ACHA NIIKABILI KESHO YANGU!
Imekuwa kama fumbo katika kuiongelea “KESHO” wakati mwingine kwa hofu au hali ya kutokuwa na uhakika wa kuwa vile mtu anavyowaza hama vile anavyotazama ndivyo itakavyokuwa, na ndomana unaweza usishangae sana mtu anaposema “KESHO TUKIJAALIWA” hama mtu akisema wakati mwingine” MUNGU AKITUPA NEEMA” bila shaka wako watu wengine kutokana na uhakika unaombatana na macho yao wanasema KESHO ITAKUWA SAWA au KESHO NITAKAMILISHA kwasababu jambo hili ni dogo sana!
Wakati mwingine nikubaliane kuwa KESHO kama fumbo kwani unaweza kujigamba sana na wakati mwingine ukaona kama unamiliki kila kitu hivyo ukatumia LEO namna unavyo ona na KESHO ikawa vile unavyopaswa kuwa na sio unavyopenda.
Niseme tu kumekuwa na maana nyingi kuhusu KESHO na ni nzuri sana kwa maana wakati mwingine zinakuwa zimebeba ushawishi wa akili na hata kusadifiwa na mazingira yanayozunguka na namna unavyoona mambo yanavyotendeka.
KESHO KAMA HATUA INAYOFUATA KATIKA MAISHA YAKO!
Katika maisha kuna mwingiliano na muachano wa vitu vingi kuna vitu vinatoka na vingine vinaingia, uzuri ni kwamba kila mtu uomba usiku na mchana kuona KESHO yake inakuwa nzuri hata mtu kama yeye mwenyewe ahusiki kuifanya kuwa kesho iliyo bora.
Wako wajawazito wanaitamani kesho yao kupakata watoto wao wakiwa na furaha na amani na wakiona heshima yao imerudi hama imekuwa kubwa katika jamii na wakati mwingine kuona kama kaongeza heshima ukweni, lakini cha ajabu wako wenye mipango ya kuikimbia kesho yao kwa maana yakutaka kutoa mimba kwa sababu nyingi tu ambazo ufahamu wa mtu huyo utamdanganya mathalani huu sio wakati sahihi wa mimi kuzaa, baba wa mtoto amtaki mtoto wake, hama sikupanga kumzaa na mtu kama huyu!
Wako watu wamekuwa na uwoga katika kupandishwa cheo kwa hofu kuwa hivi hizi changamoto zake naweza kuzikabili hama naweza kufikia mafanikio yale niliyoaminiwa kwayo, wakati mwingine uweza kuwa na maswali ni kweli naweza kupata ushirikiano mzuri wa kuniwezesha kutimiza malengo…….. ujue kwamba aliyekupa nafasi hiyo amekuamini na kujua unaweza kufanya vizuri na kama kunauwezekano wa kuweza basi utaweza!
Pia kuna watu waliomaliza hatua fulani ya masomo yao inawezekana kuwa mtu alisoma nje sasa anawaza nitakaporudi nyumbani ni kweli nitaweza kufanikiwa katika lengo langu anaweza kuwa alifuatilia watu wanamna yake jinsi walivyo sasa wako walio fanikiwa katika njia zisizo halali na wengine hawajafanikiwa,
Na wengine walio maliza nchini wanaona maisha ya waliotangulia jinsi yalivyo kwa asilimia kubwa sio ya kuvutia kwa maana sikuhizi sio jambo la kushangaza mtu mwenye stashahada kuwa mmachinga wa kutembeza nguo barabarani!
Pamoja hayo ikumbukukwe kuwa kama hakuna mabadiliko basi hakuna maendeleo” No change No improvement”
Jifunze kuyafurahia mabadiliko yenye tija kwako ili yawe rahisi katika kuyakamilisha hata kama yana ugumu gani kwa kuwa moyo wako utakuwa tayari kupambana na chochote ili mradi tu utimize lengo lako
Ikumbuke kuwa vile ulivyoishi leo sio utakavyoishi kesho kwakua changamoto zake ziko tofauti mathalani unapokuwa pekee yako ni tofauti utakapoamua kuwa na mtu mwingine lazima ujiandae katika kubadilisha mtindo wako ili uweze kuifurahia kesho yako na isiwe mzigo kwako.
Ni kweli watu wanaogopa kuiikabili kesho wakati mwingine mtu kulizika vile alivyo hama kuipenda leo yake na asione umuhimu wa kesho yake, pasipo kujua inawezekana leo una nguvu ndo mana unaifurahia lakini kesho unaweza usiwe na nguvu hizo na kushindwa kuimiri kishindo cha kesho ukabaki katika lawama na hata majuto………ni kweli leo sio kesho!
IPENDE KESHO YAKO ITAKUWA NZURI!
INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni