NAFASI YAKO;
Mivutano mingi katika
dunia/katika jamii yetu ya sasa tuliyonayo kwa asilimia kubwa ni matokeo baada
ya kuona mtu nafasi yake imechukuliwa au inataka kuchukuliwa na mwingine!
Japo watu wengi wana
amini kuwa kuchukuliwa nafasi yake na mtu mwingine basi hapo ni ishara ya
kuchukuliwa heshima yake hivyo anaona kitakachofuata hapo ni kuzalauliwa.
Katika upande wa nchi mathalani
mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala uliopo katika nchi au usaliti wa kikindi
dhidi ya taifa au kundi lingine ni kutaka kuchukua nafasi ya mtu au kundi la
watu lililoshikilia, naweza kusema moja ya pigo kubwa ambalo watu wanapolipata
mioyo yao inakuwa katika mazingira magumu sana ni kuchukuliwa nafasi yake!
Kuna
mbadilishano wa nafasi katika mazingira ya nje na mazingira ya ndani!
Mabadiliko ya nafasi
katika mazingira ya nje mathalani
ofisini katika mabadilishano wa nafasi za kazi zinaweza kuwa kutokana na sifa
kuzidiana au hujumu tu wa mtu husika katika mgongano wa kimasilai vilevile
kunambadilishano wa mazingira ya ndani
hususa katika moyo wa mtu inawezekana marafiki tu wa jinsia moja au tofauti,
mchumba na hata wanandoa panakuwa na maumivu makali sana pindi mtu anapogundua nafasi
yake katika moyo wa mtu aliyempenda kuwa haipo tena.
Na inawezekana
mbadilishano ukaanza wa ndani na baadae ukadhihirika kwa nje! yaani baada ya
moyo kugoma na mwili ukaitikia au ukatoa ushirikiano.
Na nafasi inaweza
ikatengenezwa na mtu, mungu au yenyewe ikajitokeza pasipo usaidizi wa vitu hivi
viwili(mtu au Mungu). Ni wazi kunakujiamini sana na kujivunia sana pindi
unapotambua katika moyo wa mtu au sehemu fulani unayo nafasi na hiyo nafasi
inapewa thamani yake.
Napenda kusema kuwa
watu wengi wamekuwa huru sana na wakati mwingine hata kujisahau pindi
wanapotambua kuwa wana nafasi sehemu fulani mathalani ndugu yako ana nafasi
nzuri serikalini au katika idara fulani basi panaweza kutokea na hali ya
kujiachia na hatimae kuondoa ufanisi wote katika jukumu ulilopewa.
Niseme nafasi yoyote
ili mradi imeitwa nafasi yako basi itakuwa yako siku zote kwakua yeye anayetoa
nafasi ataishikilia pasipo kutokea mtu mwenye uwezo wa mwingine katika
kuhakikisha kuondoa nafasi yako ni kweli wakati mwingine katika macho unaweza
kuona sehemu fulani hauna nafasi lakini pindi utakapo angali kwa jicho la tatu
basi unaweza kuona nafasi yako kuwa ni kubwa kuliko unavyofikiria.
Nafasi yako huwa
haibadilishwi na mtu unaweza kuona kwa macho yako imebadilishwa na mtu lakini
ukweli kwamba katika macho ya Mungu bado ipo palepale alipoweka yeye na sio
palipo na jicho la wanadamu,
Ni kweli kumetokea
matendo mabaya pindi mtu anapogundua nafasi yake imebadilishwa hama haipo tena
watu uweza kuuana,chuki zilizojikita ndani ya mizizi ya mwanadamu, maamuzi
magumu yasiyokuwa na sababu yaliyobeba hatima mbaya katika maisha ya mtu husika
na hata kwa jamii husika na wanaomtegemea.
Kisilani kikubwa uwa
kinaibuka pale tu unapotambua nafasi yako haipo tena mahali ambapo palichangia
ustawi wako mathalani kazini labda ulikuwa mkurugenzi lakini ghafla ukatolewa
hapo na kujikuta kibarua akipo tena na unajua kuwa kupitia hapo ulikuwa
unaendesha maisha yako na familia yako inakuwa katika hali nzuri,na wakati
mwingine mathalani mchumba wako anaweza alikuwa anawezesha maisha yako katika
kukupatia feha ilikujikimu katika maisha yako lakini unapoona nafasi yako haipo
tena utakumbuka mbali sana kama ulikuwa sehemu nzuri sana sasa unarudi sehemu
mbaya tofauti na matarajio yako.
Niseme sio njia sahihi
kuwa na kinyongo na mtu na kutaka kulipa kisasi kwa yale aliyokutendea bali
kubwa hapo ni kurudi kwa yeye mtoa nafasi na ndiye atakuweka katika nafasi hiyo
au kukupandisha katika nafasi iliyoko juu zaidi sana kuliko ulivyofikiria.
*Acha ugomvi usio na
maendeleo na vita ya kugombania nafasi na hatimae kufananishwa na watoto
wanaogombana kisa mwenzake kachukua nyama yake na uweza kususa hata kula pasipo
kujua kuwa nyama peke yake haishibishi na zaidi sana yuko ambaye aliyenunua
nyama anaweza kukupa kubwa kuliko hiyo lakini watoto huishia kuchukiana na
kusema huyu sili naye tena, japo watoto ugomvi wao ahudumu muda wote tofauti na
watu wazima.
Niseme kwamba nafasi
yoyote utakayokuwepo lazima uitambue kuwa ni Mungu amekupa na yeye ndiye
anahusika na maisha yako hivyo kuzidi kumuheshimu yeye na kufuata njia zake ni
kitu muhimu sana na vilevile usifikiri kuwa sasa hapo ndio umeshafika bado
unasafari ndefu sana.
Lazima ujue kuwa ustawi
wa maisha yako umebebwa na Mungu na sio kitu kingine hivyo tumia muda mwingi
katika kuhakikisha unaheshimu chanzo sahihi cha nafasi yako.
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson…………………………………………………………0764 018535
ONDOA HOFU NAFASI YAKO INALINDWA NA
MUNGU!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni