Jumamosi, 21 Septemba 2013

Jumatatu, 16 Septemba 2013

MAJENZI YA MUNGU



MAJENZI YA MUNGU NDANI YA MWAMINI;

Majenzi ni mahali ambapo kunautawala wa kitu,mtu au jambo fulani husika ambae anatawala na kuendesha ufalme wake kwa uwezo wake,kwa namna yake na kwa maamuzi/mawazo yake kwa ajili ya kuimarisha utawala wake.

I wakorintho 3:16-17

Majenzi ni mahala ambapo panakuwa ni matuo, ni mahali ambapo shughuli zinafanyika kwa umakini sana.
Mahali ambapo Mungu anafurahi maana ni mahali pametengezwa nay eye na muonekano wake ni vile ambavyo ametaka iwe na si vinginevyo.

Kila mtu ana mazingira yake ambayo anavutiwa nayo na upenda kuwa namna hiyo siku zote kwa ni namna anavyopenda, ni wazi kama kuna majenzi ambayo utayaurahia ni wazi siku zote utapenda kuwapo hapo na wala hataweza kutoka hapo.

Kwa hiyo majenzi ambayo Mungu atayapenda basi yanakuwa ushawishi wa yeye kuja kukaa mahali hapo kama mazingira hayo hayapo usitegemee kama kuna mvuto ambao Mungu utamvuta na kuja na kustarehe.

Kama hakuna majenzi mazuri ya kumfanya Mungu akae na kuimarisha utawala wake kamwe hawezi kuja na kukaa kwake hata kama ukilia kwa machozi ya namna yoyote na kutoa stairi.

Kinacho mshawishi Mungu ni namna unayaandaa mazingira yake kwa ajili yake ilia akae hapo ila ukiandaa mazingira ambayo unaandaa kwa namna yako usitegemee yeye akaja na kufanya matuo ndani yako.

Ni kweli watu wengi wanamwita Mungu awaongoze awatawale awfanikishe awape ustawi lakini ana mazingira yake amabayo kwa hayo utamfanya aje kwako na kutuama milele.

Luka 11:2

Si kazi rahisi kumfanya Mungu ajenge makazi yake ndani yako kwa kuwa anapokuja na kutaka kujenga makazi yake ndani yako anavunja ustaharabu wako wote na kuleta ustaharabu wake, kwa maana nyingine atavunja yale unayo yapenda yale unayo jivunia yale ambayo unajionea fahari kwakua si kwa faida yake bali ni kwa ajili yake.

Mfano,unapokuwa mtu anayempenda anaweza akawa mzazi,mpenzi,ndugu au rafiki lazima utambue mazingira gani ambayo atapenda yawepo ili yeye afurahie kuwa na wewe kama hauna jambo hilo usitegemee mkazidi kuwa katika hali ya umoja kushikamana.

Mungu kabla ajaweka makazi yake ndani ya mwamini lazima atengeneze mazingira yake vile anavyotaka nay eye hana haraka kwakua pindi itakapo kuwa tayari ndipo atakapoamia kama bado usije ukawa una hisi kumbe yeye hayuko ndani akiendesha utawala wake.

Hakuna maana sana kusema mimi ni meokoka au kuamini kuwa nimeokoka kama tu ndani yako hakuna majenzi ya Mungu, na kumbuka kama ndani yako hakuna majenzi basi pana majenzi mengine amabayo kwa vyovyote yatapingana na majenzi ya Mungu.

Kama ilivyo uwezi kuamia mahali ambapo ujenzi ujafanyika wa ile namna ambavyo umetaka ndivyo ilivyo kwa Mungu.

Kuwa na majenzi ya Mungu ndani yako hiyo ni kitu kingine akichangamani jambo lolote ikiwa kuwa mwimbaji,kushiriki shughuli za kanisani kwa uaminifu.

Hii ni kitu kingine kabisa ambacho hataukisimuliwa haiwezi kukupa picha halisi kama ambayo utaipata ukiwa nayo mwenyewe, unakuwa zaidi ya mwana maombi, mhubiri zaidi ya chochote katika maisha yako hakina jina wala hakijawai kutokea na wala akipo ni
MUNGU ANATEMBEA KWA WEWE KUTEMBEA.

Mwanzo 1:27-29

Muonekano wako mzima utoe muonekano wa mungu hapa duniana sio jambo la kawaida wewe unakuwa zaidi ya hatari. Yaani unapotokea umependa basi ni Mungu anapenda,ukitokea umesema basi iwe ni Mungu amesema na hata ikitokea umechukia basi ni Mungu amechukia.

Hili si swala la kuchukia bali ni swala lililo wazi sana ambalo kishindo chake sio cha kitoto kwa ukitokea umetokea basi Mungu ametokea.

Unaweza ukaacha vitu vyote vina muhusu Mungu lakini si kamwe  majenzi ya Mungu ndani yake kwakua ndani ya majenzi ya Mungu kunatoka ushidi wa kishindo usioelezeka,akili ya ajabu na uhakika ulio na matumaini yasiyopungua.

Lakini watu wengi wamekuwa wakifuatilia mambo mengine wakiwa ndani ya wokovu pasipo kuutambua msingi wakovu wenyewe.

Hili ndilo hasa kusudi la Mungu kutukomboa ili makazi yake ayaweke ndani yako kwa namna alivyo maana ndani yako ndiko aliko chagua.

Kama katika ndoa kitu hasa cha msingi kuliko yote ni kuamisha makazi ya mwezi wako na kuyajenga ndani ya moyo wako. Hapo panakuwa na kudumu na kufurahia maisha yenu yote pasipo kuwa usalama wakutosha na bila shaka yoyote.

Torati 30:15-16

Japo yote yako katika maamuzi yako binafsi ukiamua kuonekana wa maana kwa mtumishi wa Mungu, kwa washirika wezako au kwa MUNGU, amua kisha onyesha kuwa nime amua.

Hauwezi kujenga makazi ya Mungu vizuri na kufurahisha moyo wa Mungu bila kumjua Mungu zaidi vile anavyotaka umjue.

Mithali 14:12



Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com



WAKATI NI WAKO UTUMIE UNAVYOTAKIWA…………..ASANTEEEEEEE!!!!!!!

Jumatatu, 9 Septemba 2013

MATUO YA MUNGU!!!!!!!!



UPENDO KAMA MATUO YA MUNGU NDANI YAKO;

  
Kama ndani yako kuna matuo ya upendo basi pana matuo ya Mungu.(Mungu ni PENDO)

Mahali popote ambapo binadamu yeyote anatamani kukaa ni mahali ambapo pana thaminiwa uwepo wake(upendo) na mahali ambapo binadamu yeyote ambayo hatapenda kukaa ni mahali ambapo ataona uwepo wake hauthaminiwi.

1 yohana 4:12,16

Maneno haya yanaonyesha kuwa Mungu ni Upendo hivyo unapotembea katika upendo basi ndani yako Mungu anafanya makao yake.

Hivyo kama upendo unakuwa ni maisha yako basi wewe unakuwa Mungu ndio maisha yako siku zote,japo natambua kuwa upendo sio kitu rahisi lakini ni kitu chenye nafasi ya pekee kwa Mungu.

Biblia kwa kiasi kikubwa imesisitiza sana kuhusu swala zima la upendo kwa kiwango kikubwa sana;
I yohana 2:29
                                              “Asiye penda hakuzaliwa na baba”
Iyohana 4:20-21
                     “utampendaje Mungu usiye muona wakati jirani yako unamchukia”

I yohana 2:9-11
        “mtu akisema anampenda Mungu na huku anamchukia jirani ni muongo wala kweli haimo ndani yake”

I wakorintho 13:1-8
               “Hata ukiongea lugha za malaika na wanadamu kama hauna upendo si kitu kwa Mungu”

Tunaona msingi ambao Mungu ameupa neno upendo kwa kiwango kikubwa sana hata kuliko sisi tunao upa, imefika kipindi mtu uweza sema anaweza kuishi pasipo pendo na akawa salama.


Kama familia moja wazazi wanapenda sana kuona katika watoto wanaishi kwa kupendana na kuheshimiana na hata kusaidiana.

I yohana 4:7-8

Na pindi unapokuwa na upendo unatembea na Mungu na pindi unapotembea nae jua ulinzi,utoshelevu wake na kujua unachofanya na kesho iliyo bora yenye kufikika.

II petro 1:3-8
Upendo ni njia moja muhimu sana katika kuonyesha wewe ni Mungu maana ni moja ya udhihirisho wa tabia ya kimungu, moja njia ambayo itaonyesha wewe ni mtoto wa fulani basi lazima kuna tabia zinazo fanana.

Shetani amewatia ujinga watu kuwa unaweza kufanya kazi ya Mungu huku ukiwa na neno na mtu. Mathalani eva akiongea na shetani kuhusu akimuonyesha kuwa unaweza ukala tunda ambalo Mungu amekukataza nabado ukawa na Mungu pasipo shaka yeyote.

Mwanzo 3:1-10
Kutoishi katika upendo basi ni kujitoa katika himaya ya Mungu na kuruhusu mambo mengine yawe na nafasi ndani yako ambayo yataleta maumivu ndani ya moyo wako.

UPENDO ni nini hasa?
                       -ni Mungu kupenda kupitia wewe.(yohana 15:10)
                       -ni hali ya kutambua thamani yako kwa Mungu ni wewe kuwathamini wengine.

Mfano. Musa alionyesha upendo wake kwa kujitoa kwa ajili ya wengine

Waebrania 11:24-25

Yesu alipojitoa kwa ajili ya wanadamu

I yohana 4:9-10,11

Yohana 15:9
“kama mimi nilivyojitoa ndivyo na ninyi na ninyi mjitoe kwa ajili ya wengine”

Yohana 14:33-34

Umaana wa ukristo wako uko katika UPENDO, kama upendo hauta tawala maisha yako jua kuwa na utawala wa Mungu itakuwa shida.

Wagalatia 5:6

Lazima utamani kuwapenda watu wote pasipo kujali kuwa mtu huyu ni nani kwako na anafanya nini kwako ni kama Mungu alivyo wapenda wote pasipo kujali huyu ni mwenye dhambi au mwenye haki.

Yohana 3:16

I Yohana 4:19-21

Utaonyesha upendo wa Mungu kwa wengine ni pale tu utakapoanza kuwapenda hao kwakua sisi ni kioo ambacho watu wana muona Mungu kupitia wewe.

Nuru ya Mungu inaonekana kwako pindi wewe utakapoanza kuwapenda wengine, jua kiasi kile utakacho wapenda wengine ndivyo hivyo Mungu ataonyesha upendo wake kwako.

I yohana 4:17



Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com


             “PENDA  PASIPO  SABABU  MAANA  HILO  NDILO  PENDO LA MUNGU”