USIIPENDE KESHO KAMA
UJAIMALIZA LEO
Hata paa likiwa linathamani kiasi gani lakini kamwe
hauwezi kulisimika kwanza alafu ukafuata
msingi wa nyumba! KARIBU
Ni muhimu tuanze na MOJA na kisha twende kwenye MBILI, sio
vizuri tu! ila pia inaleta maana! Ni vyema kuijenga vizuri msingi ili
ikurahisishie kujenga nyumba imara na paa iweze kuwa na maana kuwepo maana
dhuruba itakapo kuja haita iangusha maana usalama wa msingi utakuwa umeishikilia
paa basi nawe utakaa salama na sio salama tu bali utayafurahia maisha yako!
Karibu sana
Ni kawaida ya binadamu kupenda jambo jema na kuchukia jambo
baya ni kawaida sana! Na katika muonekano wa jinsi hii utaitwa binadamu wa
kawaida, kwa watu wenye akili zao watasema hasa huu ndio ubinadamu kuchukia
lililobaya na kupenda kitu kizuri!
Ni jambo jema sana kupenda kitu kizuri kwa kuwa kitu hicho
kimekuwa kizuri kwa ajili ya kupendwa na sio kuchukiwa maana hilo silo lengo
lake! Changamoto inakuja katika katika kukipata kitu kizuri maana kina vutia na
wakati mwingine kinaweza kuwa na ushindani katika kukipata maana ni kitu kizuri
hivyo kila mmoja anakihitaji japo inawezekana kwa lengo tofauti.
Sio kila jambo zuri utafikiria linafaa maadam umelifahamu
kuwa ni jambo nzuri kila jambo zuri linakuwa la maana sana pindi
utakapolitambua wakati wake sahihi! Niseme tu jambo sahihi linapofanywa katika
hali sahihi basi kunakuwa na uwezesho uliobeba usahihi katika kukustawisha
(mwenye akili njema).
Nikubaliane sana katika dunia ya sasa watu wamekuwa waki harakia
mambo ya kesho kabla yakuimaliza leo wakiwa wanasababu nyingi mathalani nataka
niwe wa kwanza mimi niitwe mvumbuzi au nisiwe boya, nikichelewa kitakuwa
kimeisha, uwa mimi sipendi kujuta nataka niwai mapema ili nisijute!
Niseme kweli kuna mambo yanahitaji uwe na haraka ili
kufanikisha mambo yaende sawa mathalani ajari lazima ufanyike uwezekano wa
kuhakikisha usalama wa maisha yao waliojeruhiwa na mengine mengi lakini kamwe
sio mambo yote au mengine yenye kivutio cha macho ya kakupa msukumo mkali
pasipo kujua huu ni wakati wake wa mimi kuingia huku au kufanya hili.
*** Ni muhimu kujua kwamba kama ujaitendea haki leo basi jua
hata kesho hautaitendea haki maana itakusumbua : usione watu wanakula basi nawe
ukaingia kwenye kula lazima uangalia kweli wewe una njaa na ni kweli hicho
chakula ni salama kwa kula! Na kweli ukila chakula hicho utashiba?
Ni muhimu kuwa na maswali yenye manufaa kwako ili kujiweka
katika nafasi ya kutofanya makosa yasiyo ya lazima pindi utapoingia katika
ulimwengu wowote mathalani URAFIKI, NDOA! Sio dhambi kuangalia katika ushirika
huo mambo gani yanaendelea na majukumu gani yanaongezeka ila sio kwa kupa hofu
bali katika kukupa kujipanga ili ufanye kitu kwa ubora pasipo KUMSINGIZIA
SHETANI MAHALI AMBAPO YEYE AHUSIKI.
Alafu sio ujinga kuikamilisha LEO ikawa ni msingi wako mzuri
wa kufanya KESHO kuwa yenye maana zaidi kwako, mathalani unaweza mtu anaweza
kuwa mikakati mizuri ya biashara yake lakini baada ya kuona mwingine anauza
zaidi kuliko yeye basi anafungua na yeye biashara kama ya yule jirani yake na
baada ya muda yule akaacha ile biashara na yeye akaendelea hata baada ya
mwingine kuacha pasipo kujua mwenzake ameacha kwa sababu msimu umeisha, au
kunamtindo mpya umeingia unaanza kusema mimi nimerogwa au hapa sio bure
alivyoondoka kaniachia uchawi ona sasa biashara inadoda.
Ishi maisha ya leo vizuri sana ili hata ikifika kesho
usihitamani JANA, kwakua ulitendea ipasavyo na hivyo imekupa msingi mzuri wa
wewe kufika hatua hiyo kwa ushindi.
Lazima uelewe kuwa Mungu aliiweka LEO na KESHO alikuwa na
maana kubwa sana basi heshimu hilo na hakikisha huna haraka ya KESHO kama
UJAIMALIZA LEO, kesho hipo tu hauhitaji kuikimbilia maana itakuja tu!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………….0764 018535
KESHO YAKO IKO MIKONONI MWA MUNGU! IKO SALAMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni