ANAITWA MUNGU!
Unaweza kumwita mwenye nguvu, wa huruma, wa upendo, wa amani,
mponyaji, mfariji hizo zote ni sifa zake lakini kamwe haitabadilisha kuwa yeye
KUITWA MUNGU! Karibu sana,
Uhitaji kuchoka sana katika maisha utakapoenda katika njia
ambayo Mungu amekuagiza kuenenda wewe tambua kuwa yeye anaitwa MUNGU hakuna
jambo au hali yoyote ambayo itaweza kuzuia KISHINDO chake kwakua badala yake
hakuna na nafasi yake inabaki kuwa yake.
Uwa yeye hazuiliwi ila anaweza zuia! Achoki ila anaweza
kukuchosha! Asahau ila anaweza kukusahaulisha! Achelewi ila anaweza
kukuchelewesha! Apatoi ila anaweza kukuchelewesha ANAITWA MUNGU!
Haitaji umsaidie ili ufike mapema yeye mwenyewe anajua namna
ya kukufikisha! Ahuhitaji kujipenyeza ili uonekane, ila yeye atajidhihirisha
nawe utaonekana tu! Tembea katika hatua zake tu utafika tu maana hakuna
aliyetembea katika hatua zake akaishia njiani/akashindwa kufika.
Hana uhitaji ndani yake ila mimi na wewe tunaweza kuwa na
uhitaji lakini anajua namna ya kukutosheleza pasipo kukwama kwakua unajua njia
ya yeye kukupa uhitaji wako…mathalani yesu alipo gundua ana deni ndipo akaamuru
mwanafunzi wake kwenda kuvua samaki kisha achukue samaki na kumtoa fedha alafu
akalipe madeni wanayodaiwa.
Nipende kusema hali ya wewe kuwa na uhitaji hilo ni jambo la
kawaida kwakua katika biblia watu walikuwa nauhitaji mwingi mathalani sara(uhitaji
wa mtoto), batromayo( uhitaji wa kuona kwani alikuwa kipofu), mwanamke mjane wa
serepta(uhitaji wa chakula) hivyo sio ajabu ya wewe kuwa na uhitaji wowote
kwani unachohitaji hapo ni namna Mungu
afanyike njia ya wewe katika kukutoa hapo.
Nipende kusema mahali ambapo akili yako itakosa mwelekeo
kwakua umeshatumia njia nyingi lakini bila mafanikio, huna haja ya kutafuta
mbaya wako mtazame petro alipo jaribu kuvua samaki usiku kucha bila mafanikio
alibaki palepale mpaka yesu alipokuja pale na kutamka NENO hivyo uhitaji
kutembea tembea huku ukiangalia labda huyu atanihurumia lakini tambua kwa kila
uhitaji una njia zake za kupata au kukizi uhitaji kwa maana rahisi hakuna
mtihani ukakosa majibu, japo wakati mwingine unaweza usipate majibu lakini
mtunzi wa mtihani anayo majibu.
Muono wa watu kuona kuwa umeshindwa sio kweli kuwa umeshindwa,
kwani kushindwa kwa mwili sio kushindwa kwa roho na nguvu ya mkristo iko ndani
ambayo ndio inazalisha kunawiri katika muonekano wanje na kama ujaanza kuchanua
katika muonekano wanje jua ni mbegu iliyokaribia kuchepua ni wewe kutulia
kuhakikisha mpaka inachipua.
Katika yeye kilindini kinaweza onekana nchi kavu, katika yeye
ndani ya giza totoro unaweza ukaokota dhahabu inayoonekana peupe, na katika
yeye unaweza kuvuka bahari kama unavuka barabara kwa miguu pasipo kuhofia
chochote, katika yeye unaweza kukaa na mnyama mkali mathalani simba au chatu na
bado ukaona usalama wako badala ya kuona ni hatari kwako wakawa ulinzi kwako.
Unaweza kukubali au kukataa! Unaweza kupenda au kutopenda!
Unaweza kuchukia au kufurahi! Unaweza ng’ong’ona au kutoa sauti! Unaweza kuwaza
au kutowaza! Hali yako au hali yoyote haiwezi badilisha hali hii kuwa yeye
ANAITWA MUNGU. Na kwa lile analolikusudia kamwe uwezi kulizuia lisifanyike hata
dunia yote ikiwa kinyume nae lakini yeye mwenyewe hawezi KUSHINDWA kutimiza
hazima yake.
Hana ushemeji na mtu au ushikaji na mtu kwa kutegemea kwa
wewe kufanya baadhi ya mambo unafikiri yapendazayo basi utapata kibali kwake
Mungu! Kama hajafurahi basi hajafurahi tu unahitaji uelewe na kusimama katika
njia upasayo kuenenda ili yeye afanye kama alivyokusudia na sio kufikiri
utamshawishi Mungu kwakufanya baadhi ya mambo ayafurahiyo.
Hauhitaji kufika mbali sana na kupata picha zisizo kukusaidia
katika maisha yako kama kuona hapa kuna ubaguzi, wenyewe, kujuana kwingi wewe
tambua kuwa ANAITWA MUNGU mahali alipo ndipo kuna kunawiri na sio walipo watu
wengi anapotengeneza njia hakuna awezae kuijua na hata kuizuia.
Usitafute mambo mengine yenye tija kwako na yasiyo na faida
kwa Mungu mathalani kujulikana, kusifiwa kubali kutembea katika hatua za Mungu
pasipo haraka kuliko kuwa na haraka pasipo kuona hatima njema katika maisha
yako! KAMA YAKO NI YAKO TU MAANA ANAITWA MUNGU mtawala wa dunia na vyote
vilivyopo ndani yake. Barikiwa rafiki!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni