KINACHONIZUNGUKA KIMENITENGENEZA
Uwa atushangai sana kuona mmasai kuuza dawa za asili! Hama
akivaa mashuka yake na kutembea barabarani hilo linakuwa ni swala la kawaida tu!
Na pengine japo mtu anaweza kutembea na
rungu unaweza kumshangaa sana lakini pindi utakapo waona wamasai wengi
wakitembea na rungu na huku wakicheka hauta shangaa sana kama ulivyo muona mtu asie
mmasai ………….kwa nini? Na pindi unapomuona mmasai akila nyama ya ng’ombe uwezi
kushangaa sana lakini pindi utakapo muona mmasai anakula samaki bila shaka hapo
utaanza kuwa na maswali kichwani…………unafikiri ni kwa nini?
Tukiachana na wamasai maana hawa ni watu wazuri………..pindi
unaweza kutoka na rafiki kwenda hotelini, aliyetokea kanda ya ziwa ukaona
anaagiza samaki hasa aina sato bila shaka hauta shangaa…………hivi ni kwa nini?
Ila unaweza kushangaa kidogo kuona muhaya pindi akiona senene anasikia
kichefuchefu na kuhisi kutapika…..hivi ni kwa nini utashangaa!
Ukiwa mtafiti wa watu walifanikiwa/mashuhuri japo sio wote
ila kwa asilimia kubwa utakuta familia zao zilikuwa namna yake mathalani wana
muziki, wachoraji, wana michezo kwa ujumla wao ukiwafatilia vizuri kama sio tu
juhudi zake binafsi basi ata mazingira yaliyo mzunguka yalipa nafasi nzuri
katika kujifunza hicho kitu na hatimae akawa mahiri na kuwa kielelezo katika
jamii yake na hata ulimwengu mzima.
Ndomana uwezi kushangaa watu waliotoka sehemu fulani kuwa
wataalam katika jambo husika kwakua utakuta mtu amezaliwa na kukua katika
mazingira hayo na hatimae akaona hayo kuwa ndio maisha yake mathalani uwezi
kushangaa kuona watu wa kanda ya ziwa ni wazuri/mahiri katika uvuvi na upande
wa muziki kuona watu wana uwezo mzuri kutoka baadhi ya maeneo uwa mahiri sana
kuliko maeneo mengine mathalani unaweza usishangae ukisikia mtu toka MBEYA/KIGOMA
anaimba lakini unaweza kuongeza umakini kidogo pindi ukiona MCHAGA anaimba
sisemi watu hawa hawajui kuimba bali ni nadra kusikia.
Biblia inasema ushirika mbaya uharibu tabia njema! Kwa maana
kile kinachokuzunguka na ulichokipa nafasi kina nafasi kubwa ya kukuathiri
katika maisha yako na kukutengeneza kiasi kwamba mtu akikuona wewe atatambua
CHIMBUKO LAKO!
KARIBU!
Wako watu wamekuwa wakibadilika sana kutokana na mtu
aliyekutana nae au hali fulani katika maisha yake inawezekana katika faida au
hasara…….wako walikuwa watu wema sana ila baada ya kukutana na watu wengine
wenye roho ya ukatiri ikamvika na hatimae ukatiri ukawa ni maisha yake na wako watu
walikuwa wabaya na baada ya kukutana na watu wazuri wakawa watu wa maana sana
wenye faida katika katika jamii,taifa na katika mataifa.
Hivyo ni muhimu kabla ujamhukumu mtu ni muhimu ni muhimu
kutambua maamuzi yake ya leo yametengezwa na JANA yake ni muhimu kutambua jana
ilikuaje na ndipo utafute namna ya kumsaidia katika ufasaha zaidi.
Ndomana mtu uliye muacha kwa kitambo kidogo na pindi
unapokutana nae tena unaweza kukuta ana mabadiliko makubwa sana, inategemea amekutana
na nani? Ambaye amemtengenezea muonekano mpya
ambao una uona sasa, usishangai kumkuta sasa pombe amekuwa rafiki yake,
chumba chake kimekuwa fensi yake ya kutembea atoki tena kama zamani.
Unaweza kushangaa kuona mtu amekuwa na UPENDO, FURAHA NA
KICHEKO ukaona mbona amekuwa tofauti na mwanzo hakuwa hivyo, jua kuna kitu
amekutana nacho na hatimae kime mbadilisha
Nakubalina kwa asilimia kubwa ili mtu abadilike inategemea
nani ameungamanisha nae na mala chache sana kuona mtu anabaidilika yeye mwenyewe
tu labda NENO LA MUNGU na Mungu kwa namna yake!
Lakini kuna sababu zinazo wafanya watu wabadilike japo matawi
ni mengi lakini kubwa ni moja tu ni USHIRIKA! Unaweza:
i.
Urafiki
ii.
Ndoa
n.k
Unawa za kukuta mtu amebailika sana ni tofauti alivyokuwa
kabla ya kuoa/ kuoelewa au ajakuwa na rafiki na mtu fulani ambaye akaingia
katika maisha yake na kumtengeneza katika muonekano mwingine unaweza kuwa uliutegemea
au usioutegemea.
Hivyo ni muhimu sana kuwa makini katika muungamaniko ulionao unaweza
kukutengeneza kuwa mbaya sana au kuwa mtu wa maana sana!
NIKUTAKIE KILA LA KHERI!
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni