NJE YA AKILI
1 Wafalme 4:29 Mungu akampa
Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.
Binadamu utambuliwa na
hata kuheshimiwa kutokana na matumizi ya akili yake, kwani watu wengi
wamesaidia na kuwa wa maana katika jamii kutokana na matumizi mazuri ya akili
au hali ya kuiruhusu uweza wa Mungu kufanya kazi kupitia akili zao na hatimae
kuvumbua vitu mbalimbali na mwisho kuzaliwa MTAALAM au mtu aliyebobea jambo fulani
na kulielewa zaidi katika jambo fulani.
Zaburi
36:3 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda
mema.
Mithali
12:8 Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili zake; Bali mwenye moyo wa ukaidi
atadharauliwa
Kwa mtu ambaye
anaonekana hana matumizi sahihi ya akili yake basi uweza kuitwa chizi, kwa
maana hana matumizi sahihi ya akili yake binafsi……kwa maana nyingine mtu
anayefanya jambo ambalo ni hasara maana alina faida katika jamii yake zaidi ya
hasara basi uitwa chizi lakini kwa mtu anayefanya jambo ambalo sio la kawaida
katika jamii husika ambalo likazalisha tija katika jamii husika uitwa mtaalam.
Zaburi
49:20 Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama
wapoteao.
Matumizi ya akili
yaliyo sahihi ni kitendawili kilicho na maswali mengi katika kutaka na kujua
hivi ni nini maana ya matumizi sahihi ya akili na namjuaje mtu aliye na
matumizi sahihi ya akili mathalani ukiweza kurudisha akili yako katika enzi za
NUHU ukajichukua nawe ukawa mmoja wa wananchi waliokuwa wanaishi mahali ambapo
nuhu yupo ni kweli ungekubaliana na Nuhu kuwa kile anachojenga kina maana kweli
na kita wasaidia kweli jamii husika……..anajenga safina wakati katika jamii
husika hakuna historia ya mvua na mbaya zaidi safina kubwa sana, katika elimu
ya kibiashara tunasema high demand = high supply…….kwa maana rahisi mahitaji ya
bidhaa basi yaendane na usambazaji wa bidhaa, kwa maana halisi katika harakati
za Nuhu hazikuwa sawa kutokana hapakuwa na uhitaji wa safina kwakua watu
walikuwa hawaijui mvua.
Kwa maana hiyo wakati
mwingine katika mwanzo wa jambo unaweza usijue kama mtu kama huyu hichi anachofanya kweli ana matumizi sahihi ya
akili kweli? Lakini jibu la uhakika linaweza kuja pale mara tu ile picha iliyokuwa
katika kichwa chake au hazma iliyokuwa katika moyo wake itakapokamilika na
kuona picha inayoonekana au matunda ya kile anachokifanya mathalani mtu
anatengeza dawa na kuanza kuponya maisha ya watu.
Utofauti wa jambo
lazima uanzie kwenye utofauti wa akili kwa maana akili inapokuwa tofauti basi
bila shaka utendaji utakuwa tofauti na kuwa tofauti katika jamii husika…. Na
bila shaka wako watakao kukubali na wapo ambao hawatakukubali ila wanaweza
kukubali baadae.
Nje akili ya
kiubinadamu hichi ndicho kitu kitakachokutambulisha wewe na kukuweka katika
alama katika jamii yako na kubaki katika fahamu za watu kuwa kitu fulani
kilifanywa na mtu na kiliwasaidia watu wengi hivyo mioyo yao itabaki na
shukrani kwa tendo ulilolifanya.
Uvumbuzi unapokuwa
umetokea kwa namna yake bila shaka hata matokeo yake yatakuwa ya jinsi yake
kwakua kila uvumbuzi wajambo unaubora wake, na sio lazima ufanye makubwa sana
yakasababisha pawepo na mshangao mkubwa ni kitu chochote ambacho kitaleta
manufaa katika jamii husika kwa kiwango chochote kile.
Hauhitaji uwe na nafasi
kubwa sana ili uweze kufanya makubwa zaidi unahitaji kuwa na nafasi ndogo ili
ufanye yaliyo makubwa sana, kwa kuwa utendaji wa jambo na matokeo utegemea sana
na mipango iliyothabiti na sio nafasi kubwa.
Ili uweze kuimarika
mahali popote ulipo unahitaji sana upate ufumbuzi sahihi katika mazingira
husika kwa kutumia mapana ya akili yako, kwakua akili yako ni hazina tosha
inayoweza kuyafanya yale katika namna macho pekee hayawezi kutendeka.
Ni muhimu kutambua kuwa
utofauti wako utegemea sana na utofauti wa akili yako kwakua ndani ya akili
yako ndiko kuna zaliwa utendaji ulio na nguvu na wenye mafanikio.
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson…………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni