Jumanne, 26 Julai 2016

ANAITWA MUNGU!



ANAITWA MUNGU!


Unaweza kumwita mwenye nguvu, wa huruma, wa upendo, wa amani, mponyaji, mfariji hizo zote ni sifa zake lakini kamwe haitabadilisha kuwa yeye KUITWA MUNGU! Karibu sana,

Uhitaji kuchoka sana katika maisha utakapoenda katika njia ambayo Mungu amekuagiza kuenenda wewe tambua kuwa yeye anaitwa MUNGU hakuna jambo au hali yoyote ambayo itaweza kuzuia KISHINDO chake kwakua badala yake hakuna na nafasi yake inabaki kuwa yake.

Uwa yeye hazuiliwi ila anaweza zuia! Achoki ila anaweza kukuchosha! Asahau ila anaweza kukusahaulisha! Achelewi ila anaweza kukuchelewesha! Apatoi ila anaweza kukuchelewesha ANAITWA MUNGU!

Haitaji umsaidie ili ufike mapema yeye mwenyewe anajua namna ya kukufikisha! Ahuhitaji kujipenyeza ili uonekane, ila yeye atajidhihirisha nawe utaonekana tu! Tembea katika hatua zake tu utafika tu maana hakuna aliyetembea katika hatua zake akaishia njiani/akashindwa kufika.

Hana uhitaji ndani yake ila mimi na wewe tunaweza kuwa na uhitaji lakini anajua namna ya kukutosheleza pasipo kukwama kwakua unajua njia ya yeye kukupa uhitaji wako…mathalani yesu alipo gundua ana deni ndipo akaamuru mwanafunzi wake kwenda kuvua samaki kisha achukue samaki na kumtoa fedha alafu akalipe madeni wanayodaiwa.

Nipende kusema hali ya wewe kuwa na uhitaji hilo ni jambo la kawaida kwakua katika biblia watu walikuwa nauhitaji mwingi mathalani sara(uhitaji wa mtoto), batromayo( uhitaji wa kuona kwani alikuwa kipofu), mwanamke mjane wa serepta(uhitaji wa chakula) hivyo sio ajabu ya wewe kuwa na uhitaji wowote kwani unachohitaji hapo ni namna  Mungu afanyike njia ya wewe katika kukutoa hapo.

Nipende kusema mahali ambapo akili yako itakosa mwelekeo kwakua umeshatumia njia nyingi lakini bila mafanikio, huna haja ya kutafuta mbaya wako mtazame petro alipo jaribu kuvua samaki usiku kucha bila mafanikio alibaki palepale mpaka yesu alipokuja pale na kutamka NENO hivyo uhitaji kutembea tembea huku ukiangalia labda huyu atanihurumia lakini tambua kwa kila uhitaji una njia zake za kupata au kukizi uhitaji kwa maana rahisi hakuna mtihani ukakosa majibu, japo wakati mwingine unaweza usipate majibu lakini mtunzi wa mtihani anayo majibu.

Muono wa watu kuona  kuwa umeshindwa sio kweli kuwa umeshindwa, kwani kushindwa kwa mwili sio kushindwa kwa roho na nguvu ya mkristo iko ndani ambayo ndio inazalisha kunawiri katika muonekano wanje na kama ujaanza kuchanua katika muonekano wanje jua ni mbegu iliyokaribia kuchepua ni wewe kutulia kuhakikisha mpaka inachipua.

Katika yeye kilindini kinaweza onekana nchi kavu, katika yeye ndani ya giza totoro unaweza ukaokota dhahabu inayoonekana peupe, na katika yeye unaweza kuvuka bahari kama unavuka barabara kwa miguu pasipo kuhofia chochote, katika yeye unaweza kukaa na mnyama mkali mathalani simba au chatu na bado ukaona usalama wako badala ya kuona ni hatari kwako wakawa ulinzi kwako.

Unaweza kukubali au kukataa! Unaweza kupenda au kutopenda! Unaweza kuchukia au kufurahi! Unaweza ng’ong’ona au kutoa sauti! Unaweza kuwaza au kutowaza! Hali yako au hali yoyote haiwezi badilisha hali hii kuwa yeye ANAITWA MUNGU. Na kwa lile analolikusudia kamwe uwezi kulizuia lisifanyike hata dunia yote ikiwa kinyume nae lakini yeye mwenyewe hawezi KUSHINDWA kutimiza hazima yake.

Hana ushemeji na mtu au ushikaji na mtu kwa kutegemea kwa wewe kufanya baadhi ya mambo unafikiri yapendazayo basi utapata kibali kwake Mungu! Kama hajafurahi basi hajafurahi tu unahitaji uelewe na kusimama katika njia upasayo kuenenda ili yeye afanye kama alivyokusudia na sio kufikiri utamshawishi Mungu kwakufanya baadhi ya mambo ayafurahiyo.

Hauhitaji kufika mbali sana na kupata picha zisizo kukusaidia katika maisha yako kama kuona hapa kuna ubaguzi, wenyewe, kujuana kwingi wewe tambua kuwa ANAITWA MUNGU mahali alipo ndipo kuna kunawiri na sio walipo watu wengi anapotengeneza njia hakuna awezae kuijua na hata kuizuia.

Usitafute mambo mengine yenye tija kwako na yasiyo na faida kwa Mungu mathalani kujulikana, kusifiwa kubali kutembea katika hatua za Mungu pasipo haraka kuliko kuwa na haraka pasipo kuona hatima njema katika maisha yako! KAMA YAKO NI YAKO TU MAANA ANAITWA MUNGU mtawala wa dunia na vyote vilivyopo ndani yake. Barikiwa rafiki!

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………0764 018535

Jumanne, 12 Julai 2016

USIOGOPE!

USIOGOPE


Habari msomaji!

Karibu katika neno la leo………..Nakubaliana kabisa kuwa neno hili USIOGOPE sio geni machoni pako na uwa sio kila wakati linakuwa la maana sana kwako kama hakuna jambo LINALOKUOGOPESHA! Na zaidi sana neno hili usiogope nguvu yake utegemea sana nani amekwambia, natambua kwa uhalisi moyo unalipokea neno pindi mtu anaposema USIOGOPE bila shaka moyo wako utatoa tafsiri ya mtu huyo( kama anamaanisha kile anachokizungumza) kwako na ndipo utakapoitikia sawa na tafsiri iliyotolewa na moyo japo wote wanaweza wasijue lakini wewe katika uhalisi wa moyo wako utatambua, Mungu atusaidie.

Ukiachana na hali hiyo, najua neno hili USIOGOPE linanguvu na la maana sana kwa mwihitaji wa neno hili kama maji kwa mwenye kiu, sikatai wako watu wamepitia shida nyingi hivyo wamesikia sana hili neno USIOGOPE maana kila mtu anayeenda kumpa pole anamwambia USIOGOPE MUNGU YU NAWE! Lakini katika yote bado neno USIOGPE lina hitajika sana leo kesho naam siku zote maadam tunaishi basi tunalihitaji hili neno………na pindi utakaposikia moyo wako unaweza kuinuka na kuona nami nina watu wanaonipenda! Asante Mungu kwa hili.

Neno USIOGOPE limetafsiriwa na kupewa  maana nyingi zilizotolewa na watu mbalimbali mashuhuri na wasio mashuhuri na zenye maana nzuri na zenye kuvutia napengine zinasadifu na ukweli wa hilo neno…….. maana yangu katika neno hili USIOGOPE ni hali ya moyo kuhofia kupoteza furaha yake.

Nakubaliana kwa asilimia zote MTU akikwambia USIOGOPE na MUNGU akisema USIOGOPE haya ni maneno sawa ila kutokana na chimbuko tofauti lilikotoka basi yamebeba maana tofauti na upokeaji wake uko tofauti na mwendo wake hapo utakuwa ni tofauti, kwani binadamu hata awe na mali kiasi gani na hata akikuhurumia kiasi gani bado ubinafsi utatawala tu ila Mungu anapenda vile anavyoishi basi nawe uishi hivyo ikiwezekana YEYE AISHI KUPITIA WEWE.

Unaweza kujiuuliza Mungu atasema lini kuwa mimi NISIOGOPE kwa maana katika maisha naona watu na vitu vinavyoizunguka DUNIA nitajuaje Mungu sasa ananiambia NISIOGOPE swali hili linaweza kuulizwa na mtu anayeenda kanisani au msikitini na hata Yule ambaye sehemu zote haendi lakini sio mtu ambaye anaye MJUA MUNGU katika Roho Mtakatifu.

Kama msomaji mzuri wa biblia unaweza kugundua neno UOGOPE alina mashiko katika kitabu hiki zaidi ya neno USIOGOPE  lenye maana kubwa ukilitazama kwa jicho la rohoni lililobeba tafsiri ya Mungu uwa hakuna shaka utatambua KUTOOGOPA ndio maisha ya MUNGU kwakua kupitia yeye vyote vilifanyika na pasipo yeye akikufanyika chochote kilichofanyika!

Kiufupi tu maisha ya KUTOOGOPA ndio maisha tunayopaswa kuishi kwani kiasi kikubwa upelekea kufanya kitu kwa ubora zaidi kuliko mtu anayefanya jambo akiwa ana hofu uhakika unakuwa mdogo wa kufanya kitu kwa ufasaha zaidi, siwezi kukudanganya kuwa utakuwa na hali ya kutoogopa kwa namna ya kawaida maadamu umezaliwa tu! Sio kweli bali NENO LA MUNGU litakupa ujasiri usiokuwa wa baadhi matukio au watu fulani kwani ndio ujasiri mwingi uliopo dunia wa namna fulani lakini sio wa wakati wote kwakua msingi wake haujajengwa katika ujasiri wa kila kitu bali wa baadhi ya vitu tu.

Niseme tu hata kama utakuwa mtaratibu vipi na mwema sana ukisha iruhusu HOFU ichukue nafasi hapo kutenda kinyume na ulivyopanga ni rahisi kwani unaweza kukusudia jambo jema lakini kutokana na HOFU ukajikuta ufanyi au ukafanya tofauti,

Maisha yanayoambata na hofu yanapelekea kuwa mtumwa kwani unakuwa kifungoni ambacho umejiweka wewe mwenyewe kutokana na hali ya ndani inayokusukuma,……….maisha haya ya uwoga uweza kusababishwa na mtu unayetembea naye na kumpa nafasi katika maisha yako hivyo maisha yake yatakuathiri kwa kiasi kikubwa.

Ukitaka kuishi maisha ambayo sio yako basi ishi maisha yanayobebwa na UWOGA utaishi kila mtindo wa maisha haijarishi unataka au hautaki, bali ukitaka kuishi maisha ambayo Mungu amekukusudia ishi maisha yanayo ongozwa na NENO LA MUNGU! Upate ujasiri na akili njema sio kwa kukulupuka.

Maisha ya ujasiri ni maisha ya kumwamini Mungu na kumpenda  kunakopelekea KUJIAMINI na sio maisha ya utemi na ubabe katika kujisahau kuwa wote ni kazi ya Mungu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………0764 018535

TUMIA MUDA WAKO KUJIONA WEWE NA SIO MWINGINE!

Jumanne, 5 Julai 2016

LOVE YOUR DESTINY



IPENDE HATIMA YAKO!


 Katika jambo ambalo wanadamu wengi wamefanikiwa kulitendea haki ni KUJIPENDA, na katika jambo watu wengi hawajafanikiwa sana ni KUJICHUKIA hivyo tunaona kila mtu/ binadamu anavyo jipenda mwenyewe na kujithamihi zaidi sana KUJIONA BORA! Hongera kwa hilo…

Naweza kusema kunatofauti kubwa kati ya KUJIPENDA NA KUIPENDA HATIMA YAKO! Unaweza kujipenda sana na huku ukaichukia sana hatima japo kwa wakati mwingi wawezafanya hivi pasipo kujua kwakufanya hivyo naiangamiza hatima yangu lakini habari njema ni kwamba pindi utakapoamua KUIPENDA HATIMA YAKO BASI UTAKUWA UMEIPENDA NAFSI MOJA KWA MOJA!

Ni wazi katika ulimwengu wa sasa hali inaongezeka kwa watu wengi hasa binadamu wa sasa wamekuwa na muamko mkubwa sana kuhakikisha wanatendea kazi ile hazina iliyo ndani mwa mtu ndomana utaona kila mtu anafanya hiki na mwingine anafanya kile.

Unaweza kuwa mtu wa ajabu sana pindi utakapo tambua hatima yako na usionyeshe hali ya kufurahia kwakua hatima uwa inabeba ustawi wa mtu husika na bila shaka upelekea kuwa hali ya kufurahia na kujisikia vyema pindi unapolitumikia au unapotumika katika hatima yako,

Nakubaliana kabisa kuwa wako watu pindi watakapo tambua hatima zao mioyo yao uweza kutokufurahia na wapo wenye kutambua nafasi zao katika hatima zao nao wakafurahi sana na mioyo yao ikajawa na shauku na kiu ya kulitendea kazi lile lililo hatima yake.

Niseme kuna vitu vitatu visivyohusiana kabisana ila vinategemeana sana KULIJUA KUSUDI, KILITUMIKIA KUSUDI NA KULIPENDA KUSUDI………….ni kiwa na maana kuwa kam hakuna kulijua kusudi basi hakuna kulitumikia kusudi na kama usipolipenda kamwe uwezi kulitumikia kusudi kiufasaha,

Kama kosa kubwa unaweza kulifanya unapokuwa dunia ni hali ya kukosa kuijua hatima yako kwani unakuwa sawa na mtu asiyejua mahali pake pa kuishi kwahiyo popote anaweza kutua matuo na kuishi maadam watu wanaishi pasipo kujua kama mahali hapo panaweza kutoa nuru dhidi ya hatima yangu, bila shaka hali hii unaweza ukawa unachoka sana kimwili na kiakili pasipo kuwa na uhakika kuwa namna nguvu zako zinaweza kujenga hatima yako kuwa bora zaidi,

Sina mashaka kuwa hatima yako ndio inakutambulisha kuwa wewe ni nani na unawezo gani na inaleta maana ya wewe kuwepo duniani na ndio lina kuwa neno jema kwa Mungu pindi utakapoamua kusema ASANTE kwa kuniumba kwa wewe kutembea katika hatima ambayo kwa hiyo amekupa neema ya kuishi.

Nipende kusema KUIPENDA HATIMA YAKO sio kucheka pindi unapofanya au kulitumikia KUSUDI hilo bali ni hali ya kujidhatiti na mikakati dhabiti iliyowekwa ndani yako kupititia Roho mtakatifu na akili yako kukubaliana nayo na hatimae kuichukulia hatua katika utekelezaji kwa wakati wake sahihi.

Kwa ushauri wa bure tu ogopa mtu analipenda na kuihitumikia hatima yake kwa moyo wake kwani kucheza naye au kumfanyia chochote ambacho akistahili ni sawasawa na kuikejeli mbingu na uku ukiendelea kuishi chini yake, ……….hama ni sawa sawa na kumdharau bosi uku yeye akijua nab ado ukisubiri akupatie mshahara wa wewe kujikimu katika maisha yako.

NAIPENDAJE HATIMA YANGU! 

Hii sio kiroho kabisa na wala haitaji uwe mwana saikolojia ni kanuni ya kawaida sana kwamba lolote ili ufanikiwe unahitaji hali ya KUPENDA hapo ndipo BIDII na UFANISI na hali kutochoka uzaliwa hapo kwakua unajua hapo ndipo upande wako na ndio sehemu pekee unaweza ukaishi vizuri sawa na samaki kuishi baharini basi ni mateso kwake kwa yeye kuishi nchi kavu.

Uwezi kusema kuwa naipenda hatima yangu kama una mtu kama kielelezo chako mbali na Mungu aliweka hiyo huduma/hatima ndani ya maisha yako, ni vizuri kutmbua kuwa kila mtu ana hatima yake hata kama unaona mna landana katika huduma zenu bali utambue kila mtu kuna mahali alikutana na Mungu hivyo kila mtu ana mwisho wake na kamwe uwezi jua, unaweza kusema hata huyu kaishia hapo tena ni mkongwe je! Itakuaje kwangu kushindwa kuwa hapo ndipo mwisho wake na wewe unahitaji kuendelea, ni hatari sana kama utaruhusu ufahamu wako kuona ndio mwisho.

Ni vizuri kujifunza kwa wengine ila sio kutembea katika nyazo zao kwani ujui katika mazingira yao walikumbana na nini na hazina gani walikuwa nayo ndani yao katika kuhakikisha wanashinda katika changamoto zao zilizo wakabili.

Uwezi kusema naipenda hatima yangu kama utoi nafasi ya kutosha kwa Roho mtakatifu kuitumia hiyo hazina yake kwa ajili yake, wako watu baada ya kutambua wana kusudi ambalo limeshaanza kutambulika na kuheshima mbaya zaidi kama amesoma soma kidogo upenda kuonyesha usomi wake katika kutembea katika hatima yako pasipo kujua kuwa Roho mtakatifu ni zaidi ya profesa na hakuna mfano wake unachotakiwa ni kumwelewa na kumluhusu atende kupitia wewe.

Ni kweli unaweza kujua vizuri lakini Mungu ndio anajua zaidi yako na anajua uhitaji wa kila mtu, hivyo Roho mtakatifu anapochukua nafasi mpe nafasi akutane na watu ili watu waone majibu yao!

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………………………0764 018535

HATIMA INATUNZWA NA MWENYE HATIMA, UKIITUNZA UTAKUWA SALAMA