Jumanne, 23 Februari 2016

NGUVU ILIYOPO KATIKA UTULIVU



NGUVU ILIYOPO KATIKA UTULIVU


Wepesi wa macho sio uzito wa mizizi!

Usione mti umetulia tu ukadhani ni rahisi nitauangusha! Usipokuwa makini unaweza kuchukua miaka mingi pasipo kupata jibu…….na kubaki na swali pasipo muafaka kuwa mti huu hivi utaanguka lini?

Iko misemo mingi mizuri na ya kushawishi masikio ya watu na kivutio cha macho ya watu na kuna wakati mwingine misemo/methali hizo zinakuwa na uhalisia katika jamii yetu mathalani harakaharaka haina Baraka, polepole ndio mwendo, mvumilivu ula mbivu na nyingine nyingi na zote ziki husisha  hali sahihi katika kuamua maamuzi yoyote na nyingi zikilandana na methali hii fikiri kabla ya kutenda bado ikilalia sehemu inayoitwa tatua jambo katika njia muafaka na sio kwa kukulupuka.

Ndomana maamuzi ya vijana wengi hayathaminiki kama ya wazee kwani haya maamuzi yana aminika kuwa ndani yake hakuna umakini kama ya wazee na pia yana amini kuwa hayajakomaa au hoja zao hazina shibe/mshiko kwa kiufupi hoja zao hazina uhalisia katika maisha wanaoishi na moja ya sifa kubwa ambayo inaaminiwa sana na maamuzi ya wazee ni kuwa na hekima yanaangalia mbali sana, japo pamoja na hayo kunaweza kuwa na kasoro katika upande wa mawazo ua wazee mathalani yakawa ni mawazo yasioendana na mabadiliko ya sasa( mawazo mgando) bila shaka iliutambue hili unahitaji mawazo mapana yaani mawazo yenye utafiti wa uhakika.

Japo kuna mazingira mengine maamuzi ya haraka yanahitajika na hasa katika jambo la haraka linalohitajika utatuzi wa haraka mathali katika vita bila shaka hapo maamuzi ya haraka na yenye akili yanahitajika sana ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kuwa salama na hata kuleta ushindi kwani utambue kuwa makosa yako ndio fursa ya mwenzako!

Na kubaliana kabisa kuwa unaweza kuwa katika hali ya utulivu lakini bado unaweza usiamue jambo la maana kutokana na sababu mbalimbali migandamizo ya mawazo(stress), mshauri wako, nguvu za hisia zako na hasa pindi unaposhindwa  kuzitawala.

Pamoja na hayo nipende kusema kuwa maamuzi sahihi na yenye utendaji wa nguvu kubwa pamoja na kishindo yanayoweza kuleta mabadiliko makubwa ya ajabu sana kusababisha mafanikio makubwa katika maisha yako!

Mwanzo 1:2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi    vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

                 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

Tunaona katika utulivu wa Roho ya Mungu ndio ilikuwa ni hatua ya kwanza ya Mungu kabla ya uumbaji wa kitu chochote japo dunia haikuwa na sura nzuri wala muonekano usio faa, lakini katika utulivu ndani yake ilikuwako nguvu ya kuleta mageuza ambayo ndio imefanya sisi wanadamu tuweze kukaa na kuona fahari ya dunia tuliyonayo.

Tunaona Mungu anatumia siri kuu katika utulivu kufanya mambo makuu atuoni Mungu akiamua tu jambo kwa sababu lipo tu na anaweza kuliamua tu maadamu anayo nafasi na uwezo huo bali alitulia katika hali ya kujua mwisho kabla ya mwanzo na katika hilo tunaona Mungu kushindwa hakutajwi kwake…………….ndomana mwisho tunaona akisema 

Mwanzo 1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana………

Ukweli Mungu anatufundisha siri kubwa hapa na inadhihirika katika hali ya ushindi wake katika kila alichokifanya!

Kiubinadamu hali hii inakuwa ngumu sana unaweza ona mtu kuwa ni mtulivu sana katika muonekano wan je lakini ukweli ndani anafurukuta moto unaotaka kulipuka kwa hiyo muda wowote unaweza kulipuka ni sawa sawa na dumu la petro kupita  mahali ambapo moto unaweka na dumu  likiwa wazi.

Katika mambo yote ningependa kusema utulivu uliobeba akili ya kutosha na dhamira njema ni jambo muhimu sana katika maisha yako kama mkristo inawezekana watu wakakuona unachelewa sana, niseme ni bora wakuone unachelewa sana kuliko uwai badala ya kutengeneza ukajikuta unaharibu.
Nikubaliane kusema ukweli hasira wakati mwingi isipoongozwa na akili iliyo sahihi mwisho wake ni uharibifu au mtokeo yake yakawa chini ya kiwango au hali inayotakiwa.

Niseme utulivu wa kibinadamu hauna matokeo mazuri kwani ni kweli unaweza ukatoa maamuzi ya kuangalia kesho lakini uhakika wa hiyo kesho kuwa sawa na unavyosema au anavyoamini lakini uko utulivu wa kimbingu ambao ukiiwaza kesho kamwe haiwezi kuwa tofauti na vile alivyowaza kwani yeye anaitwa jana leo kesho hata milele na neno lake hakuna kinachoweza kutengua.

Isaya 55:10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
             11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma

Anavyosema ndivyo inavyokuwa na sio kitu kingine!

Umaana wako mbele za Mungu unaanza pale utakapoamua kumbeba Mungu!

Imeandaliwa na: 

Cothey Nelson…………………………………………….0764 018535

BARIKIWA!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni