IPENDE FURAHA YAKO
Furaha ipo kwa ajili
yako na sio wewe uwe kwa ajili ya furaha!
Furaha haina uchaguzi
wake bali wewe ndio mwenye mamlamka na hiyo furaha…..ni kutambua tu kuwa wewe
ndio mwenye kauli ya mwisho katika kuitawala furaha yako na wala sio kitu
kingine.
Hakikisha hakuna jambo
katika maisha yako lenye kauli au lenye nguvu katika kuiondoa furaha katika
maisha yako iwe kuchekwa, kusemwa, kuhisiwa vibaya au kutothaminika ni vizuri
kutambua furaha ni zaidi ya hapo au ni zaidi ya hayo.
Moja ya kipenzi cha
wengi katika dunia ya sasa ni FURAHA na kwa kawaida furaha uwa ni rafiki wa
moyo kwa kua moyo ukifurahi basi na sura itachangamka na hatimae mwili mzima
utakuwa unakuwa katika hali iliyo njema katika kuondoa makunyazi yake.
Na nzuri zaidi sana
kila mtu ana changamko la moyo binafsi wala aliingiliani na mtu mwingine
ndomana unaweza kukuta huyu analia na huyu anacheka, hapa kuna msiba na huku
kuna harusi kwa kila mtu anakuwa na upande wake, bila shaka natambua au
kukubaliana katika mwendelezo wa furaha unategemea sana msingi wa furaha yako
wako watu furaha imebebwa na msingi wa kazi nzuri au usafiri mzuri na mangine
mengi.
Nakubaliana kwa
asilimia zote ufanisi mwingi katika utendaji ubebwa na moyo wenye furaha kwa
kuwa moyo wa furaha utengeneza utulivu wa akili na upelekea ufanisi wa utendaji
na hatimae uzalisha ubora na tija katika jambo husika.
Katika ulimwengu wa
sasa kuwa na furaha ni jambo la kawaida lakini katika kudumu furaha imekuwa ni
shida kwakua watu kuto kutambua misingi sahihi ya kuwa na furaha hivyo inakuwa
kama mfa maji maji aishi kutapatapa hivyo watu wanaishi kama nguruwe leo una
muosha na baadae anajichafua.
Nipende kusema kuna
kuwa na furaha iliyo na asilimia 0%,20%,40% n.k lakini furaha ya kudumu katika
maisha ya sasa inawezekana kama ukitambua msingi sahihi wa furaha yako, kubwa
zaidi lazima uipende furaha yako na ujue wewe binafsi unahitaji furaha yako
siku zote maana ni haki yako na Mungu anataka uwe na furaha wakati wote.
Wako watu wamejiwekea
kuwa furaha sio maisha yao bali uja kwa kipindi fulani na kuondoka hivyo
kutokuwa na furaha anaona ni jambo la kawaida kuona anastahili kutokuwa na
furaha na wala ashangai yeye kutokuwa na furaha kwa kua ana amini kuwa furaha
ni swala la kitambo tu.
Ni tatizo kubwa zaidi
kwa mtu anaishi pasipo furaha kwani watu wa namna hii kuchukua maamuzi ambayo
yata hatarisha maisha yake ni jambo la kawaida mathalani ujambazi, ukahaba,
ukatiri na hata kujifikiria kujiua niseme mtu aliyekosa furaha uwa aogopi
kujitoa mwanga na kuhatarisha maisha yake, ukifuatalia vizuri utakuta watu
wengi wanafanya maamuzi magumu ya kuhatarisha maisha yao na hata ya jamii husika ni watu walioumizwa
au waliokosa furaha.
Ishara nzuri ya
kuipenda furaha yako ni kuituza na kutotaka ipotee kwa haraka katika maisha
yako kwani ndani ya furaha kuna ubora katika maamuzi husika yenye tija na
manufaa katika jamii yako kwa ujumla kwakua ndani ya furaha ya kweli hakuna
ubinafsi unaotawala ndani yake hivyo utafanya kuwa ni kitu cha Baraka na cha
maana sana.
Niseme unahitaji kuwa
na furaha katika maisha yako katika hali zote njema na sio njema katika
muonekano wa macho ya nyama, lakini bado furaha yako inakuwa imetuzwa na Mungu
mwenyewe kwa kuwa ndani yake kunatumaini lisilo na sababu linaibuka ndani yako
lenye kuonyesha njia na ustawi usio na mashaka katika hazima yako iliyo njema.
Hatuhitaji furaha ili
tufurahi tu bali tunahitaji furaha ili tuweze kufanya mambo katika hali
iliyosahihi isiyo jaa kisilani wala chuki yeyote kwani nje ya furaha ya kweli
kushindwa ni swala la kawaida.
Hakikisha furaha yako hauwiruhusu
itoke katika maisha yako kwakua mwenye uwezo wa kuiruhusu furaha itoke ni wewe
na kuimiliki ni wewe kwani iko chini ya himaya yako. Ni vizuri utambue kuwa
furaha haipo kwa kitambo ipo katika maisha yako yote.
Wafilipi
4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni