unapata picha gani katika fahamu zako? Inawezekana ukatoa tafsiri ya kitu ambacho ni nadra kuonekana, au kitu chenye thamani kubwa ambacho sio watu wote wenye uwezo wa kumudu kukimiliki kitu hicho.

Na pindi unaposikia SAUTI ADIMU bila shaka sasa akili yako inaanza kupata picha ya kufikirika, je! hiyo sauti ni ya mtu au ya mnyama na ni wanamna gani kama sauti ya mtu basi bila shaka inawezekana kuwa ni ya mtu ambaye ni nadra kupatikana au kuonekana na anaweza kuwa ana umaalum fulani mathalani rais, superstar na nakubaliana kabisa sauti inaweza kuwa adimu kwako lakini sio kwa watu wote kwakua wengine inawezekana wanaisikia kila siku lakini kwako inawezekana kuwa ni adimu.

Kwa upande wa wanyama tunaona sauti ya wanyama  ni adimu kwa wengi mathalani tembo,chui,mbwea na wengine wengi lakini kwa upande mkubwa sauti ya simba imepewa nafasi ya upekee na kuitwa kuwa sauti yake ni adimu na pindi unapoisikia lazima upate bumbuazi kwani mnyama huyu utoa sauti yake inasikiwa katika hali ya kunguruma hivyo kishindo cha sauti yake inaleta bumbuazi katika jamii husika.

Lakini hapa nazungumzia sauti adimu iliyo ndani ya mwanadamu, niseme wazi kuwa unaweza kuwa mtu na kila siku ukazungumza nae lakini ukweli unabaki ndani yake na binadamu anapozungumza uwa sauti mbili zinazotoka ndani yake iko sauti ya kinywa iliyombatana na matumizi ya akili na iko sauti ya moyo ( sauti adimu)

Sauti adimu ni sauti iliyobeba udhati wa mtu, ndani yake iliyojaa kweli ikisindikizwa na hisia za nafsi inayoakisi udhati wa maisha ya mtu, mtu anayejua kile anachokisema ndivyo kilivyo haijrishi atakosa au atapata kitu chochote.

Niseme kuwa mtu anayeishi maisha haya bila shaka anaishi maisha ya uhuru kweli kwakua ndani yake hakuna hukumu yoyote inayomtafuna, kificho kwake uwa ni mwiko uongea maneno hata ukiangalia macho yake utaona kama kitu kinakutazama

Ukisikia mambo yamebumbulika mara tu baada ya muda mfupi katika jambo lolote jua kwamba MOYO HAUKUZUNGUMZA toka awali na pindi unapozungumza unakuwa katika hali nyingine ambayo kwa ukawaida haiwezi kumudu tena hali ya mwanzo na hapo kuweza kuzua maswali mengi kusema yako mengi bado ajaniambia, kibaya sana kinakuwa ni swali…. hivi kwanini akuniambia mapema? Hivi amenionaje ? kwani mi ni mtu wa kudanganywa? Au kaona mimi sina thamani? Haya maswali ndio yanajaza jazba katika moyo wa mtu na hatimae kuamua maamuzi yanayoweza kuhatarisha maisha yake!

Dunia namna inavyoendelea ndivyo sauti adimu zinazidi kuadimika na kutoa nafasi kwa sauti kinywa kuwa na nguvu zaidi katika kusikika na kushawishi.

Unaweza kukaa na mtu kwa muda mwingi ata anaweza kuwa mwenzi wako lakini unaweza usiisikie sauti yake ya ndani ya moyo wake bali utaishia kusikia maneno ya midomo yake iliyojawa na ushawishi tu! Lakini kamwe usiisikie sauti yake ya ndani iliyobeba uhalisia wake mathalani unaweza kuishi na mwanamke kumbe huyo ni afisa mpelelezi ukawa unakula nae unalala nae siku zote lakini usijue kuwa nini hasa lengo lake la kuwa na wewe, nasio lazima awe afisa mpelelezi hata anaweza akawa mtu wa kawaida lakini anaweza kutotoa ya moyoni mwake kwako kwa kuhofia maisha yake au wewe utamuacha na mengine mengi.

Ni kweli kusema kwa mtu na kuambia ukweli kabisa hivi ni vitu viwili katika dunia ya leo visivyoambatana kabisa imebaki katika maneno tu lakini ukweli anao muhusika mwenyewe na sio mtu mwingine na hasa katika dunia ya leo mashaka yalivyo mengi na mashafu yaliyo mengi na mwisho ukigundua kuwa ulikuwa mdomo tu na haukuwa moyo ukisema unaweza kuwa katika hali nyingine inaweza kuwa ni hali mbaya.

►Unapokuwa na mtu tamani sana kusikia sauti adimu toka kwake kuliko sauti ya kinywa kwakua sauti ya kinywa haija beba uhalisia wa moyo wake kwakua kamwe hauwezi kwenda mbele na mtu ambaye yale anayoyaongea sio ya kweli mkadumu nae.

Ni bora uwe na mtu ambaye ni bubu au mlemavu kuliko kuwa na mtu ambaye ni mzima ambaye ana matumizi ya sauti adimu kuliko kuwa na mtu ambaye ana matumizi maneno ya kinywa tu, kwani ulimi unaweza kupindua mambo makubwa na mazito na hasa yale usiyoyategemea yaka fanyika.

Usipate hofu unapokuwa upande wa Mungu yeye atakufulia yaliyo ujaza moyo wa mtu hata kama yeye hayuko tayari kukuambia kwakua Mungu atasimama nawe ili uwe salama siku zote.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………….0764 018535

MWAMINI MUNGU UWE SALAMA

Jumanne, 22 Machi 2016

THE RIGHT TIME IS THE BEST TIME



WAKATI SAHIHI




Ni swali la kawaida mtu uweza kukuliza kuwa jambo unalolifanya sasa unafikiri ni wakati sahihi wa wewe kulifanya jambo hili? Au unafikiri mahali upo unafikiri ni wakati sahihi wa wewe kuwa hapo? Hama Unafikiri rafiki uliye naye sasa ata kufaa kwa wakati huu? Bila shaka jibu lake litaamliwa na utashi wa nafsi yako.

Naomba niseme kuwa kunatofauti kubwa kwa mwembe kutoa maua na kutoa embe hivyo naweza kusema kuwa maua sio maembe japo tunaita kuwa mwembe kutoa maua kuwa ni dalili nzuri ya kutoa maembe! Ila kuna utofauti mkubwa sana na kamwe hauwezi kuzifananisha ndomana …………kuna dalili ya mvua na mvua yenyewe kunyesha!

Dalili kubwa ya watu kuwa  hawajui wakati sahihi ni ugomvi miongoni mwao katika kugombania kitu fulani katika maisha yao lakini wanaotambua wakati uwa na busara katika maamuzi yao japo wakati mwingine unaweza kuona kama mtu huyo yuko nje na wakati au ajitambui.

Hichi ni kitendawili kwa watu wengi katika kujua hasa WAKATI SAHIHI kwangu ni upi? Wako watu waliopata kazi wakajua sasa ni wakati wangu wakijinafasi ghafla akafukuzwa kazi na kujikuta anarudi katika hali ya mwanzo, yuko mtu baada kuona huduma iliyo ndani yake inachemka na kuona ishara na maajabu zinaanza ambatana katika maisha yake basi akafikiri huo ni wakati sahihi wa yeye kufungua kanisa na mwisho akaona tofauti na vile alivyowaza akaamua kuacha na kujiingiza katika shughuli zingine, pia tusisahau kuwa kunatofauti kati ya muonekano mzuri na akufahae katika maisha yako.

►Ninapozungumzia wakati sahihi naweza kuita kuwa ni fumbo la moyo, mshangao wa akili au mgongano wa malengo katika kuleta usawa wa hatua katika hali ya umoja na katika ustawi!
Nipende kusema kuwa wakati sahihi sio kama hatua za bidamu katika kukua mathalani utoto, ujana na uzee au utu uzima bali uja kwa namna yake utegemea sana ratiba ya Mungu kuliko malengo yako kuwa unataka kuwa nani?

Bila shaka wakati sahihi uweza kuwa ni usiku wa giza wenye joto lisilotoa fumbo kuwa wakati gani litaishia…… uja kwa namna yake na uweza kuimarika kwa namna yake bila shaka italeta mshangao wa akili unaweza kusema wakati wote walikuwa wapi?

Wakati sahihi hautaji sana maandalizi ya akili au ya mwili ila utakapofika wenyewe utaandaa mwili wako kuupokea na akili kuwa sawa na wakati ulivyo kwani wakati unapofika na mazingira ujikusanya bila shaka unakuwa unakuwa umebeba hazina ya kutosha sana hivyo inakuja kukamilisha kila kitu kinachotakiwa.

Kama kuna kitu kibaya kukosea ni wakati endapo utatumia wakati tofauti na ulivyo ni wazi itakugharimu na sio wakati wenyewe, ni seme hakuna raha na furaha ya kweli tofauti na kufanya jambo katika wakati uliomuafaka kwani kila kitu kinakuwa tayari.
Nikubaliane kuwa katika kuutambua wakati sahihi ni swala gumu na zito kwasababu alihusishi sana utendaji wa juhudi binafsi bali uja kwa mikakati yake na wakati mwingi hata njia yake uwezi kuijua hivyo hautaji kusukuma wakati kwa akili na kujipa furaha ya muda isiyo na msingi wa kuendelea katika ubora.
Kunaweza kuwa ni wakati sahihi wa watu wote lakini isiwe ni wakati sahihi kwako hivyo lazima ukubaliane na hali hiyo na kujua kwamba wakati wako upo na pindi utakapofika basi bila shaka kila kitu kitakuwa wazi pasipo usaidizi mwingine.

Wakati wa kuchanua ukifika umefika tu maadamu uko katika mazingira ya kuruhusu hali hiyo itokee katika maisha yako lazima ujue kuwa sio kila wakati ni wako bali wakati wako sio watu watautamani bali utakuwa ni ushindi katika maisha yako, hautaji ujitambulishe bali wakati wenyewe utajitambulisha.

Matendo ya Mitume 13:22 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.

Lazima utambue wakati bora kwako ni wakati sahihi ambao hautaji kuwaza sana bali wenyewe utakuja na kukupata pale ulipo kwani kwa yeye hakuna kizingiti ambacho kitashindwa kutii mamlaka yake.

Lazima utambue kuwa wakati sahihi utakapofika utakujia pale ulipo hauna haja kuwaza na kuufikiria wakati wote na hata kushindwa kuyafanya yale uliyotakiwa kuyafanya katika ubora wake.

Marko 8:36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Ni vizuri utambue wakati sahihi umewekwa na Mungu hivyo ni vizuri uwe katika wakati huu ukiwa ndani ya KRISTO kwa maana ndani yake hakuna majuto na utautumia wakati wako vizuri utawafaidia wengine na wewe utapata neema zaidi na zaidi sana ufalme wa Mungu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………..0764 018535

THE RIGHT TIME IS THE BEST TIME

Jumanne, 1 Machi 2016

MUNGU AHITAJI UMSAIDIE

MUNGU AHITAJI UMSAIDIE


Kama kunakitu ukikifanya kitavuta watu wengi kuja kwako, hata wale uliofikiria kuwa itakuwa ngumu kuja kwako au kukukubali, naam hichi kitu kinachoweza kubadilisha adui yako akawa rafiki……… na pengine unaweza kuona moyo wa mtu ukizungumza juu yako, unaweza kukuta mtu anashikwa na kigugumizi na machozi yakaongea na hilo sio lingine bali ni  ASANTE KWA MSAADA!

Katika hali ya kawaida tu msaada unakuwa wa maana sana pale palipo pa uhitaji!!

Ni kweli jambo hili wakati mwingine  limekuwa likitumika sana katika upande usio sahihi pale ambapo mtu anapokuwa na shida ya kitu au uhitaji wa kitu fulani basi hapo ndipo anaweza saidia mathalani kijana anapomtaka binti basi hapo uweza kujitaidi kila hali ili kuhakikisha tu huyo mtu aliye naye aone kuwa yeye ni msaada kwake na wala sio kero au mzigo kwa muda tu mara tu atakapotimiza haja zake basi uweza kuiona njia nyeupe uweza kugeuka upande mwingine mbali na hilo kuna upande wa siasa hasa za kitanzania ila sijui kama kunamabadiliko yatakayotokea japo kwa Mungu hakuna linalo shindikana kwake yote yanawezekana tumekuwa tukiona misaada mingi ikitolewa kipindi wagombea(wako watu wanajenga na wengine wanasema ni kipindi cha neema) wakiwa wana gombania/wania nafasi mbalimbali katika uongozi nchini basi hapo uweza kutoa misaada mashuleni, hospitali, na katika jamii kwa ujumla yote ni katika kulainisha mioyo yao ili waweze kukubaliana na lengo analolikusudia.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa mtu yeyote katika kumsaidia mtu au kundi la watu na pindi anapogundua mtu huyu anakwenda kinyume na matarajio yake au kuona hile dhima yake haitafanikiwa hapo haoni shida kukatisha msaada wake ghafla maana anaona atakuwa anapoteza muda kupalili mti ambao matunda yake hawezi kula.

Kwakifupi tunakubaliana na msemo huu hakuna mtu anakusaidia bila sababu yake au bila msukumo ulio nyuma ambao umejaa masilai binafsi!!!!

Ila yuko mmoja ambaye anaweza kukusaidia sio tu kwa masilai yake tu bali katika ustawi wa maisha na mwendelezo uliobora uliobeba kushamiri katika maisha yako!

MUNGU AHITAJI UMSAIDIE!

Ni jambo la kawaida kwakua kila mtu utambua uweza wa Mungu ni mkubwa na hakuna mbadala wake na kamwe hakuna kitu kinachoshindikana katika kwake……………..japo kunatofauti kubwa kati ya kuelewa na kuyaishi hayo unayoyaelewa.

Niseme tu hiko hivyo hivyo kama alivyosema kwamba haitaji msaada wowote kwako zaidi ya kumsikiliza na ufuate njia zake na ajidhihirishe katika maisha yako

Mathayo 6:27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

Mungu kutohitaji msaada wako haina maana kuwa usitumie maarifa ambayo Mungu amekupa au hadhina ambayo Mungu ameweka kupitia njia zake shule, busara za wazee na njia nyingine zilizo sahihi katika kuyaimarisha maisha yako.

Lakini swala hili limekuwa tatizo kwa wengi kujitahidi kwa hali na mali kutimiza hadhima zao zilizo ndani katika maisha yao pasipo kuangalia au kufuata maelekezo sahihi ya Mungu……..mathalani mtu anasema bila kukesha hauwezi kumpendeza Mungu!,bila kutoa sana hauwezi kugusa moyo wa Mungu na bila ya kuomba sana kamwe hawezi kufanikiwa, na wengine uweza kusema bila ya kujiweka mbelembele hauwezi kujulikana kwa mchungaji,

1 Samweli 15:22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Sina shida katika kufanya haya lakini swali langu kwako haya yote ni katika msukumo wa nje au wa ndani maana kila msukumo unamshikilio wake…….. uwa vitu havifanyiki maadam vipo bali kuna msukumo unatoka ndani yako katika ujazo wa kimungu kwa uhalisia wake au la!

Uwa kazini huwa haulipwi kwasababu unafanyakazi bali ni kwa vile unafanya kazi hile uliyopewa!
Sina ugomvi na kutumika bali natamani utumike kwa faida

 Isaya 48:17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

Sina haja ya kukuvunja moyo bali nataka ni kwambie ukweli unahitaji kuwa na Mungu ndani yako na sio wa kusikia wala wakuhisi wala wamapokeo bali yeye yuko halisi mwache awe halisi katika maisha yako ili ufurahie maisha yako ya wokovu.

Imeandaliwa na:


Cothey Nelson…………………………………………………………………..0764 018535