JIONE MWENYEWE!
Kioo kimekuwa kitu kinachotoa hukumu kwa watu wengi kama sio wote, wapo watu baada ya kujiangalia kwenye kioo wanajikubali sana na wapo watu wanaojiangalia kwenye kioo na kuona bado kuna mapungufu katika muonekano wao na kundi lingine pindi linapojiona katika kioo wanajichukia ghafla na bila kusahau marafiki zangu wengine pindi wanajiangalia kwenye kioo wanakuwa na hali ya kujikataa kabisa! Sijajua upande wako?
Lakini katika yote tunaona moja ya kazi ya kioo ni kutoa taswira yako lakini watu wengi wangependa kingepewa uwezo kuwatengeneza na kuwa sawa na fikra zao wakati huo zinavyopenda maana kila kipindi kunakuwa na mabadiliko katika kutimiza matamanio fulani.
Moja ya kitu ambacho kina wa kwamisha watu wasifike mbali na kuwa vile wanavyopaswa kuwa kwakua wamejikataa wenyewe binafsi na kuanza kuishi katika hatua za wengine…. japo unaweza usione shida kwa kuwa wewe binafsi umeshapenda mtindo wa kuishi kutokana na kuona mtu akienenda katika njia fulani na mbaya sana ikitokea amefanikiwa katika kiwango fulani basi wewe ukaona njia yake ndio njia yangu.
Mtu yeyote unaye muona kuwa yuko juu unaweza usijue mtu huyu mpaka kafika hapa ametengenezwa vipi au na nani? Na pengine huo mng’ao wake unao uona ujui msingi wake hasa nini hasa kimemweka hapo! lakini ndugu yangu umezama na kuishi maisha ya mtu mwingine kujiamini na kuona hivyo ndivyo unatakiwa kuishi.
Niseme tu ni vigumu sana kufanikiwa kwa kupitia nyayo za mwenzako ukiamini kwakua yeye kafanikiwa basi bila shaka nami nitafanikiwa pasipo kujua ili mtu afanikiwe kuna vitu vingi vinausishwa na bila shaka kuna vile anavyovijua muhusika na vingine havijui ila vina kuwa na mchango katika kumfanya mtu maalum katika jamii yake.
Niseme tu hakuna kitu kizuri kama kujiona wewe mwenyewe katika mwenendo mzima wa maisha yako kwani kinakupa kujiamini na kujisikia vizuri na wala upotezi muda kutafuta mtindo nje yako bali utumia muda kuvumbua vitu vilivyo katika maisha yako na vinakuwa na radha yako hivyo watu wa kikuona wewe wana ona namna yako katika mwenendo wako.
Sikatai kitu kinacho wafanya watu wengi wasiwe wenyewe moja ni haraka katika kufanikiwa wana amini sana kwakua mwenzangu alitumia njia hii na kufanikiwa basi hakuna shida hata mimi nikitumia njia hii ya mwenzangu nitafanikiwa pasipo kujiweka katika namna yako utachukua muda mrefu ili kufikia mahali ambapo mwenzako amefikia.
Sikatai kujifunza kwa wengine katika mambo yao katika ujumla wa mwenendo wao wa kufikia hatima yako lakini sio kuchukua maisha yao na kuanza kuishi kwa namna yao na ukijisahau kuwa wewe ni siri ambayo inahitaji wakati, mahali sahihi ili ijifunue na hatimae nawe uweze kujishangaa kama wewe unavyo washangaa wengine.
Ni vizuri utambue mtu yeyote unaye muona yuko katika mng’ao fulani jua alianza moja au alikuwa na mwanzao wake ambao kama ungeliangalia mwanzo wake usingeweza kuamini kuwa leo atakuwa vile unavyomuona……..kwani mabadiliko yakifika lazima yambadilishe katika mng’ao na sio lazima abadilishe ngozi yake bali ni katika kunawiri na kujiamini zaidi.
Ni ukweli usiopingika Mungu anapenda uwe vile alivyokuumba kwani yeye ndiye alikutengeneza na bila shaka analokusudi la wewe kukuweka katika namna/hali hiyo hivyo unavyojikataa bila shaka unataka kumrekebisha muumba wako na kuona yeye alikosea kukuweka katika mwenekano.
Niseme usiogope mwanzo utaanzaji bali ningekushauri uogope sana mwisho wenye kukudhihirisha wewe kuwa ni nani ambao utabaki kama ushuhuda katika maisha yako na katika jamii yako.
Usiogope kuchukua maamuzi hata kama ni magumu sana ili mradi yamebeba manufaa katika kesho yako ya chukue tu watu watakuelewa baada ya kuona yamekuwa vizuri.
Utofauti ambao Mungu ameuweka katika dunia ya sasa ni vizuri ungeheshimiwa ili hile picha yake ikamilike maana yeye akukuumba kimakosa na wala ahitaji kukosolewa kwa maana hata wewe ukujua kama utakuwepo ila yeye alijua basi heshimu maamuzi yake, na penda kufananisha hali hii ni kama mwili wa binadamu ukiwa na viungo vingi na kila kiungo kina kazi yake na kina namna yake japo inawezekana lakini sio vizuri kazi ya mikono ikafanya na miguu hasa kwa mwanadamu aliye kamili kila kiungo kiliumbwa kwa kazi yake.
Niseme vyovyote ulivyo wewe ni bora, unaweza , unatosha sana! Na hakuna mbadala wako!
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………..0764 018535
NIKISEMA SIKU NJEMA NITAKUWA SIJAKOSEA!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni