MAJENZI YA MUNGU NDANI YA MWAMINI;
Majenzi ni mahali ambapo kunautawala wa kitu,mtu au
jambo fulani husika ambae anatawala na kuendesha ufalme wake kwa uwezo wake,kwa
namna yake na kwa maamuzi/mawazo yake kwa ajili ya kuimarisha utawala wake.
I wakorintho 3:16-17
Majenzi ni mahala ambapo panakuwa ni matuo, ni
mahali ambapo shughuli zinafanyika kwa umakini sana.
Mahali ambapo Mungu anafurahi maana ni mahali
pametengezwa nay eye na muonekano wake ni vile ambavyo ametaka iwe na si
vinginevyo.
Kila mtu ana mazingira yake ambayo anavutiwa nayo na
upenda kuwa namna hiyo siku zote kwa ni namna anavyopenda, ni wazi kama kuna
majenzi ambayo utayaurahia ni wazi siku zote utapenda kuwapo hapo na wala
hataweza kutoka hapo.
Kwa hiyo majenzi ambayo Mungu atayapenda basi yanakuwa
ushawishi wa yeye kuja kukaa mahali hapo kama mazingira hayo hayapo usitegemee
kama kuna mvuto ambao Mungu utamvuta na kuja na kustarehe.
Kama hakuna majenzi mazuri ya kumfanya Mungu akae na
kuimarisha utawala wake kamwe hawezi kuja na kukaa kwake hata kama ukilia kwa
machozi ya namna yoyote na kutoa stairi.
Kinacho mshawishi Mungu ni namna unayaandaa
mazingira yake kwa ajili yake ilia akae hapo ila ukiandaa mazingira ambayo
unaandaa kwa namna yako usitegemee yeye akaja na kufanya matuo ndani yako.
Ni kweli watu wengi wanamwita Mungu awaongoze
awatawale awfanikishe awape ustawi lakini ana mazingira yake amabayo kwa hayo
utamfanya aje kwako na kutuama milele.
Luka 11:2
Si kazi rahisi kumfanya Mungu ajenge makazi yake
ndani yako kwa kuwa anapokuja na kutaka kujenga makazi yake ndani yako anavunja
ustaharabu wako wote na kuleta ustaharabu wake, kwa maana nyingine atavunja
yale unayo yapenda yale unayo jivunia yale ambayo unajionea fahari kwakua si
kwa faida yake bali ni kwa ajili yake.
Mfano,unapokuwa mtu anayempenda anaweza akawa
mzazi,mpenzi,ndugu au rafiki lazima utambue mazingira gani ambayo atapenda
yawepo ili yeye afurahie kuwa na wewe kama hauna jambo hilo usitegemee mkazidi
kuwa katika hali ya umoja kushikamana.
Mungu kabla ajaweka makazi yake ndani ya mwamini
lazima atengeneze mazingira yake vile anavyotaka nay eye hana haraka kwakua
pindi itakapo kuwa tayari ndipo atakapoamia kama bado usije ukawa una hisi
kumbe yeye hayuko ndani akiendesha utawala wake.
Hakuna maana sana kusema mimi ni meokoka au kuamini
kuwa nimeokoka kama tu ndani yako hakuna majenzi ya Mungu, na kumbuka kama
ndani yako hakuna majenzi basi pana majenzi mengine amabayo kwa vyovyote
yatapingana na majenzi ya Mungu.
Kama ilivyo uwezi kuamia mahali ambapo ujenzi
ujafanyika wa ile namna ambavyo umetaka ndivyo ilivyo kwa Mungu.
Kuwa na majenzi ya Mungu ndani yako hiyo ni kitu
kingine akichangamani jambo lolote ikiwa kuwa mwimbaji,kushiriki shughuli za
kanisani kwa uaminifu.
Hii ni kitu kingine kabisa ambacho hataukisimuliwa
haiwezi kukupa picha halisi kama ambayo utaipata ukiwa nayo mwenyewe, unakuwa
zaidi ya mwana maombi, mhubiri zaidi ya chochote katika maisha yako hakina jina
wala hakijawai kutokea na wala akipo ni
MUNGU ANATEMBEA KWA WEWE KUTEMBEA.
Mwanzo 1:27-29
Muonekano wako mzima utoe muonekano wa mungu hapa
duniana sio jambo la kawaida wewe unakuwa zaidi ya hatari. Yaani unapotokea
umependa basi ni Mungu anapenda,ukitokea umesema basi iwe ni Mungu amesema na
hata ikitokea umechukia basi ni Mungu amechukia.
Hili si swala la kuchukia bali ni swala lililo wazi
sana ambalo kishindo chake sio cha kitoto kwa ukitokea umetokea basi Mungu
ametokea.
Unaweza ukaacha vitu vyote vina muhusu Mungu lakini
si kamwe majenzi ya Mungu ndani yake
kwakua ndani ya majenzi ya Mungu kunatoka ushidi wa kishindo usioelezeka,akili
ya ajabu na uhakika ulio na matumaini yasiyopungua.
Lakini watu wengi wamekuwa wakifuatilia mambo
mengine wakiwa ndani ya wokovu pasipo kuutambua msingi wakovu wenyewe.
Hili ndilo hasa kusudi la Mungu kutukomboa ili
makazi yake ayaweke ndani yako kwa namna alivyo maana ndani yako ndiko aliko
chagua.
Kama katika ndoa kitu hasa cha msingi kuliko yote ni
kuamisha makazi ya mwezi wako na kuyajenga ndani ya moyo wako. Hapo panakuwa na
kudumu na kufurahia maisha yenu yote pasipo kuwa usalama wakutosha na bila
shaka yoyote.
Torati 30:15-16
Japo yote yako katika maamuzi yako binafsi ukiamua
kuonekana wa maana kwa mtumishi wa Mungu, kwa washirika wezako au kwa MUNGU,
amua kisha onyesha kuwa nime amua.
Hauwezi kujenga makazi
ya Mungu vizuri na kufurahisha moyo wa Mungu bila kumjua Mungu zaidi vile
anavyotaka umjue.
Mithali 14:12
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
WAKATI
NI WAKO UTUMIE UNAVYOTAKIWA…………..ASANTEEEEEEE!!!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni