UPENDO KAMA MATUO YA
MUNGU NDANI YAKO;
Kama ndani yako kuna matuo ya upendo basi pana matuo
ya Mungu.(Mungu ni PENDO)
Mahali popote ambapo binadamu yeyote anatamani kukaa
ni mahali ambapo pana thaminiwa uwepo wake(upendo) na mahali ambapo binadamu yeyote
ambayo hatapenda kukaa ni mahali ambapo ataona uwepo wake hauthaminiwi.
1 yohana 4:12,16
Maneno haya yanaonyesha kuwa Mungu ni Upendo hivyo
unapotembea katika upendo basi ndani yako Mungu anafanya makao yake.
Hivyo kama upendo unakuwa ni maisha yako basi wewe
unakuwa Mungu ndio maisha yako siku zote,japo natambua kuwa upendo sio kitu
rahisi lakini ni kitu chenye nafasi ya pekee kwa Mungu.
Biblia kwa kiasi kikubwa imesisitiza sana kuhusu
swala zima la upendo kwa kiwango kikubwa sana;
I yohana 2:29
“Asiye penda hakuzaliwa na
baba”
Iyohana 4:20-21
“utampendaje Mungu usiye muona wakati jirani yako unamchukia”
I yohana 2:9-11
“mtu
akisema anampenda Mungu na huku anamchukia jirani ni muongo wala kweli haimo
ndani yake”
I wakorintho 13:1-8
“Hata ukiongea lugha za malaika na wanadamu kama hauna upendo si kitu
kwa Mungu”
Tunaona msingi ambao Mungu ameupa neno upendo kwa
kiwango kikubwa sana hata kuliko sisi tunao upa, imefika kipindi mtu uweza sema
anaweza kuishi pasipo pendo na akawa salama.
Kama familia moja wazazi wanapenda sana kuona katika
watoto wanaishi kwa kupendana na kuheshimiana na hata kusaidiana.
I yohana 4:7-8
Na pindi unapokuwa na upendo unatembea na Mungu na
pindi unapotembea nae jua ulinzi,utoshelevu wake na kujua unachofanya na kesho
iliyo bora yenye kufikika.
II petro 1:3-8
Upendo ni njia moja muhimu sana katika kuonyesha
wewe ni Mungu maana ni moja ya udhihirisho wa tabia ya kimungu, moja njia
ambayo itaonyesha wewe ni mtoto wa fulani basi lazima kuna tabia zinazo fanana.
Shetani amewatia ujinga watu kuwa unaweza kufanya
kazi ya Mungu huku ukiwa na neno na mtu. Mathalani eva akiongea na shetani
kuhusu akimuonyesha kuwa unaweza ukala tunda ambalo Mungu amekukataza nabado
ukawa na Mungu pasipo shaka yeyote.
Mwanzo 3:1-10
Kutoishi katika upendo basi ni kujitoa katika himaya
ya Mungu na kuruhusu mambo mengine yawe na nafasi ndani yako ambayo yataleta
maumivu ndani ya moyo wako.
UPENDO
ni nini hasa?
-ni Mungu kupenda
kupitia wewe.(yohana 15:10)
-ni hali ya kutambua
thamani yako kwa Mungu ni wewe kuwathamini wengine.
Mfano. Musa alionyesha upendo wake kwa kujitoa kwa
ajili ya wengine
Waebrania 11:24-25
Yesu alipojitoa kwa ajili ya wanadamu
I yohana 4:9-10,11
Yohana 15:9
“kama mimi nilivyojitoa ndivyo na ninyi na ninyi
mjitoe kwa ajili ya wengine”
Yohana 14:33-34
Umaana wa ukristo wako uko katika UPENDO, kama
upendo hauta tawala maisha yako jua kuwa na utawala wa Mungu itakuwa shida.
Wagalatia 5:6
Lazima utamani kuwapenda watu wote pasipo kujali
kuwa mtu huyu ni nani kwako na anafanya nini kwako ni kama Mungu alivyo wapenda
wote pasipo kujali huyu ni mwenye dhambi au mwenye haki.
Yohana 3:16
I Yohana 4:19-21
Utaonyesha upendo wa Mungu kwa wengine ni pale tu
utakapoanza kuwapenda hao kwakua sisi ni kioo ambacho watu wana muona Mungu
kupitia wewe.
Nuru ya Mungu inaonekana kwako pindi wewe
utakapoanza kuwapenda wengine, jua kiasi kile utakacho wapenda wengine ndivyo
hivyo Mungu ataonyesha upendo wake kwako.
I yohana 4:17
Prepared by ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
Katiti, James - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com
“PENDA PASIPO SABABU MAANA HILO NDILO PENDO LA MUNGU”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni