NYUFA
Nyufa ni dalili ya muachano wa kitu
kilichoshikamana au hali ya utofauti wa awali na sasa iliyojitokeza katika kitu
fulani wenye mwelekeo katika uharibifu
mkubwa!!!
Usitegemee kudumu na
kitu kama hakuna marekebisho au kukikagua mara kwa mara kuhakikisha ubora wake
kuwa haupungui na kutibu kasoro zake ili kukifanya kuwa imara na bora siku
zote, na hii ndio ishara ya kupenda kifaa chako au mtu kutathmini mwendo wenu
na kurekebisha tofauti zenu,
Nyufa ni dalili mbaya
inayojitokeza wakati wa huzuni au furaha na inawezekana kutokea kwa mtu usiyemtegemea
au uliyemtegemea kwa huyu wakati wowote jambo lolote halinaweza kutokea.
Wakati mwingine na
fananisha nyufa kama ugonjwa ambao unaweza kusababisha uharibifu kwa mtu kama
tu usipochukua tahadhari ya mapema katika matibabu yake, kwani kadili
unavyoacha ugonjwa katika mwili ndivyo unaweza kusababisha maumivu au uaribifu
mkubwa katika mwili.
Kama unataka kuwa
makini au uimara wa kitu basi kuwa makini na kila nyufa zinazotokea pasipo
kusubiria hali kuwa mbaya zaidi na kutumia gharama kubwa zaidi katika kutatua
hilo tatizo au jambo hilo, hivyo niseme tu kama hutakuwa makini na mwanzo wa
nyufa basi usishangai ukuta kuporomoka!
Ni kawaida tu kuwa
uwezi kwenda mbali kama unatumia kifaa ambacho kinakasoro nyingi au upungufu
mwingi na ndomana watu wanasema kifaa kisicho na ubora uitwa KIMEO. Niseme hata
kama umeniwia kiasi gani kama kuna nyufa fahamu tu kwamba kufika huko ni vigumu
sana!
Ni mpasuko ulioanza kwa
namna ya kuweza kuzuilika lakini unaweza kuwa ni hatari zaidi usipo kuwa makini
katika kufanya malekebisho mapema, kikawaida hakuna ukuta wowote unaweza
kubomoka bila kuanza kutoa ufa kwanza labda katika sababu zingine kama vile
matetemeko ya ardhi, mafuriko, kubomorewa na sababu zingine.
Ni ukweli usiopingika
kuwa nyufa zinapotokea zinaonekana lakini kutokana na sababu za kuaghirisha na
kupuuzia basi katika mazingira hayo uweza kupelekea ufa kuongezeka na kupelekea
gharama kuongezeka katika ukarabati na wakati mwingine maafa yakatokea.
Kama kweli unataka ukae
katika nyumba imara na kwa muda mrefu basi hakikisha unakuwa makini na mambo
madogo madogo au kasoro ndogondogo ili uweze kuendelea kudumu katika jambo hilo
au katika nyumba hiyo…………niseme mmomonyoko wa vitu vingi unatokana na kutokuwa
makini na kasoro ndogondogo au kupuuzia.
Katika kudumisha
mausiano yoyote lazima uwe makini na kila dalili mbaya inayoweza kujitokeza ili uweze kurekebisha
kabla hayajakuwa kubwa zaidi na ukashindwa kumudu………nimeshuhudia mmomonyoko wa
vitu vingi unatokana na kupuuziana na
hatimae ukatokea na mmomonyoko mkubwa
katika maisha yao.
Usipokuwa makini katika
nyufa ndogo basi hauwezi kuwa makini katika nyufa kubwa kwakua ulianza kutokua
makini katika mwanzo unaoonekana kuwa unaweza kutibika na hatimae ukatokea
katika hali iliyo ngumu zaidi, unapotaka kuwa katika mwendelezo uliona maana
sana basi unahitajika sana kuwa makini katika kila utofauti na hilo jambo
linahitaji kutatulika sio kulivumilia.
Siku zote unaweza
ukaona ni jambo dogo kwako na usione kuwa kama ni kitu kikubwa kwa mwenzako lakini usipokuwa makini basi
lolote linaweza kutokea, nyufa sio kitu kibaya kwa anayetaka mmomonyoko na ni
kitu kibaya kwa asiyetaka mmomonyoko na
hali hii isiwe ndani yako tu bali uchukulie hatua kuhakikisha kuwa ufa huo
unapata suruhu ya kudumu.
Ni kweli kila jambo
linakusudi lake!!! Lakini niseme tu wazi sio kila jambo linakuwa na mwanzo
unaofanana linakuwa na hitimisho linalofanana, upo utofauti mkubwa lazima ujue
unachofanya na unachofanyiwa kinabeba hitimisho gani! Kubwa katika maisha yako
lazima ubebe dhamira iliyosafi isiyobeba kisasi bali iliyobeba dhamira njema na
ustawi wako katika maisha yako.
Niseme nyufa sio kitu
kizuri katika kundi, jumuhiya, ndoa na ushirika wowote kama unataka msiende
mbele zaidi basi msichukulie hatua yoyote ya kusawazisha au kurekebisha
kitakachotokea hapo ni kupoteza muda na kulimana badala ya kujengana………..niseme
kuwa bora haondolewe yule anayesababisha nyufa zitokee kuliko kuendelea kukaa
na hatimae kusababisha maumivu zaidi au uharibifu zaidi.
Kinachouma sana kwa
watu wengi ni kuona nyufa zinazotokea kwa mtu uliyempenda na urifikiri atakuwa
wa maana zaidi katika maisha lakini amekuwa sababu ya kwanza katika kusababisha
mmomonyoko utakao sababisha maafa makubwa.
Mkikubali kuishi katika
utofauti basi kitakachoendelea hapo ni kuishi katika kutokuwa halisi hama kwa
lugha rahisi ni maisha ya unafiki ambayo mwisho wa siku kunakuwa hakuna
ushirikiano wowote ( vita baridi).
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson…………………………………………..0764
018535
HAKUNA KITU KIGUMU KAMA KUTUNZA
MAUSIANO!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni