SIJIONI
Wako watu
wamekuwa waki wasumbua mafundi hasa wachereani kwakutaka mshono ambao utakuwa
ni moja ya mtu fulani ambaye anampenda anavyo vaa pasipo kujua kwanini yule mtu
alivaa vile? Ila wewe kwakua unampenda basi utamsumbua fundi utafikiri umemuajiri
wewe ili mradi tu ufanane na mtu ambaye yeye mwenyewe hata ataki kukujua! Sio
hao tu bali kuna watu wanaenda salon wakita minyoo/ kutengeneza nywele zinazofanana
na watu waliokichwani mwao nao wanatumia muda mwingi kumuelekeza mwenye saloon
kama yeye amelipia saloon siku nzima!
Ni jambo
ambalo mtu ulitegemea pindi anapojiangalia katika kioo ajione yeye maana hiyo
ndio kazi moja wapo ya kioo kumuonyesha mtu jinsi anavyoonekana ili
kumrahisishia katika kujirekebisha mahali penye upungufu ili kuwa bora zaidi au
kughara zaidi au kuwa na muonekano ulio bora zaidi.
Sijui
utajisikiaje pindi utakapoamua kujiangalia katika kioo ukawa UJIONI wewe ila
unamuona mtu mwingine je! Utachukia au utaamua kubadilisha kioo ili kupata
utofauti ili uone kama kuna mabadiliko yoyote! Au utajisikia sasa uko bomba!
Lakini katika
dunia ya sasa watu wengi wamekuwa wakitamani pindi wakijiona wasiojione wao
bali waone mfanano wa mtu mmoja mashuhuri katika ulimwengu! Na hata kuibuka
mitindo mbalimbali ya nywele, nguo, muonekano na hata ongea ya mtu imebebwa na
mtu mwingine!
Siongelei
wale wanaofanya vichekesho au maigizo bali nazungumzia mtu husika akiwa na
akili timamu katika kukubali mtu mwingine aishi kupitia yeye azidi
kumtambulisha mtu mmoja kwasababu yeye anampenda pasipo kujali wewe
unamtambulisha je! Wewe nani atakutambulisha? Wako watu wanaita swaga………..!
Ukiangalia
watu wanamna hii unaweza kusema wanaweza kumuuliza Mungu kwanini umeniumba hivi
ukiniumba vile hama kwanini mimi sikuzaliwa marekani ni kazaliwa bara la giza!
Ukimuangalia jinsi mtu anavyojiangalia namna anavyoenda ni vitu fulani hivi
ambavyo haviendani kabisa,
Kweli katika
ulimwengu wa sasa watu wengi wamepoteza utambulisho wao,utaweza kuona mtu sio
kwamba anatamani kufanikiwa kama mtu mashuhuri alivyo fanikiwa bali uanza
kuishi kivuli cha mtu katika muonekano usiofanana bali unaolazimishwa kufanana
mathalani mtu anampenda mchezaji messi basi utakuta mtu anataka kuvaa kaptura
kama anayo vaa messi pasipo kujua yeye anavaa vile kwa sababu ya nini sio hilo tu
hadi kutembea, kushangilia ili mradi yeye aonekane kuwa yeye ana mapenzi ya
dhati na mchezaji huyo.
Sio mfanano
katika hilo bali hali uoenekana katika fani mbalimbali muziki, mitindo na hata
filamu mtu utaka kuenenda katika muonekano wa mtu fulani, pasipo kujua kwa
kiasi kikubwa katika kufanya hivyo unapoteza utambulisho wako ambao Mungu
ameweka ndani yako ili kuleta msaada kwa
jamii fulani ambayo Mungu amekupa neema ya wewe kuwepo.
Maisha haya
upelekea kutoishi wewe bali yeye kuishi kupitia wewe inakuwa kama wewe ukupaswa
kuwepo kwakua pacha wako ameshatokea kwakua yote anayo yafanya yeye ndiyo wewe unayafanya baada ya
kuona yeye anafanya, bila shaka unakandamiza ile hazina ambayo Mungu ameiweka
ndani yako kwa kua unaiona haina thamani ila ya wengine ndio iliyo bora kwakua
imeshatambulika na kupata kibali mioyoni mwa watu! Pasipo jua kuwa hata wewe
ukiamua kukipenda kilicho chako watu wengine watakipenda tu na hata wasipo
kipenda wewe unamalizana na Mungu kwa kutumia kile ulichopewa na Mungu.
Kupenda au
kumkubali mtu katika kitu kizuri anachokifanya sio vibaya ila sio vyema
kupoteza au kutotumia hazina ambayo Mungu ameweka ndani yako! Maana utakuta mtu
anavyompenda mtu hadi unashanga……..utakuata anataka apige mswaki kama yule,
acheke kama yule, alale kama yule na hata kulia kama yule basi hapakuwa sababu
ya wewe kuwepo, tambua Mungu kumuumba yule na WEWE kuna sababu na wala haikuwa kwa bahati.
Kupenda kitu
kizuri anachokifanya mwingine ni vizuri kwani Mungu amesema TUPENDANE ni sawa
na ni vizuri lakini sio watu wakikuona wewe wamuone mtu mwingine kabisa ambaye
anaushirikiano na wewe kabisa.
Ni vizuri
kujifunza mambo mazuri kwakua ni jambo jema litakuongeza katika lile ambalo
unalolifanya ili liwe bora zaidi zaidi, kwani kila utendaji wa mtu una
mapungufu yake hivyo utakapo kuwa pale utajifunza vyema ili usifanye makosa
tena bali uendelee mbele katika ubora mpya.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson……………………………………………………………0764 018535
JITHAMINI UTATHAMINIKA-------JIONE
MWENYEWE MAANA WEWE NI BORA!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni