KUFA
KWA YESU HAIMAANISHI KUWA MUNGU AMESHINDWA:
Luka 24:19-26
Utendaji wa Mungu kwa
namna nyingine avieleweki kwakua katika kila tendo huwa kuna kazi yake
anaifanya ambayo unaweza usielewe lakini itakapoanza kutumika ndipo hapo
utaanza kuona umuhimu wa kile kitu
Pindi unapokuwa katika
imaya ya Mungu usitegee kushindwa bali kuna kushinda japo zipo tafsiri mbili za
hali ya kuonyesha kuwa umeshindwa ambazo ni kibinadamu na ya kimungu,
Tafsiri ya kibinadamu ya kushindwa ni kukosa
vitu vya dunia lakini kwa Mungu tafsiri ni kuvunjika kwa uhusiano kati yake na
binadamu.
Hivi ni vitu viwili
vyenye mtazamo tofauti kutokana na hatma yake ya Mungu mwisho wake ni UZIMA na
ya kibinadamu mwisho wake ni MAUTI.
Katika mauti ya yesu
kwa namna ya kibinadamu apakuwa na matumaini yoyote kuwa hatainuka na kuwa
mshindi zaidi alivyokua awali.
Katika mauti na kukaa
yesu ndani ya kaburi inatafsiri kubwa katika maisha ya mwamini haina maana ya
ubatizo tu bali inamaana kubwa sana katika ulimwengu wa roho na wa mwili.
Ili ni tendo(yesu kukaa
kaburi) ambalo kama mkristo atakapolipita unapoinuka hauwezi kama ulivyokuwa
awali.
Na mahali utakapo
kuwepo unahitaji nguvu ya Roho mtakatifu ikutoe mahali ulipo si kitu kingine
hivyo usiruhu kitu kingine kiendelee ndani ya ufaham wako.
Japo watu wengi
hawapendi kufa lakini ni muhimu kufa ili uibuke mwingine pasipo kufa hauwezi
kufufuka tena katika hali iliyo bora kuliko awali.
-kama mbegu katika
ardhi inahitajika ionze ili kwamba iweze kuzaa matunda mengi. Na nivizuri ujue
kwamba hii hatua kama usipo ipitia usitegemee ukawa bora au wa maana sana kwani
hiyo ndiyo njia na hakuna njia nyingine ikaleta mafanikio ya kudumu.
Na sio kwamba watu
wanapenda kufa bali hii ni hatua ambayo Mungu ameiandaa mwenyewe kwa ajili ya
kutung’alisha vizuri.
Unapofika hatua
ukaogopa kufa basi jua hapo ulipo hautaweza kwenda mahali pazuri unapo fikiri
wewe binafsi.
KUFA hii ni hatua
ambayo mwili unapoteza utawala wake na roho ya Mungu ndani yako inaanza kuwa na
nguvu katika maisha yako.
Mungu hawezi kutenda
jambo ndani yako katika ukamilifu wake huku matendo ya mwili ya kawa na nguvu
ndani yako.
Pindi utakapo kubali
kufa basi hapo ndipo penye mchakato wa Mungu kutoa uhai wake na uzima kisha
kuchukua unyonge wako na kukupatia vyake.
Hii hatua ni ya muhimu
sana kwa inakuweka njia panda ujui nini kinafanyika kama mgonjwa aliye NUSU
KAPUTI ni hatua ambayo unahitaji utulivu wa kumsikiliza Roho mtakatifu ili
afanye ndani yako.
Ni kipindi ambacho
Mungu anajifunua kwako kwa namna nyingine tena ambayo unaanza kumwelewa Mungu
kwa namna tofauti kuliko ile ya awali.
Hapa penye udhihirisho
kuwa umeamua kufuata yesu pasipo maslahi yoyote ya kibinadamu kwa maana hii
umeamua kujikana kiukamilifu.
Hiyo ndiyo ishara pekee
ambayo Mungu anaitaka kuiona kutoka kwako ili umdhihirishie kuwa wewe ukotayari
kujigharimu kwa ajili yake.
Na nivizuri kutambua
kwamba maumivu ya mwili ndio furaha ya roho na maumivu ya ya roho ndio furaha
ya mwili. Unaishi kwa kufuata nini?
Usiogope kufa kwakua
kufa ni darasa la roho yako na Mungu kama hautaki kufa basi jua kwamba hautaji
darasa kati yako na Mungu.
Kufa haifurahishi
katika mwili wa kibinadamu hivyo haishawi sana kupenda kufa bali ni vizuri
kutambua kuwa kama hauto kufa kimwili basi utakufa kiroho. Lipi jema basi
chagua katika hayo usalama au mauti.
Hakuna kitu kizuri kama
kupitia kwenye mafunzo ili upate uelewa zaidi kwa ajili ya kufanya vitu katika
ubora na nguvu zaidi.
Mtu yeyote alikubali
kufa halafu akabaki vilevile jua kuwa hakumaliza kozi, kwakua mbegu haiwezi
kufa halafu ikachupa pasipo uzidisho kama hajachipuka basi wadudu wamekula hiyo
mbegu.
Usiogope kufa kwakua
kifo si kwa ajili yako bali ni kwa ajili ya mwili wako ila ni kwafaida yako
hivyo kama unatamani kufanikiwa basi tamani kufa.
Hakuna ustawi usio kuwa
na mizizi na hakuna mizizi pasipo kuwa na mbegu iliyo kufa halafu ikaoza.
Kwa maana nyingine kutamani kufa ni
kumtamani MUNGU. Hakuna maana ya kumtamani Mungu kama
utaki kufuata yale anayo yataka.
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
“Naomba nikutakie wakati
mzuri……….”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni