HAIKUWA RAHISI
Ukitaka kuona mtu
anaongea na maneno hayaeleweki, na ukitaka kuona mtu anaongea maneno ambayo
hayaishi, ukitaka kuona mtu analia pasipo kupigwa wala kukasalishwa, ukitaka
kuona mtu anagalagala chini pasipo kuangalia chini panausafi kiasi gani,ukitaka
kuona mtu anashikwa kigugumizi cha ghafla na mwisho uweza kutamka neno hili
HAIKUWA RAHISI!
Hili neno kwa kawaida linatamkwa mwisho wa
jambo au wa safari na hasa jambo hilo linapokuwa na mwisho mwema au ushindi wa
kishindo! Na kwa kawaida kinachofuata hapo ni pumziko la moyo na hali hii
inaweza kujitokeza katika hali ya mwilini kwa namna mtu anavyo shusha pumzi na
kusema kwa kweli HAIKUWA RAHISI napingine anaweza kusema HAKIKA MUNGU
AMETUSAIDIA.
Na pengine hili neno linatamkwa baada ya mtu kupitia
changamoto katika maisha yake yawezekana magonjwa, mateso,kuchelewa kuolewa
(kadiri ya ufahamu wa mtu),misukosuko ya mahusiano,kunyimwa haki zake na
pengine hata kukosa kazi kwa muda mrefu, na ukubali kuwa changamoto
zinatofautiana na pindi mtu mmoja anapotokea akutie moyo….bila shaka unaweza kuamini
kuwa nami Mungu atanikumbuka na hatimae nitakuwa katika nafasi iliyo bora zaidi
ambayo itafanya ni mwabudu Mungu kwa raha zaidi kuliko kitu kingine chochote.
Japo kuna wakati katika
maisha unaweza kuishi na usione kama kuna haja ya kumshukuru Mungu na kuzidi
kumwamini kwakua unaweza usiuone ushindi kwa namna ya akili ya kimwili niseme
tu kuwa ipo nguvu kubwa sana kwa wewe kumuona Mungu katika kila hatua
unayofikia na sio manung’uniko kwani manung’uniko sio sehemu yako bali
unahitajika kuona nguvu na uweza wa Mungu kuhusika katika maisha yako.
Hauhitaji kuona makubwa
sana na ndio uone kuwa haikuwa rahisi na mengine ukaona kuwa ni ya kawaida tu,
kubwa ni kutambua kuwa katika yote unahitaji kuona uwezo wa Mungu katika
kukutoa mahali fulani na kukupeleka katika hatua nyingine kwa maana hiyo
usisubiri upone kwenye ajali, magonjwa makubwa na ndio uone kuwa uweza wa Mungu
la hasha jifunze kushukuru Mungu kwakua yeye anapenda kushukuriwa sana.
Yoshua 4:24 watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa
Bwana, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche Bwana, Mungu wenu, milele.
Na ni kweli Mungu
anafanya jambo ili kuhakikisha kuwa yeye aonekane na sio kitu kingine na pia anafanya yote ili
wewe ujisikie vizuri na watu wamuone Mungu katika hali nyingine na ya kiupekee
zaidi kupitia wewe.
Kwa kusema ukweli mtu
yeyote anayefanya kazi,anayesoma na shughuli zingine upenda kufikia hatua
ambayo itakayomluhusu kusema kuwa mimi kuwa hapa au kuwa hivi HAIKUWA RAHISI na
hivyo upata sababu au heshima ya kumwabudu Mungu zaidi na kumshukuru sana kwa
kuwa ana amini ni Mungu pamoja na yeye ameweza kufika hatua aliyoifikia( mwenye
akili njema).
Japo siwezi kukataa
kuwa kuna wakati unaweza kuona sasa yamekwisha ukamshukuru Mungu sana lakini
ukumbuke kwamba maadamu unaishi jua kila jambo kuna majira yake kuna majira ya
kucheka na majira ya kulia na kadharika sawa na neno la Mungu linavyosema…………
Japo furaha/huzuni ya
jana haitakuwa sawa na furaha/huzuni ya leo.
Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake,
Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
Ndivyo hivyo ilivyo
Mungu ajawai kukosea na kamwe hatakosea kama alivyosema ndivyo itakavyo kuwa
kwa kuwa yeye analokusudi lililokamili kwa ajili ya kusudi lake…..mathalani
unaweza kuona mtu baada ya kumaliza hatua fulani katika maisha yake anaweza
kufanya sherehe kubwa katika hali njema tu kuwa Mungu amemsaidia mathalani
mwanafunzi wa chuo anapohitimu anakuwa na furaha sana lakini hajajua kile
kitakachofuata wakati mwingine anaweza kukaa mtaani bila kazi na ikamfikia hata
kuwaza hivi kwa nini nilifanya sherehe katika baada ya kuhitimu hatua fulani ya
elimu.
HAIKUWA RAHISI inapaswa
kuwa ni lugha yako kwakua utakuwa ukimuona Mungu akikuvusha siku baada ya siku
kadili ufahamu utakapozidi kumuona Mungu katika kufanana na Mungu kwa namna
alivyotaka tuwe.
Waefeso 4:13 hata na sisi sote tutakapoufikia
umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata
kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson……………………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni