AMANI YAKE NDIO MWENDO
WANGU!
Yohana 14:27
Amani nawaachieni; amani
yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni
mwenu, wala msiwe na woga.
Yohana 16:33
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani
ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda
ulimwengu.
Kama binadamu kuna uwezekano
kuwa kuna mambo mbalimbali yanayoweza kukupa nguvu katika kuendelea kufanya
jambo fulani katika maisha yako, mathalani wako watu wengine wanasema
nisipofanya kazi watoto wangu/ wanaonitegemea wataishije? Kwa maana hiyo basi bidii
yake ya kazi inabebwa na majukumu yake yanayomkabili.
Na wako wengine
wanakuwa na msukumo wa kuendelea kufanya jambo jema kwa mtu aliye maalum kwake
kwakua kila anapompa zawadi mtu yule anayepokea zawadi anapotoa tabasamu kwa
ishara ya shukrani kwakile anachokipokea basi mtoaji ujisikia deni zaidi katika
kutoa ili azidi kuliona lile tabasamu!
Ni jambo jema sana
pindi unapofanya jambo jema kwa mtu unategemea sana aonyeshe moyo wa shukrani
na hapo ndani ya moyo wako utaona umefanya jambo jema basi hapo kunauwezekano
wa moyo wako kuwa na AMANI.
Na imekuwa ni jambo la
kawaida sana kuona mtu kuacha kufanya kitu haijarishi ni kizuri au kibaya hama
kuna maslahi makubwa au madogo pindi anapoona ndani ya moyo wake AMANI haipo.
Na unaweza kuona mtu
anaweza kufanya kazi katika mazingira magumu au yenye kipato cha chini sana
lakini bado ukaona mtu anabidii katika kufanya pasipo kuonyesha dalili yoyote
ya kukata tama, ukikaa nae mtu huyo bila shaka atasema ndani ya moyo wangu kuna
AMANI hivyo nafurahia kile ninachokifanya.
Kwahiyo tunaona
kufanya jambo katika kuwa na AMANI ni jambo la msingi sana kwani linakupa
mwendelezo wenye manufaa na wenye tija maana utafanya kwa ufanisi na pasipo
AMANI basi hapo ubora uwa mdogo.
AMANI YAKE NDIO MWENDO WANGU!
Kweli kuna amani
zinazozalishwa na vitu hasa vitu vinavyoonekana pesa au mahusiano yanapochanua,
lakini iko AMANI isiyo na mipaka, sababu zaidi ya yeye mwenye amani kuwa ndani
yako.
Niseme tu mtu yeyote
unaye muona aliyefanikiwa hasa katika utumishi wake mbele za Mungu lazima Amani
ya Mungu ndani yake ndio ilikuwa ina mtawala na kumtia nguvu na hatimaye
kumwezesha kudumu kuishi katika kusudi la Mungu
Na pindi unapokuwa na
amani hii basi lawama, chuki,kisilani haitakuwa maisha yako kwakua kila jambo
basi wewe utaona njia ya kufika kule unakokwenda kakua uliye mbeba ndani uwa
azuiliwi na sio mtu tu bali hata kitu chochote.
Pindi unapoamua
kufanya jambo kwa kufuata amani hii kamwe hauta kuwa na kusuwasuwa hama
kushindwa katika jambo ulilo liamua kulifanya katika dhamira ya dhati usio beba
kisasi.
Unapokubali kuishi
kwakufuata Amani hii unakuwa hauishi wewe bali ile amani itakuwa ikiamua katika
maisha yako na hata kuongoza hatua zako na zitakuwa salama sana kwakua mbeba
salama yuko nawe.
Niseme kama kweli unataka
kuona uzuri wa Mungu katika maisha yako lazima uikubali Amani yake itawale
katika hatua zako.
INAITWA SIKU! BARIKIWA
SANA.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson…………………………………………………0764 018535