Jumanne, 9 Februari 2016

USIISUMBIKIE KESHO



USIISUMBIKIE KESHO

 Kila mtu utamani sana kuwa na kesho,na sio bora kesho tu bali kesho nzuri yenye ushawishi na mvuto kwa wengine na iliyobeba maswali yake ya leo mathalani kuwa na nyumba, maisha yenye furaha na mwenzi sahihi na mengine mengi….. kwa hakika ni kitu kizuri kwa mtu yeyote mwenye akili njema sana ni lazima awaze mambo kama haya kwakua ndiko huko anakoelekea ……….na unaweza kuwa katika hali njema sasa kwa maana mke mwema, watoto wazuri nyumba nzuri na bila shaka na usafiri wa maana lakini bado utahitaji kuona kesho yako ikiwa njema sana kuliko leo, naamini bado utamani kuona ustawi watoto wako katika elimu, mali na kuishi maisha ambayo yatampendeza Mungu kulingana na imani yako na matarajio yako binafsi kwa kusema hivyo ni seme kesho inatofautiana kulingana na leo yako uko katika hatua ipi?.

Sio ajabu kuona watu wakichukua maamuzi ya kuhatarisha maisha mara baada ya kuona mwanga hafifu au giza katika kesho yao unaweza kukuta mtu anaingia katika shughuli ambazo zita hatarisha maisha yake na hata kupelekea ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha yake lakini dhamira yake ni kuilinda kesho yake au kuifanya kesho iliyo na manufaa kwake,

Ukitaka kumtambua mtu katika upande mwingine basi ukute mtu anaona njia iliyo bora katika kufikia kesho yake lakini wewe ukasimama na kuwa kizuizi katika njia yake, hapo utaweza kuona namna mtu huyu anavyoweza kuziruhusu hisia zake kuchukua nafasi katika utendaji wake na hatimae akachukua nafasi hata ya kukudhuru katika sehemu kubwa katika maisha yako

Ninapozungumzia kuwa usisumbukie keshi uwa sina maana kuwa usifanye kazi au  uridhike tu au uridhike katika hatua ya maisha uliyofikia ila nazungumzia usijaribu kuilazimisha kesho yako kuwa kama unavyotaka bali iache kesho ijitengeneze kisha nawe uingie kuikabili

Mathayo 6:30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba

Mungu apingani na wewe kujishughulisha katika maisha yako bali inakuwa katika mazingira magumu pindi pale mtu anaanza kuona umuhimu wa kesho yake hata kuliko Mungu, na anakuwa yuko tayari kufanya chochote ili mradi asikose kitu ambacho anakiwaza kuwa ni cha maana katika kesho yake pasipo kujua uweza Mungu unaweza ukamtosheleza na kumpa ustawi ulio bora kuliko kile ambacho anacho fikiria.

Wako watu walioacha imani zao kwa kuona kesho inaingiliwa na mwingine mathalani mtu alikuwa na mchumba wake na baadae wakaachana na kisha akamuona na mtu mwingine basi hapo uweza kuzaliwa kisirani kisicho koma na bila shaka furaha yake inakuwa ni maumivu ya mwenzake, wako watu wanachukua maamuzi na kusahau kuwa wameokoka na maisha mtu aliyeokoka anatakiwa aishi vipi badala yake anakumbuka baada ya kutimiza hazma yake inawezekana katika kumdhulu au jambo lingine.

Watu wengi wamekuwa wakihama makanisa kwa kuona hapa kesho yangu imeingiliwa na mtu mwingine mathalani alikuwa anajiona kuwa anastahili kuwa na nafasi fulani kanisani lakini akaona ile nafasi imechukuliwa na mtu mwingine na hivyo kuona hapo kuna hujuma imefanyika basi na kuona hakuna la maana sana hapa na ukaanza kuona kama vile thamani yake imekwisha potea na kuona bora aende mbali ajiondoe na aibu au kuona kama umeshuka kiroho kwa wewe kukosa nafasi hiyo.

Mathayo 6:34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake

Ni jambo la kawaida sana pindi utakapoanza kuipigania kesho kwa nguvu na kujitahidi sana bila shaka uovu utaanza kukunyemelea na kutaka kukumeza kwa ndipo hapo shetani uweza kukupa akili nyingine ya haraka katika kufanikisha lile kusudi lililo ndani ya moyo wako, atakupa akili yake kama aliyo mpa eva pale bustanini

Mwanzo 3:1Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana    Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

►Yalikuwa maneno machache lakini yaliweza kuupindua ufahamu wa eva na atimae kuangukia sehemu isiyo salama katika maisha yake!

Ukikaa katika nafasi yako ambayo Mungu amekuweka kesho sio swala la kukunyima raha bali ni swala la kufurahia na kuamini kuwa itakuwa tu kwakua Mungu atakuweka hapo!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni