ACHA IPITE
Kibinadamu uwa atupendi mazuri yapite…… bali tunaomba usiku na mchana kuwa mambo mazuri yazidi kuwepo sikuzote wala yasikome kamwe lakini katika upande wa mambo mabaya tunapenda yaondoke haraka sana yaani kufumba na kufumbua hilo jambo liwe limetoweka kabisa.
Unaweza ukawa katika eneo ambalo kwa kipindi fulani kukawa na hewa nzuri sana na nafsi yako pamoja na mwili wako ikapafurahia sana lakini kama hiyo hali ya hewa ni ya kipindi tu bila shaka itaondoka atakama utakuwa umeipenda kiasi gani! Mbali na hali ya hewa pia kuna hatua katika mwanadamu inayojulikana kama hatua ya ujana ambayo wanadamu wengi wanaipenda sana lakini kwa uhakika ujue tu kuwa kipindi hicho uwezi kudumu nacho siku zote ahijarishi ataukifanya mazoezi kiasi gani ili kuutunza ujana wako bado mwili utakataa tu! Unaweza ulikuwa na mtu ambaye uliye mpenda sana, kumuheshimu na kumthamini lakini usiopingika kuwa kuna majira mtaachana tu kwa kupenda au kutopenda! Unaweza kuipenda siku kwa namna ilivyokuwa na usiitamini ata usiku uingie lakini kwa kutamani kwako usiku usiingie ni kweli hautaingia ni swali jepesi.
Wako watu wengi sana wamekuwa katika hali mbaya sana pindi wanapokuta kuna kitu alichokipenda sana na kuona sasa kimeshatoweka na hakuna la kufanya uweza kuugua ugonjwa wa kichaa, shinikizo la moyo na wengine ufika mbali sana hata kutaka kujiua kwa kuona kile alichokipenda au alichojivunia akipo tena hivyo ana amini sasa aibu imesha mfika na hakuna njia nyingine ya kurejesha furaha yake.
Acha ipite inaweza kuwa katika hali ya kukosa au kufukuzwa kazi, kupoteza rafiki, mpenzi, na hata ndugu! Kinachoweza kuwatengisha katika kuachishwa au kuachana mathalani kusafiri kwenda mbali sana ambako kumuona si rahisi tena au kufungwa jera kwa muda wa miaka mingi kiasi kwamba uhuru wako hautakuwepo tena.
Isaya 40:8 Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.
Najua kwa uhalisia ni ngumu katika kuyaruhusu mambo mazuri kupita japo ingekuwa ni amri yako usingeweza kukubali hali hiyo itokee lakini mambo mengi kutokana na asili yake ni lazima yapotee tu…..aijalishi unapenda au haupendi.
Na sio mbaya kujua kama kitu kilikuja basi pasipo shaka kitatoweka tu ila shida inakuja pale kutojua ni wakati gani hiki nilichonacho kitatoweka na je! Utakuwa radhi pindi kitu kitakapo toweka. Najua kuna mambo mengi yanapotoka kwako hasa yale uliyo yapenda na kuyawekea malengo mazuri uwa moyo wako unakuwa katika hali ya chini.
Niseme kuna kuwa na wakati mzur(jicho jingine) katika kuacha hali kwanza kutoweka na hatimae kuchipuka katika hali nzuri, wakati watu wameinuka sana pale walipoamua kuachana na vitu vya awali na wakati mwingine ilikuwa katika hali ya maumivu lakini mwisho wake ulikuwa bora kuliko mwanzo wake.
Na katika kipindi cha kuacha kitu kipite usipokuwa makini unaweza ongeza maadui kuliko marafiki na kuwa mbali hata watu wale ambao ulikuwa unawaona kuwa ni watu wazuri ukaanza kugeuza moyo wako na kuwapa mtazamo mwingine.
Najua inaweza kuwa ngumu au kuchukua muda katika kukubali kuwa imesha tokea na imeshakuwa na hapo kukubali kuwa imeshatokea kutokana na majira yaliyopo sasa lakini bado yule aliyenikutanisha au aliyenipa nafasi bado yuko anawezafanya makubwa kuliko vile ninavyowaza na kuhofia sasa itakuwaje? Mbona hivi au nitakamilishaje ndoto zangu usihofu aliyeweka ndoto atazitimiza tu kwa namna yoyote maana ameziweka kwa ajili yake na kusudi lake kamwe aliwezi kuzuiliwa kamwe.
Lazima utambue ukubwa wa Mungu wako na Upendo wake usio kuwa na mipaka wala kizuizi chochote kwani bila yeye hakuna kilichofanyika na ndani kuna kushamiri na ubora usio koma kwakua ndani yake asili ya kuzalisha vitu vikubwa vikafanya mwisho ukawa mkubwa kuliko mwanzo.
AMINI MUNGU HAKOSEI WALA ACHELEWI!
Imeandaliwa:
Cothey Nelson………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni