Jumanne, 31 Mei 2016

GOD'S PROMISE



AHADI YA MUNGU


Kama kuna kitu ambacho utakiwi kuweka mashaka atachembe!...wala moyo wako kushuka chini na hata fahamu kupoteza muelekeo ni hiki kitu kinaitwa AHADI YA MUNGU! Nitangulie kusema tu maadamu unaishi ndani ya dunia hii jua ahadi ya Mungu juu ya maisha yako ipo kama isingelikuwepo isinge likuwa ya maana ya wewe kuwepo duniani, hivyo uhitaji kuomba ahadi ya Mungu jua zipo na zitakuja kwa namna yake kutokana na mfumo na utaratibu wake.

Yeremia 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Haya ni maneno ya Mungu yanaishi na yana nguvu mpaka leo! Ni akili yako ni kutambua tu.
Ni pende kusema tu ahadi ziko nyingi…..ziko zinazo toka kwa wanadamu, miungu na MUNGU lakini kamwe haziwezi kufanana lakini nikubaliane tu kuwa kila ahadi ina taratibu zake na ili uzipate ahadi zake basi hauna budi uzifuate hizo kanuni zake kwakua ndani ya taratibu zake huko ndiko ahadi upitia.

Najua yako malengo mengi ya ahadi lakini mimi niseme malengo machache tu:
i.                    Kufanya uwe na furaha
ii.                  Kufanya uzidi kuimarika pasipo kuchoka
iii.                Kudumu katika mwenendo mzuri
iv.                Kufanya usahau mengine na kuweka bidii katika jambo husika

Nikubaliane tu ahadi imetumika sana katika maeneo mbalimbali mathalani ofisini bosi anaweza kukuambia ukiifanya vizuri kazi hii kuna zawadi nitakupa au kukuongeza kima cha mshahara wako na nyingine nyingi, katika familia wazazi wengi wamekuwa waki waahidi sana watoto wao zawadi ilikuwafanya watoto  wasome kwa bidii au wabadilike kutoka katika tabia fulani ambayo wazazi/mzazi afurahishwi nayo.

Nipende kusema tu kuwa ahadi ya Mungu juu ya maisha yako ni zaidi ya kukopa salio katika mitandao ya mawasiliano (voda,tigo,zantel,airtel) na pindi utakapoongeza salio kwa njia ya kawaida utaona meseji watakayokuandikia “asante kwa kurudisha deni lako” japo kuwa tunaona ni mtandao uliotengenezwa na hiyo program kuanza kufanya kazi…..lakini ahadi ya Mungu kumbukumbu  yake ni zaidi ya hapo kamwe haiwezi kuwa rahisi kusahaulika!

Ahadi za Mungu ni nyingi katika maisha yako na katika mwendo wako na Mungu bila shaka utaona mambo mengi wala usijue haya mambo mbona sikuyajua wala sikuwai kumuomba bali yatakuja kwakua yeye kama baba anajua wajibu wake kwako na atatoa kwakua  hilo ni jukumu lake.

Mathayo 6: 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

Na wakati mwingine unaweza kujua baadhi ya ahadi ya Mungu katika maisha yako, Ni ukweli usiopingika kuwa hivi ni vitu viwili tofauti sana kati ya kutambua ahadi ambayo Mungu amekuwaidi na kuipata ahadi hiyo, kwani kuna mchakato mrefu sana(majira sahihi) na hapo ndipo kuna kuwa ni kipindi kizuri cha kupima PENZI LAKO kwa Mungu.

Warumi  4:18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
             19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
             20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
             21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.

Tunaona ibraham japo Mungu mwenyewe alimuahidi lakini alihitaji kutiwa nguvu na Mungu mwenyewe ili kuifikia ahadi yake.

Kama nilivvosema hapo awali kuwa kila mtu maadamu uko duniani unayo ahadi ya Mungu katika maisha yako hasa mtu uliye okoka unapata kibali kuishi katika maisha yanayoambata na ahadi ya Mungu kwa asilimia mia, lakini kutokana na mabadiliko ya dunia imekuwa ni changamoto sana acha mbali na sayansi na teknolojia bali hasa injiri ya sasa imekuwa ikiwapa watu njia fupi katika kuwapatia mapumziko ya shida zao mathalani maombezi kwa wagonjwa kwa namna ya kimwili fedha imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na hilo wa kristo wengi wanashindwa kudumu katika imani zao za kweli kutokana na misingi waliyo ibeba sio imara imara zaidi.

Mathayo 7: 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
                      25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
                     26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
                      27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa

Nipende kusema ahadi ya Mungu ni amina na kweli na kamwe awezi kusahau ila uzidi kudumu katika yeye kwa majira yake atakutoa na kuchomoza!

Sina maneno mengi zaidi ya kusema!

Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………….0764 018535

BARIKIWA SANA RAFIKI

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni