USIOGOPE
Habari msomaji!
Karibu katika neno la leo………..Nakubaliana kabisa kuwa neno
hili USIOGOPE sio geni machoni pako na uwa sio kila wakati linakuwa la maana
sana kwako kama hakuna jambo LINALOKUOGOPESHA! Na zaidi sana neno hili usiogope
nguvu yake utegemea sana nani amekwambia, natambua kwa uhalisi moyo unalipokea
neno pindi mtu anaposema USIOGOPE bila shaka moyo wako utatoa tafsiri ya mtu
huyo( kama anamaanisha kile anachokizungumza) kwako na ndipo utakapoitikia sawa
na tafsiri iliyotolewa na moyo japo wote wanaweza wasijue lakini wewe katika
uhalisi wa moyo wako utatambua, Mungu atusaidie.
Ukiachana na hali hiyo, najua neno hili USIOGOPE linanguvu na
la maana sana kwa mwihitaji wa neno hili kama maji kwa mwenye kiu, sikatai wako
watu wamepitia shida nyingi hivyo wamesikia sana hili neno USIOGOPE maana kila
mtu anayeenda kumpa pole anamwambia USIOGOPE MUNGU YU NAWE! Lakini katika yote
bado neno USIOGPE lina hitajika sana leo kesho naam siku zote maadam tunaishi
basi tunalihitaji hili neno………na pindi utakaposikia moyo wako unaweza kuinuka
na kuona nami nina watu wanaonipenda! Asante Mungu kwa hili.
Neno USIOGOPE limetafsiriwa na kupewa maana nyingi zilizotolewa na watu mbalimbali
mashuhuri na wasio mashuhuri na zenye maana nzuri na zenye kuvutia napengine zinasadifu
na ukweli wa hilo neno…….. maana yangu katika neno hili USIOGOPE ni hali ya moyo kuhofia kupoteza furaha yake.
Nakubaliana kwa asilimia zote MTU akikwambia USIOGOPE na
MUNGU akisema USIOGOPE haya ni maneno sawa ila kutokana na chimbuko tofauti
lilikotoka basi yamebeba maana tofauti na upokeaji wake uko tofauti na mwendo
wake hapo utakuwa ni tofauti, kwani binadamu hata awe na mali kiasi gani na
hata akikuhurumia kiasi gani bado ubinafsi utatawala tu ila Mungu anapenda vile
anavyoishi basi nawe uishi hivyo ikiwezekana YEYE AISHI KUPITIA WEWE.
Unaweza kujiuuliza Mungu atasema lini kuwa mimi NISIOGOPE kwa
maana katika maisha naona watu na vitu vinavyoizunguka DUNIA nitajuaje Mungu
sasa ananiambia NISIOGOPE swali hili linaweza kuulizwa na mtu anayeenda
kanisani au msikitini na hata Yule ambaye sehemu zote haendi lakini sio mtu
ambaye anaye MJUA MUNGU katika Roho Mtakatifu.
Kama msomaji mzuri wa biblia unaweza kugundua neno UOGOPE
alina mashiko katika kitabu hiki zaidi ya neno USIOGOPE lenye maana kubwa ukilitazama kwa jicho la
rohoni lililobeba tafsiri ya Mungu uwa hakuna shaka utatambua KUTOOGOPA ndio
maisha ya MUNGU kwakua kupitia yeye vyote vilifanyika na pasipo yeye
akikufanyika chochote kilichofanyika!
Kiufupi tu maisha ya KUTOOGOPA ndio maisha tunayopaswa kuishi
kwani kiasi kikubwa upelekea kufanya kitu kwa ubora zaidi kuliko mtu anayefanya
jambo akiwa ana hofu uhakika unakuwa mdogo wa kufanya kitu kwa ufasaha zaidi,
siwezi kukudanganya kuwa utakuwa na hali ya kutoogopa kwa namna ya kawaida
maadamu umezaliwa tu! Sio kweli bali NENO LA MUNGU litakupa ujasiri usiokuwa wa
baadhi matukio au watu fulani kwani ndio ujasiri mwingi uliopo dunia wa namna fulani
lakini sio wa wakati wote kwakua msingi wake haujajengwa katika ujasiri wa kila
kitu bali wa baadhi ya vitu tu.
Niseme tu hata kama utakuwa mtaratibu vipi na mwema sana
ukisha iruhusu HOFU ichukue nafasi hapo kutenda kinyume na ulivyopanga ni
rahisi kwani unaweza kukusudia jambo jema lakini kutokana na HOFU ukajikuta
ufanyi au ukafanya tofauti,
Maisha yanayoambata na hofu yanapelekea kuwa mtumwa kwani
unakuwa kifungoni ambacho umejiweka wewe mwenyewe kutokana na hali ya ndani
inayokusukuma,……….maisha haya ya uwoga uweza kusababishwa na mtu unayetembea
naye na kumpa nafasi katika maisha yako hivyo maisha yake yatakuathiri kwa
kiasi kikubwa.
Ukitaka kuishi maisha ambayo sio yako basi ishi maisha
yanayobebwa na UWOGA utaishi kila mtindo wa maisha haijarishi unataka au
hautaki, bali ukitaka kuishi maisha ambayo Mungu amekukusudia ishi maisha
yanayo ongozwa na NENO LA MUNGU! Upate ujasiri na akili njema sio kwa kukulupuka.
Maisha ya ujasiri ni maisha ya kumwamini Mungu na
kumpenda kunakopelekea KUJIAMINI na sio
maisha ya utemi na ubabe katika kujisahau kuwa wote ni kazi ya Mungu.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………0764 018535
TUMIA MUDA WAKO KUJIONA
WEWE NA SIO MWINGINE!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni