Jumanne, 4 Oktoba 2016

UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE.



UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE


Kwa maana ya haraka haraka unaweza kushindwa kuona uhusiano wa karibu kati ya haya maneno mawili UGUMU na UBORA! Kwa maaana ya kawaida kitu kigumu kinahusishwa kitu kibaya hama kitu ambacho kinachohitaji nguvu nyingi ili ukipate na pindi unapokikosa basi huitwa KUJICHOSHA hivyo hapo swali uweza kujitokeza katika mwisho wa namna hii, UBORA utatoka wapi?

Kuna namna lazima uwe ili uweze kuvipata vitu ambavyo havipatikani kwa urahisi………….uwezi kufananisha maisha ya mtu anayetafuta dhahabu kama mtu anayetafuta ng’ombe.

Ifahamike kuwa watu upenda kitu sio kwakua ni kigumu tu, kwa maana ya kukaa muda mrefu bali kwakua ni bora! Kwa maana kinakuwa na tija ile iliyokusudiwa,

Na ikumbukwe kuwa ugumu wa kitu utegemea nini kimfanya kuwa na ugumu na ubora wa kitu utegemea kile kinachotoka/kinachozalisha!

Katika  picha ya kawaida tu, uwa tunaamini kitu kigumu ndicho kinachodumu basi hapo tuna amini kuwa chenye ugumu ndipo hapo kuna ubora! Japo wakati mwingine sio kweli kwani sio kilicho kigumu kina ubora kwa kuwa vingine vinakuwa vimekomaa hivyo vinakuwa havina faida zaidi ya maumivu.

Samahani naomba niuongelee upande huu japo sio dhima ya ujumbe bali yote ni kukupa mwanga zaidi katika kile ninachotaka uimarishe akili yako ikawe katika njia inayostahili, watu wengi wana amini kuwa msichana mgumu ndio bora kwa kuwa sio rahisi kutoa jibu sawa hama nimekubali kuwa mtu wako katika kuanzisha safari ya kuwa pamoja! Swali langu alipo katika ugumu au uwepesi bali msingi wake/akili yake imeshikiliwa na nini katika kutoa jibu la kusema ndio au hapana……kwa maana rahisi katika hali hii uwezi kusema UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE! Japo wakati mwingune inaweza kuwa sawa lakini sio mara zote.

UGUMU WAKE NDIO UBORA WAKE!

Ni jambo la kawaida unapoendelea kusaga nafaka ndipo unawezidisha ulaini(kupondeka) wa hicho kitu unachokisaga!

Bila shaka unapotaka kutengeneza maandazi mazuri basi ahunabudi kukanda vizuri ngano  hatimae ile ngano yako iweze kuwa laini na hapo kutengeza ubora wa maandazi yako na kuzidi kutamaniwa na watu wengi!

Hakuna shaka ukitaka samaki wakubwa na wenye uzito mkubwa ahunabudi kuingia vilindini zaidi katika maji kule waliko ndipo uweze kupata  mbali na hapo utaishia katika kupata wale waliosawa na kina kile ulichoingia.

Unapoangalia katika ufalme wa giza unaweza usiuelewe lakini wenyewe unajitambua na kuhakikisha unakuwa pale panapohitajika na sio chini ya lile kusudio kwa kuwa chini  ni ishara ya kushindwa katika utawala wake, ndomana wako radhi kutoa uhai wa mtu yeyote katika utawala uliondani yao ili mradi kudumisha ufalme wao.

Na ukiingia ndani zaidi utatambua nafasi ya mtu utegemea uwezo wake katika sadaka inaweza kuwa miili ya watu, vichwa hama watoto wachanga, ukubwa wa sadaka ndio ukubwa wa mtu husika.
Na ndipo unaweza kuunganisha kuwa mateso ya mtu ndio nafasi ya mtu katika utawala wa ufalme huo kwakua sadaka kubwa inatakiwa kujitoa na kuteseka zaidi ili uweze kukamilisha ile shehena unayotakiwa kuileta katika ufalme huo.

Kwa maana rahisi katika ufalme huo sadaka yako ndiyo inayoamua nafasi katika ufalme iwe kubwa au ndogo sio kitu kingine kwakua uko ndiko kunaitwa kujidhabiu.

Unaweza kumuona mtu kuwa na muonekano na fahari yake ya kuvutia na ya kutisha lakini kamwe usijue UGUMU anaoupata katika kuhakikisha anakuwa hapo, mateso ya usiku wengine wanaambiwa kulala katika banda la kuku! Uwa ahuhitaji maswali zaidi ya kutekeleza.

KATIKA UPANDE ULIO BEBA USALAMA WA MAISHA!

Katika kuhakikisha ufalme kuwa na nguvu na kuzidi kuwepo kwa kishindo kisicho zuiliwa ukweli unahitaji watu, na sio kwa maana ya watu bali unahitaji watu waliotayari kuutumikia ufalme huo kwa moyo uliobeba dhamira njema ulio na maongozo ya Roho mtakatifu.

Bila shaka ukiona ufalme umelala basi tambua watu wake wamefanya ulale au watu wenyewe wa melala na ukiona umeanza kushamiri basi tambua watu wake wameamua kuutumikia.

Namna unavyojigharimu katika kuhakikisha ufalme unasimama na kuimarika basi nawe unazidisha nafasi yako mbele za Mungu na kanuni alizoziweka Mungu kuanza kuchukua nafasi katika maisha yako, katika kukufanikisha.

Mwanzo 22:15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni
                    16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
                    17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

Sio lazima utoe sadaka kubwa la kwanza yatoe maisha yako kwanza kuhakikisha ufalme wa Mungu unajengwa na mengine yatakuwa sawa,

Ukumbuke kuwa namna unavyojitoa ndivyo unavyotengeneza nafasi yako kwa Mungu, hivyo usijitoe kidogo ukategemea kuyapata makubwa kwa Mungu,

Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni