Jumanne, 1 Machi 2016

MUNGU AHITAJI UMSAIDIE

MUNGU AHITAJI UMSAIDIE


Kama kunakitu ukikifanya kitavuta watu wengi kuja kwako, hata wale uliofikiria kuwa itakuwa ngumu kuja kwako au kukukubali, naam hichi kitu kinachoweza kubadilisha adui yako akawa rafiki……… na pengine unaweza kuona moyo wa mtu ukizungumza juu yako, unaweza kukuta mtu anashikwa na kigugumizi na machozi yakaongea na hilo sio lingine bali ni  ASANTE KWA MSAADA!

Katika hali ya kawaida tu msaada unakuwa wa maana sana pale palipo pa uhitaji!!

Ni kweli jambo hili wakati mwingine  limekuwa likitumika sana katika upande usio sahihi pale ambapo mtu anapokuwa na shida ya kitu au uhitaji wa kitu fulani basi hapo ndipo anaweza saidia mathalani kijana anapomtaka binti basi hapo uweza kujitaidi kila hali ili kuhakikisha tu huyo mtu aliye naye aone kuwa yeye ni msaada kwake na wala sio kero au mzigo kwa muda tu mara tu atakapotimiza haja zake basi uweza kuiona njia nyeupe uweza kugeuka upande mwingine mbali na hilo kuna upande wa siasa hasa za kitanzania ila sijui kama kunamabadiliko yatakayotokea japo kwa Mungu hakuna linalo shindikana kwake yote yanawezekana tumekuwa tukiona misaada mingi ikitolewa kipindi wagombea(wako watu wanajenga na wengine wanasema ni kipindi cha neema) wakiwa wana gombania/wania nafasi mbalimbali katika uongozi nchini basi hapo uweza kutoa misaada mashuleni, hospitali, na katika jamii kwa ujumla yote ni katika kulainisha mioyo yao ili waweze kukubaliana na lengo analolikusudia.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa mtu yeyote katika kumsaidia mtu au kundi la watu na pindi anapogundua mtu huyu anakwenda kinyume na matarajio yake au kuona hile dhima yake haitafanikiwa hapo haoni shida kukatisha msaada wake ghafla maana anaona atakuwa anapoteza muda kupalili mti ambao matunda yake hawezi kula.

Kwakifupi tunakubaliana na msemo huu hakuna mtu anakusaidia bila sababu yake au bila msukumo ulio nyuma ambao umejaa masilai binafsi!!!!

Ila yuko mmoja ambaye anaweza kukusaidia sio tu kwa masilai yake tu bali katika ustawi wa maisha na mwendelezo uliobora uliobeba kushamiri katika maisha yako!

MUNGU AHITAJI UMSAIDIE!

Ni jambo la kawaida kwakua kila mtu utambua uweza wa Mungu ni mkubwa na hakuna mbadala wake na kamwe hakuna kitu kinachoshindikana katika kwake……………..japo kunatofauti kubwa kati ya kuelewa na kuyaishi hayo unayoyaelewa.

Niseme tu hiko hivyo hivyo kama alivyosema kwamba haitaji msaada wowote kwako zaidi ya kumsikiliza na ufuate njia zake na ajidhihirishe katika maisha yako

Mathayo 6:27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

Mungu kutohitaji msaada wako haina maana kuwa usitumie maarifa ambayo Mungu amekupa au hadhina ambayo Mungu ameweka kupitia njia zake shule, busara za wazee na njia nyingine zilizo sahihi katika kuyaimarisha maisha yako.

Lakini swala hili limekuwa tatizo kwa wengi kujitahidi kwa hali na mali kutimiza hadhima zao zilizo ndani katika maisha yao pasipo kuangalia au kufuata maelekezo sahihi ya Mungu……..mathalani mtu anasema bila kukesha hauwezi kumpendeza Mungu!,bila kutoa sana hauwezi kugusa moyo wa Mungu na bila ya kuomba sana kamwe hawezi kufanikiwa, na wengine uweza kusema bila ya kujiweka mbelembele hauwezi kujulikana kwa mchungaji,

1 Samweli 15:22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Sina shida katika kufanya haya lakini swali langu kwako haya yote ni katika msukumo wa nje au wa ndani maana kila msukumo unamshikilio wake…….. uwa vitu havifanyiki maadam vipo bali kuna msukumo unatoka ndani yako katika ujazo wa kimungu kwa uhalisia wake au la!

Uwa kazini huwa haulipwi kwasababu unafanyakazi bali ni kwa vile unafanya kazi hile uliyopewa!
Sina ugomvi na kutumika bali natamani utumike kwa faida

 Isaya 48:17 Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

Sina haja ya kukuvunja moyo bali nataka ni kwambie ukweli unahitaji kuwa na Mungu ndani yako na sio wa kusikia wala wakuhisi wala wamapokeo bali yeye yuko halisi mwache awe halisi katika maisha yako ili ufurahie maisha yako ya wokovu.

Imeandaliwa na:


Cothey Nelson…………………………………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni