Jumanne, 24 Novemba 2015

NILIFIKIRI YAMEISHA, KUMBE SAFARI BADO?



NILIFIKIRI YAMEISHA, KUMBE SAFARI BADO IPO?





Umekuwa ni msemo wa kawaida kuwa baada ya dhiki ni faraja! Au mchumia juani ulia kivulini na nyingine nyingi zikiwapa matuamini watu kuwa baada hali ngumu kuna hali njema itatokea na pindi hali njema inaposhindwa kutokea apo ndipo uweza kuzaliwa methali nyingine kama  ng’ombe wa masikini azai wakiwa na maana kuwa kama hauna bahati ya kufanikiwa kamwe hauwezi kufanikiwa………….Kufikiri kunaweza kukupa jibu linaloweza kukufurahisha moyo wako au kufanya moyo wako kuwa chini lakini wakati wote haiwezi kutoa picha iliyokamili mpaka pale itakapo dhihirika na ndipo hapo unaweza kujitia matuamaini au kujilaumu.

Katika kuamini kuwa sasa nimeshafika mwisho kinachofuata ni kipindi cha neema……….hii ni kauli ambayo watu wengi wanaipenda na wanahali ya kuamini kuwa pindi nitakapofanya hili basi nitakuwa katika hali njema zaidi lakini wakati mwingine inapokuwa tofauti ndipo hapo mawazo mengine yanaweza kuzaliwa hapo na hasa hali ya kukata tama uweza kuzaliwa hapo.

Hali hii inaweza kutokea katika mazingira tofauti;

i.Mausiano
swala la mausiano katika dunia ya sasa imekuwa ni jambo la kawaida sana na hata kupoteza ile hadhi yake lakini kubwa zaidi jambo hili limekuwa likileta maafa makubwa katika jamii tunayoishi au inayotuzungaka na pengine  hata kusababisha ugomvi mkubwa usioisha.

Inaweza kuwa katika maisha yako ulipitia mikasa mingi inayohusiana na kimapenzi hasa katika hali ya kutendwa, na kuacha mahali ambapo wewe ulipenda sana……..inaweza kuna wakati uliamua kukaa pekee yako kwa muda na kuwa na msimamo mgumu kutokana na yale uliyotendewa lakini mwisho ukuweza kuimiri hali yako katika msimamo ulionao na ukajishauri na ukaamini kuwa watu wanaweza kutofanana hivyo huyu anaweza kuwa ni mtu mwema basi ukafungua milango ya hisia zako na kufungua moyo wako na kisha ukampa nafasi ya kipekee katika maisha yako ukiamini kuwa huyu awezi kuwa kama wale,

lakini maadamu siku zinaenda na majira yanazidi kuzunguka  ukaanza kuhisi kuwa hewa safi imeanza kuingia hewa isiyotakiwa ambayo imeleta uzito na hatimae kuondoa furaha ya kuishi katika dunia ya wapendanao.

Na mwisho ukajikuta baada ya safari kuchanua sasa inaanza kufubaa na kuwa nzito na hivyo kupelekea pumzi kushindwa kutoka vizuri katika hali stahiki na pindi ukaanza kuona nuru ya upendo ikaanza kufifia na kuhisi muda si mrefu hiyo nuru itazimika, na kupoteza matuamani uliokuwa nayo hapo baadae.

Kweli kipindi hiki akina mzoefu kwani katika kipindi hiki ili uweze kukimudu akihusishi sana akili tu bali kina husika sana swala zima la hisia na mfumo kamili wa mwili kwakua swala hili pindi linapoathiri hisia linabadilisha mfumo wa kuishi katika maisha yako ya kila siku.

Na hapo fikra zako zinapokosa jibu muafaka na pindi hapo unaweza ukaishi maisha ambayo ukuwai kufikiria wala ukuwai kutarajia na katika hali utakayoishi kutokana na hali iliyotia giza  akili na usione mwanga wa matuamini tena!

ii.Elimu
ili ni jambo ambalo watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba kupitia hili watu wengi wanaweza kutoka chini sana na hata kufikia sehemu ya juu sana, lakini sikatai kuwa wako watu ambao wameweza kutoka mahali pa chini na kwenda juu sana.

Lakini katika hali ya kushangaza sana wako watu walipata elimu ambayo kijamii wanaamini kuwa mtu huyu sio mwezetu kutokana na elimu aliyoipata lakini mwisho imekuwa ni tofauti na hali halisi inavyozaniwa.

Mfano ulikuwa wa kweli….Katika nchi Fulani hapa ulimwenguni kuna kijana alitoka katika familia masikini sana na alijitaidi sana kujisomesha hadi alifika katika ngazi ya juu ya elimu (chuo kikuu) lakini pindi alipomaliza elimu yake alikuwa na furaha sana akiwa anaamini kabisa kuwa sasa atapata ahueni ya maisha lakini pindi alipoingia katika jamii baada ya kumaliza masomo yake, alijaribu kutafuta kazi kila kona akuona matunda yake alijipa moyo lakini mwisho hakuona maana ya yeye kusoma katika hatua ya shahada, baadae akaamua kuwa mjasiriamali wa kuuza matunda aina ya machungwa kwa kutembeza mtaani na pamoja na hilo kuna siku maaskari walimvamia na kumpora matunda yake na hatimae kuharibu mtaji wake na hatimae kijana baada ya kukaa na kujiuliza sana akaamua atoke hadharani mbele ya watu wengi na kujimwagia mafuta ya petrol na kujiwashia moto na hatimae kujilipua na hapo ukawa mwisho wa historia yake ya kuwepo duniani.
Siko kinyume na kusoma kwani hata mimi napenda kusoma sana lakini tambua kuna wakati elimu inaweza isikupe nuru ile unayoitarajia inaweza kukupa maarifa lakini isikupe namna ya kuyatumia katika mazingira unayoyazunguka au kukosa fursa ya kutumia kile ulichonacho katika ufahamu wako.

iii.huduma
kwakua hapa ndipo kunabeba sababu ya wewe kuumbwa na ndio dhamira kuu kwako katika kuhakikisha unatoa kile ambacho Mungu amekiweka ndani yako.kuna wakati unaweza kuona sasa ni wakati wangu wa huduma yangu kuanza kutambulika au kuanza kazi lakini ukiangalia vizuri unaona inazidi kufichwa zaidi baada ya kuachiwa kufanya kazi katika uhuru zaidi ili ni jambo ambalo watu wengi wanalia sana kutokana na kukosa mazingira ya kuruhusu huduma yake kufanya kazi katika hali stahiki, katika huduma ilikutenda kazi kuna mazingira yaliyoandaliwa na kuandaa mazingira mwenyewe katika kufanikisha ile huduma.

Natambua yako maumivu makubwa sana pindi mtu anapoona kuwa hakuna utendaji wa huduma iliyo ndani yake, lakini yote juu ya yote kama huduma imewekwa na Mungu hauna budi kupata shida kwa wakati wake itachomoza na kung’ara tu.

Usitumie muda mwingi kujiandalia nafasi au kuchochea kitu ndani yako kwa kutumia akili yako jua yeye aliyeweka ndani yako anaouwezo wa kuhakikisha hali hiyo inakuwa na nafasi ya utendaji kwakua yeye ndiye amekiweka ndani na atahakikisha kinafanya kazi tu.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 17 Novemba 2015

MUUNGAMANIKO WA MAANA

UNGAMANIKO NA MUNGU;



Kuna kuungamanishwa na kujiungamanisha!!!

Katika dunia ya sasa muunganiko(connection or network) wanaseama kuwa ni mafanikio na wako watu upenda kuwa na marafiki mbalimbali mathalani wanasheria, daktari, waasibu na hata wenyefani zingine ili siku wakipata shida waweze kusaidiwa kirahisi……..lakini pamoja na hayo inaweza isiwe vile walivyofikiria.

Zaburi 52:7  “kumbe! Huyu ndiye mtu Yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake aliutumaini wingi wa mali zake na kujifanya hodari kwa madhara yake”

Unaweza kuungamanika na mtu kwa namna yeyote vile alivyo,hata kama ni imara kiasi gani lakini anaweza asikufae katika kila kona lakini MUUNGAMANIKO NA MUNGU huu umebeba utoshelevu wako wote na unakidhi mahaitaji yako kila kona.

Hakuna muungamaniko unaweza kukufikisha kwenye hatima yako mbali na muunganiko huu muungaminiko wowote hauna mwanga katika maisha yako lakini muungamaniko wa Mungu sio tu kukupa mwanga bali na uwezesho wa kukufikisha pale unapotakiwa kuwepo.

Na ushuhuda mwingi sana kwa watu walioungamanika na watu wengi na mwisho ukasababisha majeraha katika mioyo yao lakini sijawai kusikia kamwe mtu aliye ungaminika na mbingu na mwisho akawa na majuto kwa Mungu kwakua ndani ya Mungu hakuna ubinafsi wenye kumuumiza mwingine bali furaha yake ndio nguvu yako.

Nikubaliane tu kuwa kuna miungaminiko mingi mizuri ya kuvutia ya kiabiashara, urafiki na uchumba lakini kamwe sio kama UNGAMANIKO NA MBINGU, laiti ungetambua ubora na uzuri na upekee wake unaweza usitamani muunganiko mwingine.Umeungamika kiasi gani? Au unamwingiliano kiasi gani kwa mtu bila shaka ndio utaamua utendaji wako na bidii yako kwa ujumla wake,Utendaji wa mtu wakati mwingi utegemea sana muungamaniko wake na wengine watu baki, wafanyakazi wenzake na hata bosi wake.

Moja ya kitu kinachowapa watu matumaini makubwa na ujasiri mkubwa ni kutambua kuwa anausiana na mtu ambaye yeye ana nafasi ambayo anaona kuwa yeye itampa nafasi iliyobora zaidi kuliko wengine.

Ukitaka kupotea kirahisi tu basi wewe  muamini binadamu hautachelewa sana kupotea kwakua ndani yake japo atafikiria yako ila jua pia kuna sehemu kubwa kuna yake ambayo ameyapa uzito mkubwa sana kwakua anajua asipoyafanya inakuwa ni aibu yake!

Ungamaniko la kweli la uhakika ambalo linaweza kuleta miungamaniko iliyo salama yenye tija na manufaa katika maisha yako ni UNGAMANIKO NA MUNGU.

Hatua za kuungamanika na muungamaniko na Mungu!

i.kuokoka
niseme hakuna mtua anaweza kumfuata Mungu kwa njia ya kawaida nae akamuona Mungu kama pasipo kupitia njia ya kristo yesu.
Yohana 14:6
Asikudanganye mtu kuwa na mfuata Mungu kwakua na heshimu taratibu zilizowekwa hapa duniani hapana unapoheshimu taratibu za duniani ndipo unaweza kupata neema na kibali cha kuishi vizuri duniani lakini pindi utakapo heshimu taratibu za mbingu( kuokoka) ndipo utakapo pata kibali cha wewe kuishi hapa duniani ukiwa na kibali kwa Mungu.

ii.Aishi yeye kupitia wewe
usiishi maisha kujikopesha kwa Mungu mara unampa nafasi Mungu na baadae unajimirikisha mwenyewe!

ni rahisi tu kwakua ni yeye anaamua kuishi kupitia wewe na kuanza kukufikisha katika lile ulilokusudia yeye ambalo kwahilo yeye amekuumba.

Hauwezi kufikia katika hatima yako kama unaishi wewe tu kwakua vipo vikwazo na mitihani mingi ambayo kiukweli vinamwitaji yeye kwa asilimia zote ili uweze kushinda kirahisi pasipo kutumia muda mwingi ilikutoka hapo kwakua yupo mwenye akili zisizo zuilika.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson…………………………………….0764 018535

Jumanne, 10 Novemba 2015

NAFASI YAKO



NAFASI YAKO;


 Mivutano mingi katika dunia/katika jamii yetu ya sasa tuliyonayo kwa asilimia kubwa ni matokeo baada ya kuona mtu nafasi yake imechukuliwa au inataka kuchukuliwa na mwingine!

Japo watu wengi wana amini kuwa kuchukuliwa nafasi yake na mtu mwingine basi hapo ni ishara ya kuchukuliwa heshima yake hivyo anaona kitakachofuata hapo ni kuzalauliwa.

Katika upande wa nchi mathalani mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala uliopo katika nchi au usaliti wa kikindi dhidi ya taifa au kundi lingine ni kutaka kuchukua nafasi ya mtu au kundi la watu lililoshikilia, naweza kusema moja ya pigo kubwa ambalo watu wanapolipata mioyo yao inakuwa katika mazingira magumu sana ni kuchukuliwa nafasi yake!

Kuna mbadilishano wa nafasi katika mazingira ya nje na mazingira ya ndani!
Mabadiliko ya nafasi katika mazingira ya nje mathalani ofisini katika mabadilishano wa nafasi za kazi zinaweza kuwa kutokana na sifa kuzidiana au hujumu tu wa mtu husika katika mgongano wa kimasilai vilevile kunambadilishano wa mazingira ya ndani hususa katika moyo wa mtu inawezekana marafiki tu wa jinsia moja au tofauti, mchumba na hata wanandoa panakuwa na maumivu makali sana pindi mtu anapogundua nafasi yake katika moyo wa mtu aliyempenda kuwa haipo tena.

Na inawezekana mbadilishano ukaanza wa ndani na baadae ukadhihirika kwa nje! yaani baada ya moyo kugoma na mwili ukaitikia au ukatoa ushirikiano.

Na nafasi inaweza ikatengenezwa na mtu, mungu au yenyewe ikajitokeza pasipo usaidizi wa vitu hivi viwili(mtu au Mungu). Ni wazi kunakujiamini sana na kujivunia sana pindi unapotambua katika moyo wa mtu au sehemu fulani unayo nafasi na hiyo nafasi inapewa thamani yake.

Napenda kusema kuwa watu wengi wamekuwa huru sana na wakati mwingine hata kujisahau pindi wanapotambua kuwa wana nafasi sehemu fulani mathalani ndugu yako ana nafasi nzuri serikalini au katika idara fulani basi panaweza kutokea na hali ya kujiachia na hatimae kuondoa ufanisi wote katika jukumu ulilopewa.

Niseme nafasi yoyote ili mradi imeitwa nafasi yako basi itakuwa yako siku zote kwakua yeye anayetoa nafasi ataishikilia pasipo kutokea mtu mwenye uwezo wa mwingine katika kuhakikisha kuondoa nafasi yako ni kweli wakati mwingine katika macho unaweza kuona sehemu fulani hauna nafasi lakini pindi utakapo angali kwa jicho la tatu basi unaweza kuona nafasi yako kuwa ni kubwa kuliko unavyofikiria.

Nafasi yako huwa haibadilishwi na mtu unaweza kuona kwa macho yako imebadilishwa na mtu lakini ukweli kwamba katika macho ya Mungu bado ipo palepale alipoweka yeye na sio palipo na jicho la wanadamu,

Ni kweli kumetokea matendo mabaya pindi mtu anapogundua nafasi yake imebadilishwa hama haipo tena watu uweza kuuana,chuki zilizojikita ndani ya mizizi ya mwanadamu, maamuzi magumu yasiyokuwa na sababu yaliyobeba hatima mbaya katika maisha ya mtu husika na hata kwa jamii husika na wanaomtegemea.

Kisilani kikubwa uwa kinaibuka pale tu unapotambua nafasi yako haipo tena mahali ambapo palichangia ustawi wako mathalani kazini labda ulikuwa mkurugenzi lakini ghafla ukatolewa hapo na kujikuta kibarua akipo tena na unajua kuwa kupitia hapo ulikuwa unaendesha maisha yako na familia yako inakuwa katika hali nzuri,na wakati mwingine mathalani mchumba wako anaweza alikuwa anawezesha maisha yako katika kukupatia feha ilikujikimu katika maisha yako lakini unapoona nafasi yako haipo tena utakumbuka mbali sana kama ulikuwa sehemu nzuri sana sasa unarudi sehemu mbaya tofauti na matarajio yako.

Niseme sio njia sahihi kuwa na kinyongo na mtu na kutaka kulipa kisasi kwa yale aliyokutendea bali kubwa hapo ni kurudi kwa yeye mtoa nafasi na ndiye atakuweka katika nafasi hiyo au kukupandisha katika nafasi iliyoko juu zaidi sana kuliko ulivyofikiria.

*Acha ugomvi usio na maendeleo na vita ya kugombania nafasi na hatimae kufananishwa na watoto wanaogombana kisa mwenzake kachukua nyama yake na uweza kususa hata kula pasipo kujua kuwa nyama peke yake haishibishi na zaidi sana yuko ambaye aliyenunua nyama anaweza kukupa kubwa kuliko hiyo lakini watoto huishia kuchukiana na kusema huyu sili naye tena, japo watoto ugomvi wao ahudumu muda wote tofauti na watu wazima.

Niseme kwamba nafasi yoyote utakayokuwepo lazima uitambue kuwa ni Mungu amekupa na yeye ndiye anahusika na maisha yako hivyo kuzidi kumuheshimu yeye na kufuata njia zake ni kitu muhimu sana na vilevile usifikiri kuwa sasa hapo ndio umeshafika bado unasafari ndefu sana.

Lazima ujue kuwa ustawi wa maisha yako umebebwa na Mungu na sio kitu kingine hivyo tumia muda mwingi katika kuhakikisha unaheshimu chanzo sahihi cha nafasi yako.

Imeandaliwa na;

Cothey  Nelson…………………………………………………………0764 018535

ONDOA HOFU NAFASI YAKO INALINDWA NA MUNGU!!!

Jumanne, 3 Novemba 2015

NYUFA



NYUFA


 Nyufa  ni dalili ya muachano wa kitu kilichoshikamana au hali ya utofauti wa awali na sasa iliyojitokeza katika kitu fulani wenye mwelekeo katika  uharibifu mkubwa!!!

Usitegemee kudumu na kitu kama hakuna marekebisho au kukikagua mara kwa mara kuhakikisha ubora wake kuwa haupungui na kutibu kasoro zake ili kukifanya kuwa imara na bora siku zote, na hii ndio ishara ya kupenda kifaa chako au mtu kutathmini mwendo wenu na kurekebisha tofauti zenu,

Nyufa ni dalili mbaya inayojitokeza wakati wa huzuni au furaha na inawezekana kutokea kwa mtu usiyemtegemea au uliyemtegemea kwa huyu wakati wowote jambo lolote halinaweza kutokea.
Wakati mwingine na fananisha nyufa kama ugonjwa ambao unaweza kusababisha uharibifu kwa mtu kama tu usipochukua tahadhari ya mapema katika matibabu yake, kwani kadili unavyoacha ugonjwa katika mwili ndivyo unaweza kusababisha maumivu au uaribifu mkubwa katika mwili.

Kama unataka kuwa makini au uimara wa kitu basi kuwa makini na kila nyufa zinazotokea pasipo kusubiria hali kuwa mbaya zaidi na kutumia gharama kubwa zaidi katika kutatua hilo tatizo au jambo hilo, hivyo niseme tu kama hutakuwa makini na mwanzo wa nyufa basi usishangai ukuta kuporomoka!

Ni kawaida tu kuwa uwezi kwenda mbali kama unatumia kifaa ambacho kinakasoro nyingi au upungufu mwingi na ndomana watu wanasema kifaa kisicho na ubora uitwa KIMEO. Niseme hata kama umeniwia kiasi gani kama kuna nyufa fahamu tu kwamba kufika huko ni vigumu sana!

Ni mpasuko ulioanza kwa namna ya kuweza kuzuilika lakini unaweza kuwa ni hatari zaidi usipo kuwa makini katika kufanya malekebisho mapema, kikawaida hakuna ukuta wowote unaweza kubomoka bila kuanza kutoa ufa kwanza labda katika sababu zingine kama vile matetemeko ya ardhi, mafuriko, kubomorewa na sababu zingine.

Ni ukweli usiopingika kuwa nyufa zinapotokea zinaonekana lakini kutokana na sababu za kuaghirisha na kupuuzia basi katika mazingira hayo uweza kupelekea ufa kuongezeka na kupelekea gharama kuongezeka katika ukarabati na wakati mwingine maafa yakatokea.

Kama kweli unataka ukae katika nyumba imara na kwa muda mrefu basi hakikisha unakuwa makini na mambo madogo madogo au kasoro ndogondogo ili uweze kuendelea kudumu katika jambo hilo au katika nyumba hiyo…………niseme mmomonyoko wa vitu vingi unatokana na kutokuwa makini na kasoro ndogondogo au kupuuzia.

Katika kudumisha mausiano yoyote lazima uwe makini na kila dalili mbaya  inayoweza kujitokeza ili uweze kurekebisha kabla hayajakuwa kubwa zaidi na ukashindwa kumudu………nimeshuhudia mmomonyoko wa vitu vingi unatokana na kupuuziana  na hatimae ukatokea  na mmomonyoko mkubwa katika maisha yao.

Usipokuwa makini katika nyufa ndogo basi hauwezi kuwa makini katika nyufa kubwa kwakua ulianza kutokua makini katika mwanzo unaoonekana kuwa unaweza kutibika na hatimae ukatokea katika hali iliyo ngumu zaidi, unapotaka kuwa katika mwendelezo uliona maana sana basi unahitajika sana kuwa makini katika kila utofauti na hilo jambo linahitaji kutatulika sio kulivumilia.

Siku zote unaweza ukaona ni jambo dogo kwako na usione kuwa kama ni kitu kikubwa  kwa mwenzako lakini usipokuwa makini basi lolote linaweza kutokea, nyufa sio kitu kibaya kwa anayetaka mmomonyoko na ni kitu kibaya kwa asiyetaka  mmomonyoko na hali hii isiwe ndani yako tu bali uchukulie hatua kuhakikisha kuwa ufa huo unapata suruhu ya kudumu.

Ni kweli kila jambo linakusudi lake!!! Lakini niseme tu wazi sio kila jambo linakuwa na mwanzo unaofanana linakuwa na hitimisho linalofanana, upo utofauti mkubwa lazima ujue unachofanya na unachofanyiwa kinabeba hitimisho gani! Kubwa katika maisha yako lazima ubebe dhamira iliyosafi isiyobeba kisasi bali iliyobeba dhamira njema na ustawi wako katika maisha yako.

Niseme nyufa sio kitu kizuri katika kundi, jumuhiya, ndoa na ushirika wowote kama unataka msiende mbele zaidi basi msichukulie hatua yoyote ya kusawazisha au kurekebisha kitakachotokea hapo ni kupoteza muda na kulimana badala ya kujengana………..niseme kuwa bora haondolewe yule anayesababisha nyufa zitokee kuliko kuendelea kukaa na hatimae kusababisha maumivu zaidi au uharibifu zaidi.

Kinachouma sana kwa watu wengi ni kuona nyufa zinazotokea kwa mtu uliyempenda na urifikiri atakuwa wa maana zaidi katika maisha lakini amekuwa sababu ya kwanza katika kusababisha mmomonyoko utakao sababisha maafa makubwa.

Mkikubali kuishi katika utofauti basi kitakachoendelea hapo ni kuishi katika kutokuwa halisi hama kwa lugha rahisi ni maisha ya unafiki ambayo mwisho wa siku kunakuwa hakuna ushirikiano wowote ( vita baridi).


Imeandaliwa na;

Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535

HAKUNA KITU KIGUMU KAMA KUTUNZA MAUSIANO!!!