WAKATI SAHIHI
Ni swali la kawaida mtu uweza kukuliza kuwa jambo unalolifanya sasa unafikiri ni wakati sahihi wa wewe kulifanya jambo hili? Au unafikiri mahali upo unafikiri ni wakati sahihi wa wewe kuwa hapo? Hama Unafikiri rafiki uliye naye sasa ata kufaa kwa wakati huu? Bila shaka jibu lake litaamliwa na utashi wa nafsi yako.
Naomba niseme kuwa kunatofauti kubwa kwa mwembe kutoa maua na kutoa embe hivyo naweza kusema kuwa maua sio maembe japo tunaita kuwa mwembe kutoa maua kuwa ni dalili nzuri ya kutoa maembe! Ila kuna utofauti mkubwa sana na kamwe hauwezi kuzifananisha ndomana …………kuna dalili ya mvua na mvua yenyewe kunyesha!
Dalili kubwa ya watu kuwa hawajui wakati sahihi ni ugomvi miongoni mwao katika kugombania kitu fulani katika maisha yao lakini wanaotambua wakati uwa na busara katika maamuzi yao japo wakati mwingine unaweza kuona kama mtu huyo yuko nje na wakati au ajitambui.
Hichi ni kitendawili kwa watu wengi katika kujua hasa WAKATI SAHIHI kwangu ni upi? Wako watu waliopata kazi wakajua sasa ni wakati wangu wakijinafasi ghafla akafukuzwa kazi na kujikuta anarudi katika hali ya mwanzo, yuko mtu baada kuona huduma iliyo ndani yake inachemka na kuona ishara na maajabu zinaanza ambatana katika maisha yake basi akafikiri huo ni wakati sahihi wa yeye kufungua kanisa na mwisho akaona tofauti na vile alivyowaza akaamua kuacha na kujiingiza katika shughuli zingine, pia tusisahau kuwa kunatofauti kati ya muonekano mzuri na akufahae katika maisha yako.
►Ninapozungumzia wakati sahihi naweza kuita kuwa ni fumbo la moyo, mshangao wa akili au mgongano wa malengo katika kuleta usawa wa hatua katika hali ya umoja na katika ustawi!
Nipende kusema kuwa wakati sahihi sio kama hatua za bidamu katika kukua mathalani utoto, ujana na uzee au utu uzima bali uja kwa namna yake utegemea sana ratiba ya Mungu kuliko malengo yako kuwa unataka kuwa nani?
Bila shaka wakati sahihi uweza kuwa ni usiku wa giza wenye joto lisilotoa fumbo kuwa wakati gani litaishia…… uja kwa namna yake na uweza kuimarika kwa namna yake bila shaka italeta mshangao wa akili unaweza kusema wakati wote walikuwa wapi?
Wakati sahihi hautaji sana maandalizi ya akili au ya mwili ila utakapofika wenyewe utaandaa mwili wako kuupokea na akili kuwa sawa na wakati ulivyo kwani wakati unapofika na mazingira ujikusanya bila shaka unakuwa unakuwa umebeba hazina ya kutosha sana hivyo inakuja kukamilisha kila kitu kinachotakiwa.
Kama kuna kitu kibaya kukosea ni wakati endapo utatumia wakati tofauti na ulivyo ni wazi itakugharimu na sio wakati wenyewe, ni seme hakuna raha na furaha ya kweli tofauti na kufanya jambo katika wakati uliomuafaka kwani kila kitu kinakuwa tayari.
Nikubaliane kuwa katika kuutambua wakati sahihi ni swala gumu na zito kwasababu alihusishi sana utendaji wa juhudi binafsi bali uja kwa mikakati yake na wakati mwingi hata njia yake uwezi kuijua hivyo hautaji kusukuma wakati kwa akili na kujipa furaha ya muda isiyo na msingi wa kuendelea katika ubora.
Kunaweza kuwa ni wakati sahihi wa watu wote lakini isiwe ni wakati sahihi kwako hivyo lazima ukubaliane na hali hiyo na kujua kwamba wakati wako upo na pindi utakapofika basi bila shaka kila kitu kitakuwa wazi pasipo usaidizi mwingine.
Wakati wa kuchanua ukifika umefika tu maadamu uko katika mazingira ya kuruhusu hali hiyo itokee katika maisha yako lazima ujue kuwa sio kila wakati ni wako bali wakati wako sio watu watautamani bali utakuwa ni ushindi katika maisha yako, hautaji ujitambulishe bali wakati wenyewe utajitambulisha.
Matendo ya Mitume 13:22 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.
Lazima utambue wakati bora kwako ni wakati sahihi ambao hautaji kuwaza sana bali wenyewe utakuja na kukupata pale ulipo kwani kwa yeye hakuna kizingiti ambacho kitashindwa kutii mamlaka yake.
Lazima utambue kuwa wakati sahihi utakapofika utakujia pale ulipo hauna haja kuwaza na kuufikiria wakati wote na hata kushindwa kuyafanya yale uliyotakiwa kuyafanya katika ubora wake.
Marko 8:36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Ni vizuri utambue wakati sahihi umewekwa na Mungu hivyo ni vizuri uwe katika wakati huu ukiwa ndani ya KRISTO kwa maana ndani yake hakuna majuto na utautumia wakati wako vizuri utawafaidia wengine na wewe utapata neema zaidi na zaidi sana ufalme wa Mungu.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………..0764 018535
THE RIGHT TIME IS THE BEST TIME
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni