UNAPENDA NINI KWA MTU?
Kupenda kwa jina rahisi
nimelipa kuwa ni kifungo huru kwa maana hakuna mtu anakuja kukulazimisha kuwa
sasa unahitaji kuingia huku, bali inakuwa ni kwa utashi wako na akili zako
timamu pamoja na msukumo mkali wa hisia zako bila kusahau ikisaidiwa na ndoto
zako katika maisha yako.
Japo siku hizi kiukweli
ni ngumu kutofautisha kiukweli yupi anakupenda kweli au upendo wake sio wa
kweli na kuna wakati mwingine unaweza fikiri kirahisi kuwa huyu mtu kwa namna
anavyonitendea naona hapa kuna upendo wa kweli lakini muda si mfupi unaweza
kubadilisha maneno yako kwa kuona tofauti na akili yako ilivyoamini mwanzo
nakuona kama uko ndotoni au katika mawazo yalikuamisha kuwa ndio huyu kweli au
mwingine kwa namna alivyobadilika hasa katika utendaji wake uliouona mwanzo na
wa sasa unao ushuhudia.
Katika hali ya kawaida
tunaposema KUPENDA tunasema ni haki ya
tu na sio wajibu wa mtu hivyo unahiari ndani yake kuwa naweza kupenda au
nisipende kwani hakuna mahakama au jela utapelekwa kwakua wewe umekiuka kifungu
cha kupenda kanakwamba ni wajibu na wewe ukuutekeleza zaidi sana utaweza
kujikita na kuamini kuwa hili ni jambo la ubinafsi wa mtu! Na sio swala la
kushurutishwa.
Tukiingia katika uwanja
wa kupenda kuna vitu na viona hapo kupenda kunaweza kuzaliwa kutokana na
muonekano wa ndani au muonekano wan je, na muonekano wan je ni rahisi tu kuona
lakini muonekano wa ndani ni ngumu kuona kwa haraka haraka.
Ni
maswali ndani yangu?
►aina kazi uliyonayo
ndio ina amua aina ya mwenzi kuwa naye?
►muonekano ulionao ndio
unaweza kuamua aina ya mwenzi kuwa nae?
►kipato ulichonacho
ndicho kina amua aina ya mwenzi kuwa naye?
►ni kweli mwenzi mzuri
utoka katika familia yenye maadili mazuri?
►na nikipimo gani
unachotumia kugundu mtu huyu ametoka katika familia yenye maadili bora?
►ni kweli umri ni
kigenzo au ni kikwanzo katika mausiano katika ndoa?
►je! Ni kweli muonekano
wa mtu uweza kusadifu tabia ya mtu?
Haya ni baadhi ya
maswali yaliyo ndani katika kichwa changu ni kijaribu kutafuta kwa umakini
uhalisia wa hali hii ni kweli iko hivyo na usawa wa mambo haya na ubora wake.
Basi tukirudi katika
mada yetu kuwa UNAPENDA NINI KWA MTU najua wewe sio chizi wa kupendapenda
hovyohovyo hata kama umechelewa kuwa na mwenzi na pia hata chizi naye anachagua
sio kila mtu uweza kumtupia takataka bali kwa wale atakao wachagua.
Ningependa kuongelea
muonekano wa ndani?
Hali hii unaweza
kumtambua mtu katika kuongea na mwitikio katika katika changamoto anazozikabili,
wako wengi uweza kuvutiwa namna mtu
anavyokuwa kimya anaposemwa vibaya basi hali hiyo uweza kupelekea kuwa ikitokea
mtu huyu akiwa mwenzi wangu basi bila shaka atanisikiliza mahitaji yangu na
kunifanyia sawa ninavyopenda na hatimae tutaishi maisha ya raha mstarehe na
hapo ikawa chanzo cha mausiano.
Napia ninapoongelea
muonekano wa ndani wa ndani uwa naongelea rutuba ambayo mtu aliyonayo ndani
yake ambayo pindi inapotoka inaweza kuwa ustawi wa watu wengi na wengi waka mea
kutokana na rutuba toka kwa mtu.
Ni kweli hali ya ndani
ya mtu imekuwa kivutio kwa wengi pasipo kujua ili uweze kumjua mtu vizuri
unahitaji kuchukua muda katika kuishi nae ukaona kwa undani tabia kujua hii
ndio halisi au sio halisi watu wengine wamekuwa wakigundua baada ya kufanya
maamuzi tayari na kujikuta kuingia katika shimo lisiloweza toa uwezekana
wa kutoka inategemea na imani yako.
Si katai mtu kuvutiwa
kwa mtu katika hali mbalimbali mathalani mcheshi, mkarimu, mwenye upendo,
mwenye huruma na hata busara ningependa kusema kuwa binadamu kama huyo wako
wengi japo kiukweli natambua kuwa hakuna mfanano wowote wa utendaji wao.
Kwa dunia ya sasa
muonekano wa ndani ushawishi wake ni mkubwa lakini ukweli unaweza kuwa sio
sahihi kwani mtu anaweza kuficha makucha kwa muda lakini mwisho akayachia baada
ya kuishi kama mke na mme.maumivu yake uyasikiage kwa mwingine kwani yakikuta
utaona afadhali moto wa jehanamu japo ujawai kuona wala kuhuhisi kuliko kuishi
na mtu aliyachia makucha mara tu baada ya kuingia ndani.
Niseme ulimwengu wa
wapendao ni ulimwengu unaobadilika kwa kasi kubwa lakini ushindi wako
unategemea uwezo wa nguvu uelewa wa mambo hayo na ungamaniko la kweli kati yako
na Mungu.
Ushauri wangu
kwako..USIMPENDE MTU ZAIDI YA KUYAPENDA MAONGOZI YA MUNGU!
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson…………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni