UNGAMANIKO
NA MUNGU;
Kuna kuungamanishwa na
kujiungamanisha!!!
Katika dunia ya sasa
muunganiko(connection or network) wanaseama kuwa ni mafanikio na wako watu
upenda kuwa na marafiki mbalimbali mathalani wanasheria, daktari, waasibu na
hata wenyefani zingine ili siku wakipata shida waweze kusaidiwa
kirahisi……..lakini pamoja na hayo inaweza isiwe vile walivyofikiria.
Zaburi
52:7 “kumbe! Huyu ndiye mtu Yule,
Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake aliutumaini wingi wa mali zake na kujifanya
hodari kwa madhara yake”
Unaweza kuungamanika na
mtu kwa namna yeyote vile alivyo,hata kama ni imara kiasi gani lakini anaweza
asikufae katika kila kona lakini MUUNGAMANIKO NA MUNGU huu umebeba utoshelevu
wako wote na unakidhi mahaitaji yako kila kona.
Hakuna muungamaniko unaweza
kukufikisha kwenye hatima yako mbali na muunganiko huu muungaminiko wowote hauna
mwanga katika maisha yako lakini muungamaniko wa Mungu sio tu kukupa mwanga
bali na uwezesho wa kukufikisha pale unapotakiwa kuwepo.
Na ushuhuda mwingi sana
kwa watu walioungamanika na watu wengi na mwisho ukasababisha majeraha katika
mioyo yao lakini sijawai kusikia kamwe mtu aliye ungaminika na mbingu na mwisho
akawa na majuto kwa Mungu kwakua ndani ya Mungu hakuna ubinafsi wenye kumuumiza
mwingine bali furaha yake ndio nguvu yako.
Nikubaliane tu kuwa kuna
miungaminiko mingi mizuri ya kuvutia ya kiabiashara, urafiki na uchumba lakini
kamwe sio kama UNGAMANIKO NA MBINGU, laiti ungetambua ubora na uzuri na upekee
wake unaweza usitamani muunganiko mwingine.Umeungamika kiasi gani? Au
unamwingiliano kiasi gani kwa mtu bila shaka ndio utaamua utendaji wako na
bidii yako kwa ujumla wake,Utendaji wa mtu wakati mwingi utegemea sana
muungamaniko wake na wengine watu baki, wafanyakazi wenzake na hata bosi wake.
Moja ya kitu kinachowapa
watu matumaini makubwa na ujasiri mkubwa ni kutambua kuwa anausiana na mtu
ambaye yeye ana nafasi ambayo anaona kuwa yeye itampa nafasi iliyobora zaidi
kuliko wengine.
Ukitaka kupotea
kirahisi tu basi wewe muamini binadamu
hautachelewa sana kupotea kwakua ndani yake japo atafikiria yako ila jua pia
kuna sehemu kubwa kuna yake ambayo ameyapa uzito mkubwa sana kwakua anajua
asipoyafanya inakuwa ni aibu yake!
Ungamaniko la kweli la
uhakika ambalo linaweza kuleta miungamaniko iliyo salama yenye tija na manufaa
katika maisha yako ni UNGAMANIKO NA MUNGU.
Hatua
za kuungamanika na muungamaniko na Mungu!
i.kuokoka
niseme hakuna mtua
anaweza kumfuata Mungu kwa njia ya kawaida nae akamuona Mungu kama pasipo
kupitia njia ya kristo yesu.
Yohana 14:6
Asikudanganye mtu kuwa
na mfuata Mungu kwakua na heshimu taratibu zilizowekwa hapa duniani hapana
unapoheshimu taratibu za duniani ndipo unaweza kupata neema na kibali cha
kuishi vizuri duniani lakini pindi utakapo heshimu taratibu za mbingu( kuokoka)
ndipo utakapo pata kibali cha wewe kuishi hapa duniani ukiwa na kibali kwa
Mungu.
ii.Aishi
yeye kupitia wewe
usiishi maisha
kujikopesha kwa Mungu mara unampa nafasi Mungu na baadae unajimirikisha
mwenyewe!
ni rahisi tu kwakua ni
yeye anaamua kuishi kupitia wewe na kuanza kukufikisha katika lile ulilokusudia
yeye ambalo kwahilo yeye amekuumba.
Hauwezi kufikia katika
hatima yako kama unaishi wewe tu kwakua vipo vikwazo na mitihani mingi ambayo
kiukweli vinamwitaji yeye kwa asilimia zote ili uweze kushinda kirahisi pasipo kutumia
muda mwingi ilikutoka hapo kwakua yupo mwenye akili zisizo zuilika.
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson…………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni