Jumanne, 28 Juni 2016

ASANTE KWA HILI...............!!!



ASANTE KWA HILI

Naweza sema ni neno tamu na lenye mvuto wa kipekee na hasa kwa mtu uliyetegemea aseme ASANTE! Naye akakubaliana na sauti ya moyo wako na hatimae akasema ASANTE! Na amini utaona kama unaota na hatimae moyo wako utakuwa na furaha itakayokosa kificho katika muonekano wanje!

Na kubaliana kuwa neno ASANTE linafuata baada ya tendo jema mtu alilotendewa, japo kuna wakati unaweza kutendewa jambo jema lenye maana baadae ila pasipo kujua ni jambo jema kwako unakosa kuwa na moyo wa shukrani kwa wakati huo……….mathalani mwanafunzi anapoaandaliwa kuwa mtu fulani katika jamii yake hasa kutokana na kipawa chake bila shaka katika matengenezo ya kuwa mtu bora sio rahisi kusema ASANTE.

Changamoto kubwa katika kushukuru kwa jambo unalotendewa ni wazi inakuwa vile watu wote hamjui mnalopaswa kufanya kwa kuwa inakuwa ni mission ya Mungu katika kumwandaa mtu kuwa MTU hivyo mnakuta huyu ampendi huyu na huyu anamchukia huyu kumbe hiyo hali inasababishwa na jambo linaendelea ndani ya Mungu ila hapo kunakuwa na udhihirishi tu.

Niseme kuna siri kubwa sana katika kusema asante (shukrani) kuna minyororo inavunjika, kuna kuta zinabomoka na thamani yake kamwe huwezi kulinganisha na chochote kwani liko vile kama lilivyo hakika hili neno limebeba utoshelevu na mbaraka wake usio kuwa wa kawaida ni wewe kuutambua tu.

Nimeona mtu akikatisha kumsaidia mtu kisa kilikuwa huyu mtu ajui neno ASANTE kinywani mwake hivyo haoni kile ninachokifanya kama ni cha maana katika maisha yake hivyo sijisikii kuendelea kumsaidia maana yeye haoni jinsi ninavyojinyima juu yake hivyo ni bora niangalie kitu kingine ambako Moyo wangu unasukumwa kuwa huko.

Katika yote ni bora uone hivyo katika upande wa wanadamu wenzako kuwa awanashukrani lakini wanadamu sasa hivi imekwenda mbali sana kiasi cha kuona hata Mungu pia amewekwa katika kuchunguzwa kana kwamba ni binadamu kwani nini anitendei mimi au haoni juhudi zangu kwa ajili yake! Watu wamekuwa na kisasi sio kwa wanadamu bali wamevuka mpaka hata kwa upande wa Mungu kana kwamba na yeye walishirikiana hama kushauriana ili kwamba yeye atokee dunia na kujichagulia maisha hayatakayo na sio aliopangiwa kuishi.

ASANTE KWA HILI……….usipo ona kuwa Mungu mwema kwa yale yana yofanyika yaliyo nje ya uwezo wako basi hakuna jambo ukampa thamani yako Mungu katika hali stahiki na katika mwendelezo unaotakiwa!

Imekuwa kama mtu ukamfanyia mema mengi pindi anapoona pungufu lake moja basi uweza kusahau yote basi linakuwa na nguvu zaidi ya mema yake yote , hivi ndivyo watu wanavyoona kwa Mungu laiti ukikaa chini na kutafakari na kuona jinsi Mungu alivyo mwema katika maisha yako kamwe usinge fungua mlango mwingine wa kuona upendeleo wa Mungu kwa wengine kuliko kwako.
Samahi kwa mfano huu japo sio wote, usiwe na hasira kama mama mjamzito katika miezi ya awali kwani unaweza ukamfurahisha katika mambo mengi ukimuuzi kitu kimoja tu basi anaweza akasusa na kuona kila kitu kibaya kwake.

Lazima ujifunze kuona pamoja na yote lakini katika hili Mungu ni mwema sana  ASANTE KWA HILI kwa kuwa hakuna kipimo cha kupima wema Mungu katika maisha yako na laiti pangekuwa na mizani kati ya Mungu kwa yale apasayo kukutendea na kwako kwa yale upasayo kutenda kwake kamwe pasingekuwa na hata kushamiliana hata chembe na amini utajiona kuwa wewe ni mkosaji sana japo Mungu haoni yale unayo yawaza  na kujihukimu basi upaswi kuona kuwa Mungu sio mwema kwako.

Ni vizuri utambue unapo mzungumzia MUNGU sio kitu fulani ambacho unaweza ukakiweka unavyotaka nacho kikawa kwa namna unavyofikiria, ni vizuri utambue kwa sababu yake ndomana wewe uko japo upaswi kumuogopa zaidi sana PENZI lake likuongoze naamini utakuwa salama.
Jifunze kumshukuru Mungu hata kwa madogo maana ndio mapenzi ya Mungu kwetu, maana Mungu yeye ndie awezae kuamuru jambo jema kukufuata popote ulipo pasipo kuangalia umbali gani uliopo kati yako na mbaraka wako.

Usiruhusu kufikia maamuzi ya kuona Mungu ameniacha sasa naweza fanya chochote tambua sio kila mawazo yanayokuja kwako yamebeba usahihi hivyo usiruhusu kuwa hayo ndio maisha yako ya kuona Mungu ahusiki katika maisha yako.

Ni kweli mawazo mazuri ni kitu kimoja lakini bila neema yake uwezi kukamilisha tambua upana wa Mungu na Upendo katika kila hali inayokuzunguka na hapo ndipo uone NJIA YA KUTOKA!! NA SIO  LAWAMA,

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535

FURAHA YA MUNGU IWE NCUVU YAKO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni