IPENDE HATIMA YAKO!
Katika jambo ambalo wanadamu wengi wamefanikiwa kulitendea
haki ni KUJIPENDA, na katika jambo watu wengi hawajafanikiwa sana ni KUJICHUKIA
hivyo tunaona kila mtu/ binadamu anavyo jipenda mwenyewe na kujithamihi zaidi
sana KUJIONA BORA! Hongera kwa hilo…
Naweza kusema kunatofauti kubwa kati ya KUJIPENDA NA KUIPENDA
HATIMA YAKO! Unaweza kujipenda sana na huku ukaichukia sana hatima japo kwa
wakati mwingi wawezafanya hivi pasipo kujua kwakufanya hivyo naiangamiza hatima
yangu lakini habari njema ni kwamba pindi utakapoamua KUIPENDA HATIMA YAKO BASI
UTAKUWA UMEIPENDA NAFSI MOJA KWA MOJA!
Ni wazi katika ulimwengu wa sasa hali inaongezeka kwa watu
wengi hasa binadamu wa sasa wamekuwa na muamko mkubwa sana kuhakikisha
wanatendea kazi ile hazina iliyo ndani mwa mtu ndomana utaona kila mtu anafanya
hiki na mwingine anafanya kile.
Unaweza kuwa mtu wa ajabu sana pindi utakapo tambua hatima
yako na usionyeshe hali ya kufurahia kwakua hatima uwa inabeba ustawi wa mtu
husika na bila shaka upelekea kuwa hali ya kufurahia na kujisikia vyema pindi
unapolitumikia au unapotumika katika hatima yako,
Nakubaliana kabisa kuwa wako watu pindi watakapo tambua
hatima zao mioyo yao uweza kutokufurahia na wapo wenye kutambua nafasi zao
katika hatima zao nao wakafurahi sana na mioyo yao ikajawa na shauku na kiu ya
kulitendea kazi lile lililo hatima yake.
Niseme kuna vitu vitatu visivyohusiana kabisana ila
vinategemeana sana KULIJUA KUSUDI, KILITUMIKIA KUSUDI NA KULIPENDA
KUSUDI………….ni kiwa na maana kuwa kam hakuna kulijua kusudi basi hakuna
kulitumikia kusudi na kama usipolipenda kamwe uwezi kulitumikia kusudi
kiufasaha,
Kama kosa kubwa unaweza kulifanya unapokuwa dunia ni hali ya
kukosa kuijua hatima yako kwani unakuwa sawa na mtu asiyejua mahali pake pa kuishi
kwahiyo popote anaweza kutua matuo na kuishi maadam watu wanaishi pasipo kujua
kama mahali hapo panaweza kutoa nuru dhidi ya hatima yangu, bila shaka hali hii
unaweza ukawa unachoka sana kimwili na kiakili pasipo kuwa na uhakika kuwa
namna nguvu zako zinaweza kujenga hatima yako kuwa bora zaidi,
Sina mashaka kuwa hatima yako ndio inakutambulisha kuwa wewe
ni nani na unawezo gani na inaleta maana ya wewe kuwepo duniani na ndio lina
kuwa neno jema kwa Mungu pindi utakapoamua kusema ASANTE kwa kuniumba kwa wewe
kutembea katika hatima ambayo kwa hiyo amekupa neema ya kuishi.
Nipende kusema KUIPENDA HATIMA YAKO sio kucheka pindi
unapofanya au kulitumikia KUSUDI hilo bali ni hali ya kujidhatiti na mikakati
dhabiti iliyowekwa ndani yako kupititia Roho mtakatifu na akili yako
kukubaliana nayo na hatimae kuichukulia hatua katika utekelezaji kwa wakati
wake sahihi.
Kwa ushauri wa bure tu ogopa mtu analipenda na kuihitumikia
hatima yake kwa moyo wake kwani kucheza naye au kumfanyia chochote ambacho
akistahili ni sawasawa na kuikejeli mbingu na uku ukiendelea kuishi chini yake,
……….hama ni sawa sawa na kumdharau bosi uku yeye akijua nab ado ukisubiri akupatie
mshahara wa wewe kujikimu katika maisha yako.
NAIPENDAJE HATIMA YANGU!
Hii sio kiroho kabisa na wala haitaji uwe mwana saikolojia ni
kanuni ya kawaida sana kwamba lolote ili ufanikiwe unahitaji hali ya KUPENDA
hapo ndipo BIDII na UFANISI na hali kutochoka uzaliwa hapo kwakua unajua hapo
ndipo upande wako na ndio sehemu pekee unaweza ukaishi vizuri sawa na samaki
kuishi baharini basi ni mateso kwake kwa yeye kuishi nchi kavu.
Uwezi kusema kuwa naipenda hatima yangu kama una mtu kama
kielelezo chako mbali na Mungu aliweka hiyo huduma/hatima ndani ya maisha yako,
ni vizuri kutmbua kuwa kila mtu ana hatima yake hata kama unaona mna landana
katika huduma zenu bali utambue kila mtu kuna mahali alikutana na Mungu hivyo
kila mtu ana mwisho wake na kamwe uwezi jua, unaweza kusema hata huyu kaishia
hapo tena ni mkongwe je! Itakuaje kwangu kushindwa kuwa hapo ndipo mwisho wake
na wewe unahitaji kuendelea, ni hatari sana kama utaruhusu ufahamu wako kuona
ndio mwisho.
Ni vizuri kujifunza kwa wengine ila sio kutembea katika nyazo
zao kwani ujui katika mazingira yao walikumbana na nini na hazina gani walikuwa
nayo ndani yao katika kuhakikisha wanashinda katika changamoto zao zilizo
wakabili.
Uwezi kusema naipenda hatima yangu kama utoi nafasi ya
kutosha kwa Roho mtakatifu kuitumia hiyo hazina yake kwa ajili yake, wako watu
baada ya kutambua wana kusudi ambalo limeshaanza kutambulika na kuheshima mbaya
zaidi kama amesoma soma kidogo upenda kuonyesha usomi wake katika kutembea
katika hatima yako pasipo kujua kuwa Roho mtakatifu ni zaidi ya profesa na
hakuna mfano wake unachotakiwa ni kumwelewa na kumluhusu atende kupitia wewe.
Ni kweli unaweza kujua vizuri lakini Mungu ndio anajua zaidi
yako na anajua uhitaji wa kila mtu, hivyo Roho mtakatifu anapochukua nafasi mpe
nafasi akutane na watu ili watu waone majibu yao!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………………………………0764 018535
HATIMA INATUNZWA NA MWENYE HATIMA, UKIITUNZA UTAKUWA SALAMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni