DAKIKA MOJA KWA MUNGU NI NYINGI
Ndomana unaweza usishangae kukuta huyu anafukuzwa kazi na mwingine
anapata kazi, na wengine uchumba unavunjika na kwa wengine unaanza na mambo
mengi yanatokea na kuwa katika hali ya mbadilishano, kwa kusema hivyo tujue
kile kinachompata au kukikosa sio kila mtu uweza kuwa katika hali hiyohiyo
(vitu au hali hazifanani),
Biblia inasema;
Mwanzo 8:22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati
wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
Kwahiyo hatuna shaka na hili maadam DUNIA inaendelea kuwepo basi
namna yake itaendelea kuwepo kwa jinsi yake sawa na asili yake.
Ni kawaida tunatambua utendaji wa mtu uamliwa na uwezo wa uchumi
alionalo pamoja na matamanio ya moyo wake naam kuchelewa/ kuwai kufanikisha jambo lake mara nyingi utegemea
uwezo wa kulifanikisha (fedha, mikakati na dhamira ya dhati)
Ni vizuri kutambua kuwa utendaji wa jambo linalokukabili mathalani
unaweza kuishi katika hali ya kutoifurahia kwa muda mwingi na ukahisi kuwa hayo
ni maisha yako hivyo ahunabudi kuyaishi lakini utokaji wa mahali hapo kwa mkono
wa Mungu “sekunde” inaweza
kubadilisha historia yako.
Kwahiyo siku moja katika muda mchache unaweza kuzalisha hali njema
katika maisha yako ikaifanye siku yako kufungwa hiki hiacha akili katika hali
ya kutaharuki kwa namna ilivyofanyika ikitoa njia katika macho ambayo akiwa
kawaida.
Kuna wakati mwingine inakuwa ngumu sana katika kutoka katika hali
moja na kwenda katika hali nyingine iliyo njema sana kutokana akili zetu kuwa
tofauti na uwezo wa akili ya Mungu tunafikiri utendaji unaoaminika katika akili
zetu ndio unaohakisi mtazamo wa akili ya Mungu.
Ahutaji kuhesabu msoto wako kwani moyo wako utashuka bali tambua
dakika ya Mungu yawezafuta historia ambayo inaweza kuwa neno moja tu lililochukua sekunde mbili,
likarejesha nguvu na matumaini mapya katika maisha yako linaweza kuwa SAWA! UNAWEZA KUENDELEA! IMEKUWA!
Changamoto ya watu wengi walionao ni kutaka akili za Mungu
zifanane na wanadamu pasipo kujua akili za mwanadamu katika hali ya mwili hazina mwanga wa
uhakika.
Waamuzi 16:28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba,
ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi
juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
Tunaona Samson anafanyika kuwa mkombozi wa Israel japo kuwa
waliishi utumwami muda mwingi lakini ukombozi wa kiMungu haukuchukua miaka
mingi bali ndani ya siku moja katika masaa machache furaha ikarejea katika
himaya ya watu wa Mungu.
Nakubaliana
kuwa utendaji wa Mungu uko katika namna mbalimbali yapo mambo yanachukua muda
kutokana akili ya mtu kushindwa kuhimili huo utukufu lakini inaweza kuchukua
muda mfupi ajabu na ikabadilisha kabisa maisha yako.
Mungu
hayupo kukuchosha wala kukudhalilisha bali ni katika hali ya kukufanya uwe na
maandalizi bora ya kufaa kwa ajili ya ufalme wake katika nafasi atakayo kupa
utumike.
Usitazame
jambo katika ukubwa wake ikakuonyesha kuchukua muda mwingi katika kuishia/utatuzi
wake bali tambua inahitaji kauli ya Mungu tu itakayochua chini ya dakika na
mambo yatafanyika tu!
INAITWA
SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson……………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni