Jumanne, 21 Juni 2016

INAITWA KESHO



INAITWA KESHO



Ki ukweli sina jina jingine zaidi ya kusema kuwa inaitwa KESHO! 

Na swali kwako ni kweli unaipenda kesho? Na unaweza kutofautisha mtu anayeichukia kesho yake na anayeipenda kesho yake? Karibu………………..!

Ni siku baada ya leo au kwa jina jingine uweza kuitwa ni masaa 24 yajayo, unaweza usiipende sana au ukaipenda lakini bado itabaki kuitwa KESHO na bila shaka kama Mungu akikujalia NEEMA ZAKE basi utaiona! Wapo waliona kesho kama ni siku tu ya kawaida hatimae ilipofika walijuta hivi kwa nini KESHO imekuwa LEO na bila kusahau wapo walioiogopa sana KESHO naam pindi ilipofika walipata raha sana na hata kujiuliza hivi kwa nini nilikuwa naiogopa sana kesho. 

Imekuwa kauli ya kawaida sana ikisema bora mtu akucheke LEO kuliko akucheke KESHO! Kwa maana rahisi wacha acheke LEO ili KESHO akuheshimu itakuwa picha nzuri na bila shaka italeta picha nzuri na kutambua yupi wako na yupi umesingiwa tu ila ki ukweli akuwa wako.

Bila shaka KESHO inaweza kuwa majibu ya wengi na utatuzi wa wengi katika maswali yao na wengine kuwa chanzo cha furaha na upendo miongoni mwao! Imekuwa jambo la kawaida sana kutaka kujua kitu kilichobora watu watasema kisifae kwa LEO tu bali hakikisha kitatumika hata KESHO.

Ni jambo la kawaida sana mtu kusema kuwa maana lazima awe tayari kwa LEO na hata KESHO yaani akufae leo na hata kesho maana kama umepewa kuiona pamoja naye basi utaitaji utumie vizuri pamoja nae kama Mungu akiwakupa neema kuiona.

Sikatai binadamu yeyote mwenye akili timamu bila shaka atakuwa anajitahidi sana kuiweka kesho kuwa na picha nzuri na pindi itakapofika basi ajisikie fahari zaidi ya LEO na kuona alikuwa anastahili kuwa hapo na mahala hapo palistahili yeye kuwepo na kamwe apamchoshi zaidi ya kupafurahia tu.

Japo sipingani sana kusema usiifurahie Leo ila napenda kusema pindi utakapoamua kuifurahia leo bila shaka weka mazingira mazuri ya furaha yako kuwa kuu KESHO kwa maana LEO yako hasa ujengwa na KESHO sio leo kwakua Leo itapita ila KESHO utafika……….kwa hiyo kuipenda sana njia kuliko mahali unapo pumzika ni hatari  kwa furaha endelevu.

Ki ukweli baadhi ya mambo ungelikuwa una angalia KESHO yake usingetia bidii kuyafanya sasa ila kwakua ujui kesho yake kwa ufasaha zaidi hivyo unaweza kujikuta unajikita zaidi sana kuibomoa kesho yako kwa kuipenda LEO yako.

Sina tatizo kwa wewe kuipenda leo ila ninatatizo la wewe kuipenda leo kuliko kesho yako! Japo na amini sababu moja wapo ya kuipenda leo kuliko kesho ni vile leo unaiona na kesho hauioni hivyo unaweka bidii kwa kile unachokiona pasipo hatari zaidi ya kile usichokiona na pindi kitakapo kufikia kitakukuta katika hali gani? Sina jibu.

Ni vizuri unapoiangalia LEO basi iangalie sana kwa umakini sana KESHO kwani katika hilo kunaweka usalama mkubwa wa kesho yako…..na utakubaliana nami kwa hili wale wengi walioijari kesho yao zaidi leo kwa jina lingine wanaitwa wawekezaji walijisikia vizuri pindi kesho ilipofika maana walifanya kwa ajili ya siku inayofuata na sio kuitengeneza JANA yao ili leo yao iwe na muonekano mzuri.

Ni vizuri kutambua tu kuwa haijarishi uko wapi au unafanya nini au unaweza nini au unatamani nini katika yote bado kesho itafika na itakuwa sawa na kanuni yake! Kwani hauwezi kupanda mkorosho ukategemea kuvuna karanga hapo hapaitaji imani wala busara yoyote bali kanuni inavyosema ndivyo itakavyotokea.

Niseme wazi ni bora uchoke leo maana inaweza ikatengenezeka kuliko kuchoka kesho pasipo kujua utakuwa katika hali gani? Na msaada gani utaupata na je! Uo msaada utakuwa wa maana kwako itategemea sana na namna itakavyo kukusaidia au kukubomoa kabisa.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………….0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni