Jumanne, 27 Septemba 2016

AMANI YAKE NDIO MWENDO WANGU!



AMANI YAKE NDIO MWENDO WANGU!


Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.

Yohana 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Kama binadamu kuna uwezekano kuwa kuna mambo mbalimbali yanayoweza kukupa nguvu katika kuendelea kufanya jambo fulani katika maisha yako, mathalani wako watu wengine wanasema nisipofanya kazi watoto wangu/ wanaonitegemea wataishije? Kwa maana hiyo basi bidii yake ya kazi inabebwa na majukumu yake yanayomkabili.

Na wako wengine wanakuwa na msukumo wa kuendelea kufanya jambo jema kwa mtu aliye maalum kwake kwakua kila anapompa zawadi mtu yule anayepokea zawadi anapotoa tabasamu kwa ishara ya shukrani kwakile anachokipokea basi mtoaji ujisikia deni zaidi katika kutoa ili azidi kuliona lile tabasamu!

Ni jambo jema sana pindi unapofanya jambo jema kwa mtu unategemea sana aonyeshe moyo wa shukrani na hapo ndani ya moyo wako utaona umefanya jambo jema basi hapo kunauwezekano wa moyo wako kuwa na AMANI.

Na imekuwa ni jambo la kawaida sana kuona mtu kuacha kufanya kitu haijarishi ni kizuri au kibaya hama kuna maslahi makubwa au madogo pindi anapoona ndani ya moyo wake AMANI haipo.
Na unaweza kuona mtu anaweza kufanya kazi katika mazingira magumu au yenye kipato cha chini sana lakini bado ukaona mtu anabidii katika kufanya pasipo kuonyesha dalili yoyote ya kukata tama, ukikaa nae mtu huyo bila shaka atasema ndani ya moyo wangu kuna AMANI hivyo nafurahia kile ninachokifanya.

Kwahiyo tunaona kufanya jambo katika kuwa na AMANI ni jambo la msingi sana kwani linakupa mwendelezo wenye manufaa na wenye tija maana utafanya kwa ufanisi na pasipo AMANI basi hapo ubora uwa mdogo.

AMANI YAKE NDIO MWENDO WANGU!

Kweli kuna amani zinazozalishwa na vitu hasa vitu vinavyoonekana pesa au mahusiano yanapochanua, lakini iko AMANI isiyo na mipaka, sababu zaidi ya yeye mwenye amani kuwa ndani yako.

Niseme tu mtu yeyote unaye muona aliyefanikiwa hasa katika utumishi wake mbele za Mungu lazima Amani ya Mungu ndani yake ndio ilikuwa ina mtawala na kumtia nguvu na hatimaye kumwezesha kudumu kuishi katika kusudi la Mungu

Na pindi unapokuwa na amani hii basi lawama, chuki,kisilani haitakuwa maisha yako kwakua kila jambo basi wewe utaona njia ya kufika kule unakokwenda kakua uliye mbeba ndani uwa azuiliwi na sio mtu tu bali hata kitu chochote.

Pindi unapoamua kufanya jambo kwa kufuata amani hii kamwe hauta kuwa na kusuwasuwa hama kushindwa katika jambo ulilo liamua kulifanya katika dhamira ya dhati usio beba kisasi.
Unapokubali kuishi kwakufuata Amani hii unakuwa hauishi wewe bali ile amani itakuwa ikiamua katika maisha yako na hata kuongoza hatua zako na zitakuwa salama sana kwakua mbeba salama yuko nawe.

Niseme kama kweli unataka kuona uzuri wa Mungu katika maisha yako lazima uikubali Amani yake itawale katika hatua zako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni