Jumanne, 13 Septemba 2016

NINI MAANA YA KUMUANGALIA MUNGU?



MUANGALIE MUNGU


Neno “muangalie Mungu” alina tofauti sana na kumwachia Mungu!

Ili neno limekuwa likitamkwa na wanadamu karibia wote, na hasa mahali ambapo jitihada zao zimefikia mwisho basi hapo utakuta mtu/watu wanasema tumwachie Mungu!
Inawezekana mtu alikuwa anamdai mwenzake/shirika  fedha nyingi tu na amesumbuka kwa kila njia pamoja na vitisho, mahakamani, busara zake na hata vikao lakini bado imekuwa sawa na kupanda mkorosho ukitegemea kuvuna mpunga.

Pia wako watu wanaweza kuwa walipendana sana na kupanga malengo mbalimbali inawezekana namna ya kuiendesha kampuni katika njia ya mafanikio zaidi lakini ghafla mtu mmoja  akaanza kwenda tofauti na lile kusudio kuu na mwingine akawa anavuta subira akitegemea kuna wakati mtu huyu atajitambua na kubadilika lakini bado anaona hana dalili ya kubadilika na mwisho anaikuta anasema na mwachia Mungu au mimi na mwangalia Mungu tu!

Nawakati mwingine katika kumwangalia Mungu imekuwa ni jambo la kawaida sana hasa pindi jambo hilo linapo pita/changamoto kupata jibu basi mtu uweza kuendelea na maisha yake! Ulegevu juu mambo ya Mungu uweza kurejea tena! Au mwingine  Mlevi katika kunywa pombe tena! Mwizi katika kuendelea katika shughuli yake! Na mengine mengi………… sawa na kile kilicho ujaza moyo na chenye nafasi katika maisha yako.

Kwa asilimia kubwa tumekuwa tukimkumbuka sana Mungu katika kipindi cha shida kanakwamba anaitwa MUNGU SHIDA! Kwa maana unapokosa msaada sehemu nyingine hivyo unakwenda kwake ambaye kwa yeye ulipata kuwako hivyo unakuwa na mtazamo wa kupata jibu la maswali yako.
Sikatai kuwa inaweza kuwa njia za Mungu katika kukufanya umjie yeye na kuanza kumwamini katika njia iliyo sahihi! Lakini inakuwa shida sana pindi unapomuona mtu akiwa na bidii katika kipindi fulani na baadae anakuwa / rudi katika maisha ya kawaida ambayo yanaondoa nafasi ya Mungu katika maisha yake.

Hapa ni na swali kidogo hivi ni kweli tunaposema tunamwachia Mungu naye anapokea na kuanza kutenda kazi kama yeye Mungu au tuna amini tu! Na tunapomwangalia Mungu kama bidamu unatakiwa ufanye yapi au ukae katika mkao upi ili na yeye Mungu afanye kama Mungu.

Kwa maana ya haraka haraka pindi unapozungumza neno hili kuwa TUMWANGALIE MUNGU kwa watu wengi wanaweza kuona kuwa wewe ni mzee wa hekima sana! Lakini ukiangalia katika upande mwingine unaweza kuona ni dharau ni kama kumpelekea mtu unaye muheshimu” kiporo” pasipo na wasiwasi ukiamini kuwa atakipokea na kukifurahia na unaamini baadae atakushukuru kwa chakula kilicho bora na cha heshima.

MUNGU ANATAKI NINI UMWACHIE NINI!

Mungu anataka MAISHA yako umwachie sio kitu kingine, anataka awe kwako zaidi ya rafiki, mfariji, jibu katika maswali yako, ulione pendo lake katika maisha yako, awe Mungu wako katika shida yako na katika uhitaji wako.

Ufunuo wa Yohana 3:20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Mungu hana maslahi na wewe kwa jambo lolote au kitu chochote kwa maana yeye anajitosheleza anakuitaji wewe uwe wake kwakua alikujua kabla ya dunia kuwapo, watu wanaweza kukutamani kwa manufaa yao lakini sio kwa Mungu anakutaka na anakupenda vile ulivyo ahitaji ujiongeze wala ujipunguze( maana anakujua vema).

Unapo amua kuishi na Mungu yeye anauhusika na shida kabla ya kuomba au kutafuta msaada wowote yeye anakuwa anaandaa jibu! Kabla ya swali ndo maana anasema yeye anaijua kesho kabla ya leo.

Ndo mana anasema….Isaya 43:26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. 

Mungu yuko kwa ajili yako ni wewe tu kuwa kwa ajili yake ili mambo yako yawe mambo yake.
Mathayo 28:20…………………… na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Anavyosema yeye ndicho anacho maanisha! Na ndicho atakacho kitenda.
BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni