NAJUAJE KAMA NAMJUA MUNGU?
Katika maswali ambayo
watu wengi hawatafikiria sana ilikutoa jibu, ni swali hili JE! UNAMJUA MUNGU?
Watu wengi watasema yah! Kwakua naenda kanisani, nasaidia watu, naishi vizuri
na majirani zangu, nina biblia nyumbani, na wengine watasema uwa wakati
mwingine nikipata nafasi kutokana na majukumu yangu naenda kanisani kwakua
natambua yeye ni muweza wa yote, na wengine wataenda mbali kidogo wanasema mimi
mchungaji wangu ananijua na ameniambia nitakuwa mtumishi mkubwa kwakua ndani
yangu ameona huduma kubwa na hata mtaani kwangu watu wananihita mchungaji! Na
wengine watasema mimi hata mapepo yananitambua na yana niogopa na mara mtu
mwenye mapepo anaponiona uwa anapiga kelele yaani ni kama yesu anapokutana na
mtu mwenye pepo! Uku ndiko kumjua Mungu swali jepesi?
Ukweli watu wengi
tumekuwa tukijifunika sana katika kutembea katika vipawa tukiamini katika hali hiyo
basi sisi tunamjua Mungu sana hata kuliko watu wengine ambao hawatembei katika
vipawa vyao! Hivyo nasi ikatupelekea kujihesabia haki au kujipa nafasi ambayo
tuna amni kuwa tunastahili kuwa nayo kwa hiyo tunaweza kuwanyoshea vidole
wengine kuwa Yule bado sana! Mpaka anifikie mimi sijui mpaka lini labda mwaka
3000 Mungu akitujalia.
Niseme wazi ili jambo
linajibiwa vizuri hata mtu asiye okoka pindi utakapo muuliza kuwa wewe unamjua
Mungu atasema pasipo shaka anamjua ten asana mbali zaidi uwakute wasomi wenye
uelewa mdogo kuhusu Mungu wanaweza kushusha data mapaka ukasema hakuna asiye
mjua Mungu katika ulimwengu wa sasa, hata kama anajua wakati mwingine anakosea
uweza kusema japo najua ninachofanya ni makosa lakini najua usahihi ni upi kwa
maana namjua Mungu japo na mkosea sana lakini na amini siku moja atanisaidia tu
ni taka vizuri sawa ninavyojua.
KUMJUA MUNGU! Kumekuwa
ni jambo la kawaida sana kwa kuwa kila mtu anasema anamjua Mungu kwakua
asilimia kubwa ya wanadamu wana amini Mungu yupo japo wako watu ambao wanaamini
hakuna Mungu katika dunia ya sasa bali ujikita zaidi kwenye sayansi na
teknolojia pamoja na uvumbuzi wa mambo mbalimbali yenye kuwapa kiburi na
majivuno kuwa wao wanaijua dunia kuliko hata mwenye dunia.
Mbaya zaidi hata watu
waliokoka wanaaminika kuwa wanamjua Mungu na kuwa kielelezo safi katika
kuwaonyesha jamii kuwa mtu anayemjua Mungu anatakiwa aweje! Lakini wamekuwa wakipeperushwa
uku na kule na kutoa ushuhuda mbovu kwa watu wasio okoka wanaoenda kanisani
wengi wamekuwa wakiwa waongo sana katika mambo mengi mathalani kuomba kazi,
mausiano, kujirahisisha na wakati mwingine kushiriki katika vitendo vya
kuwadhulumu watu, rushwa na mengine mengi kwa namna hiyo imekuwa ni kawaida kwa
mtu asiyeokoka kuamini anamjua Mungu
kama kuokoka namna hii basin a yeye anamjua Mungu na hali hii imekuwa ngumu
sana katika kuwatofautisha watu waliookoka na wasiokoka! Lakini jambo alimtishi
kwa mtu ambaye ameamua KUMPENDA MUNGU KWELI.
Nipende kusema kuwa
KUMJUA MUNGU sio kitu kidogo na wala sio kitu kigumu sana kipo na kinawezekana
tu endapo utakapoamua kwa dhati kuwa sasa nataka kumjua Mungu. Kwani katika
kumjua Mungu ndivyo unaweza kukaa naye katika ubora na kumtumikia kwa uhuru
zaidi pasipo mashaka yoyote.
Na mtu anaye mjua Mungu
kamwe hawezi kujiona kuwa amefika kiasi kwamba Mungu amekuwa shemeji yake hivyo
anaweza kumtania anavyotaka kana kwamba ameenda kule aliko Mungu na hatimae
amerudi kutusalimia tu!
Kumjua Mungu ni kitu
kingine na mtu anaye mjua Mungu ni kitu kingine anaweza kumdhihirisha Mungu kwa
uhalisia na watu wote wakamuona pasipo shaka na wakaelewa na kukubali kuwa huyu
ni Mungu mwenyewe wala hakuna udanganyifu wowote.
Sio swala lakusema mimi
na mjua Mungu kama kusema hata viumbe wengine wanaweza sema tena vizuri
haijarishi wanaelewa au awaelewi!
Kuna kuanza KUMJUA
MUNGU na kuendelea KUMJUA MUNGU!
Yote inakutegemea wewe
binafsi unavyoenenda na Mungu na sio namna unavyoenenda na rafiki, mchungaji
wako.
NAJUAJE NA MJUA MUNGU!
I.Mtazamo
wa Mungu katika maisha yako.
Ni kweli maisha yako ni
bora kuliko Mungu au Mungu ni bora kuliko maisha yako!
Ukitazama maisha yako
kama kioo ni kweli unaona thamani ya Mungu katika maisha yako. Unapoona maisha
yako ni kweli unaona nafasi ya Mungu katika kunawiri au kuwa mshindi katika
maisha yako. Ni kweli moyo wako unaona uzuri wa Mungu, upendo wa Mungu
ukidhihirika katika maisha yako?
Ni namna unavyomuona
bila shaka ndivyo utakavyoishi maisha pamoja na Mungu au mbali na Mungu
ahijarishi unaenda kanisani au ahuendi kanisani!
Nidhamu yako mbele za
Mungu ndio itakupa mwenendo wako na Mungu katika uharibifu au katika ustawi.
Maisha (ni mwenendo
binafsi unavyoenenda kila siku) sio familia bali ni namna unavyo muona Mungu
alivyo wa muhimu katika maisha yako ni vile unaona pasipo msaada wa Mungu ni
ngumu kutoka pale ulipo ni ngumu kuwa salama pasipo yeye kuhusika na maisha
yako.
Wako watu wanaona bila
kitu Fulani maisha yao ni taabani mathalani bila mchumba,kazi,rafiki maisha
yangu hayaenda inavyotakiwa .
II.Mtazamo
wako juu ya changamoto zako.
Matumaini ya moyo wako
yanapo didimia ni kweli roho yako ina nguvu ya kusimamisha na kuendelea
kumwamini katika NJIA SAHIHI.
Hapa ndipo unaweza
kuona maajabu unaweza kukuta mtu anabiblia alafu ana hirizi, hivyo akienda
kanisani anabiblia na akirudi nyumbani anaiamini hirizi au kingine chochote
mbadala wa Mungu.
Mbali na hilo unaweza
kukuta mtu aliyekuwa na imani nzuri yenye utisho ukakuta amekuwa katika imani
isiyo sahihi kabisa nay eye uko amezama sana.
Ukisikia kiini cha
mwanadamu kutoka kujidhihirisha ana amini nini aua anajua nini ni hapa katika
kiti moto kitakachomfanya awaze kukaa lakini aone uwezekano wa kukaa kuwa
imeshindikana, akasikia hali ya kukimbia lakini akakuta anashindwa kukimbia kwa
kufupi lile analowaza sio lile analolitenda.
Changamoto zipo kwa
ajili ya kuinua uende katika daraja linguine na inapokuwa shida kwako kufaulu
kwenda katika daraja linguine ndipo hapo unaweza kuchukua muda mrefu katika
hatua Fulani pasipo kupata.
Kumjua Mungu ni namna Mungu anavyozifunua siri zake! Ili uimarike
zaidi.
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson……………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni