Jumanne, 29 Desemba 2015
URAFIKI NA MUNGU: SWALI LISILO NA JIBU!
URAFIKI NA MUNGU: SWALI LISILO NA JIBU!: SWALI LISILO NA JIBU Mwanzo 41:8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wo...
SWALI LISILO NA JIBU!
SWALI LISILO NA JIBU
Mwanzo
41:8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa
Misri, na watu wote wenye hekima
walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao
mambo hayo.
KARIBU……………………….!!
Kwa mwalimu mwenye
mapenzi mema na wanafunzi wake pindi inapotokea ametunga mtihani na baadhi ya
maswali au swali pakatokea makosa kwa kutumia busara weza kutoa alama za bure
katika hilo swali au maswali!
Na tukiingia katika
maisha ya kila siku kuna mambo mengine yanakutokea katika maisha yako yanaweza
kuwa magumu sana lakini pindi huo ugumu
utakapokuwa sio wakudumu/baada ya kupata jibu basi tunaita ni changamoto ya
kitambo lakini pindi jambo hilo litakaposababisha akili yako kukosa mwelekeo
mwingine tunaita jambo lilikosa jibu na hatimae uweza kupelekea akili kufika mwisho! Sikatai katika
hali ya kisomi na hata ya kikawaida(kijamii)
katika maswali yako yenye majibu na yako yasiyo na majibu na maswali
haya kwa jina lingine uweza kuitwa maswali yenye utata!au yaliyoshindikana.
►Hivi kwanini niko hapa
na wala sio kule?Hivi kwa nini nilizaliwa huku na sikuzaliwa kule? Hivi kwanini
nilikutana na huyu na wala sikukutana na Yule? kwanini napenda hiki na sipendi
kile kile? Na hivi kwanini sikuwaza vile ni kawaza hivi? Hivi ni kwanini
nilitamani vile wala sikutamani hivi?………………………………!!!
Hivi kwanini niliishia
pale sikuishia hapa? Hivi kwanini niliomba hivi sikuomba vile? Hivi kwanini
naomba hivi na wala siombi vile? Hivi kwanini nachoka hivi na wala sichoki vile?.............................................!!!
Haya yote ni aina ya
maswali ambayo mwanadamu mwenye akili timam lazima ajiiulize na wakati mwingine
uweza kuijiuliza hivi mimi nimemkosea Mungu kitu gani mpaka ni kawa hivi
nilivyo leo au nilivyoleo mimi binafsi nilifanya jambo gani? Lakini wengi uweza
kujijibu majibu yaliyo kawaida ya wanadamu na mengine kukosa majibu kabisa
lakini wengi watasema ni neema ya Mungu! Hasa katika hali njema.
Ni wazi tu kuwa jibu la
kujipa mwenyewe kutokana na ukawaida wa wengi unakuwa na nguvu pale tu
utakapoona jibu ulilolipata ni sawa na ulivyofikiria lakini pindi itakapo kuwa
kinyume na vile ulivyokusudia ndipo hapo akili inakosa mwegemeo na kuanza
kuyumbayumba kwakukosa mwelekeo uliothabiti katika kushikiria.
Japo na kubaliana
kabisa jambo lolote zuri uzaliwa katika wazo na baadae kupelekea utekelezaji na
pindi utakapokuwa ukiwaza kuna maswali yatakuwa yakiibuka na yote ni katika
kukusaidia namna ya kuteleza lile wazo ulilokuwa nalo katika mkakati wako
uliokuwa nao. Katika hilo unaweza kuwa na maswali yakapata jibu na mengine
yakakosa jibu kutokana na imani
iliyondani yako au kutokana na mawazo ya watu yaliyo katika hali ya kusikika au
kuandikikwa.
Na pindi utakapo fikia
kipindi cha swali kukosa jibu hapo uwezekano wakufanya jambo lisilopaswa ni
mkubwa sana au kufanya jambo nje ya matarajio yako au katika mipango yako kuwa
kufanyika kuwa tofauti, kuna wakati unaweza fikiri kuwa unalo jibu sahihi
lakini pindi utakaposhindwa kufanikiwa basi litakuwa swali lisilo na jibu mathalani
mtu anaweza kuhisi kuwa anaumwa ugonjwa wakichwa na bila wasiwasi akaenda duka
la dawa na kununua dawa lakini pindi hiyo dawa ikashindwa kutibu kichwa chake
ndipo hapo ataanza kuona ugumu wa swala linalo mkabili na kuanza kutumia muda
wake na fedha zake katika kushughulikia tatizo linalo mkabali katika kila kona
na pindi jitihada zake zitakapofika mwisho pasipo mwelekeo wa kupata nafuu hapo
bila shaka itazaliwa swali lililokosa jibu!
Ni jambo linaloleta
huzuni sana pindi unapotambua swali ulilonalo limekosa jibu kwa maana nyingine
kama ni mwanafunzi basi hapo kosa ni haki yako na kama ni maisha basi yanaweza
kuwa na mwelekeo mwingine na anaweza asiupende au upande mbaya.
Kunakuwa ni wakati
mgumu sana kwa mtu pindi anapokuwa na wakati ambao haoni jibu sahihi, wako watu
wajiingiza katika ulevi uliopitiliza, wengine wanakuwa makahaba, wengine
wanakuwa na maisha ya upweke na hata mwingine kufikia hatua ya kujiua.
Katika kipindi hiki
hata profesa/ata watu wenye uweza mkubwa
la kusaidia jamii lakini unaweza kuta kufanya jambo ambalo kwa hakika ukilisikia hutaweza
kuamini kama ndiyo yeye amefanya jambo hilo na hata kushindwa kujua kwa nini
amefikia hatua hii, wako watu wanafika hatua ya kuuana kwa sababu amefikiria
sana lakini bado amekosa jibu hasa la kujibu moyo wake na moyo wake ukatulia.
Unaweza kuwa na mtu
mwenye heshima katika kijiji/mtaa wako lakini baada ya maswali yako kukosa jibu
unaweza ukakuta kafanya jambo ambalo hata chizi hawezi kufanya jambo hilo na
watu wote kubaki kushangaa lakini yote ni matokeo ya swali lako kukosa jibu!
►Swali lililokosa jibu
ni mateso ya akili na ni usumbufu wa moyo na zaidi sana adhabu katika maisha
yako!
*Mwisho wa swali hili
ni mpaka pale utakapotambua Mungu ni mkubwa na mpana sana katika maisha yako na
hapo akili yako itakapoelewa kuwa kweli uwezo wa Mungu hauna kipimo chake
anaweza fanya jambo lolote wakati wowote na katika mazingira yoyote!
*Hapa ndipo sehemu
sahihi ya kusema acha Mungu aitwe Mungu kwakua unakuwa umemuona katika maisha
yako na sio habari ya kusikia kwa mtu na ni mahali ambapo akili yako inapata
funzo jingine na kupata hatua nyingine!
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson…………………………………………0764 018535
Jumanne, 22 Desemba 2015
MUNGU HAKOSEI
MUNGU HAKOSEI
Hili swala sio la
kusikia tu ukaishia hapo bali ni hali halisi ya moyo wako kukwambia kuwa Mungu
hakosei kwa uthibitisho wa Roho mtakatifu ndani yako. Japo ni kweli kukosea ni
sifa ya binadamu lakini sio sifa ya Mungu na pindi utakapo amua kwa dhati kumbeba
Mungu itakuwa si rahisi kwa wewe kukosea kwani uwezo wa Mungu utakuwa
umekufunika katika hali ya kukuwezesha.
Ni rahisi kumshukuru
Mungu katika jambo jema alilokutendea na pia ni rahisi kunung’unika katika
jambo baya ambalo litakalo kupata! Katika maisha yako ya kila siku ni vizuri
utambue kwamba kosa lako sio kosa la Mungu na pia kushindwa kwako sio kushindwa
kwa Mungu.
Ni kweli kama binadamu
mabaya yanaweza kukukabili lakini hapo sio fursa ya kuona kuwa Mungu amekosea
kwa wewe kupitia hali ngumu japo wakati mwingine unaweza kuona mambo
yamekuandama ukaanza kufikiri na kusema Mungu anioni.
Hili ni neno kwa namna
ya uhalisia wake unaweza sema AMEN kweli Mungu ajawai kukosea na kamwe
hatakosea kwakua kazi zake ni kamilifu, na kunakipindi unaweza kuwa njia panda
kujua huyu ni kweli Mungu wa huruma kweli au ! na wakati mwingine unaweza
kusema katika jambo hili Mungu ajakutendea haki kwa maana nyingine amekuonea!
Ukweli uponyaji wa
hatua hii unahitaji sana ufahamu wako kuweza kumwelewa Mungu kwa namna ya
kimungu tu! Zaidi ya hapo ukweli hautaweza kuona ukamilifu wa Mungu katika kila
jambo linalokutokea kwani unaweza kuyumbishwa kama upepo huku na huko.
Ni maisha mengine
utaanza kuishi pindi utakapoweka kwenye ufahamu wako kuwa Mungu ajawai kukosea
na hata kosea hata kama jambo lolote likikukuta haijarishi jambo hilo ni baya
kiasi gani? Niseme tu kuna maisha watu wengi wanaishi katika mateso na dhiki na
kugandamizwa pasipo kujua kuwa uwa Mungu hakoseibali wanaishia kulalamika, wako
watu wanaishi maisha yasiyo ya kwao kutokana mioyo yao imejaa lawama kuhusu
Mungu kwa kuona anaruhusu mabaya katika maisha yake siku zote.
Matokeo ya watu kuona
Mungu anakosea matunda yake kama ifuatavyo,wako watu hawana tena imani ya
ukristo walionao wamekuwa hawaoni maana ya kwenda kanisani, hata thamani ya
mchungaji na kuona nafasi yake haipo katika kanisa, mtu huyu amejawa na lawama
maisha yake yote…….mtu huyu hana maombi zaidi ya malalamiko, hana maneno mazuri
ya Mungu zaidi ya kulaumu. Zaburi 36:3 “Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na
akili na kutenda mema.”
Ni kweli hauwezi kuwa
mtu wa tofauti kama tu ufahamu wako umejawa na hali ya kuona Mungu anakosea
itakuwa ni kizingiti kitachoshika maisha yako na mbaya zaidi kitasambazaa hata
kwa watoto wako huzuni yako haitakuwa
kwako tu bali hata kwa wale watakao kufuata wata beba msalaba wako.
Waebrania
11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.
Napindi utakapo tambua
kuwa Mungu hakosei hapo itakuhakikishia ushindi wa kimungu katika yale
yanayokukabili kwakua katika dogo utakapo ona uweza wa Mungu bila shaka Mungu
naye atakushangaza kukufanyia makubwa zaidi ……….hii tunaiona pale yesu walipo
pewa mikate mitano na samaki wawili yesu alishukuru kwa kile kilichopo na Mungu
akaanza kukizidisha sawa na uhitaji uliokuwepo,
Mathayo
14:19 “Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na
wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate,
akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano”
Napenda kusema kwa
kiasi kikubwa utendaji wa Mungu utegemea sana na vile unavyomuona au mwamini,
imani yako ndio kigezo kikubwa katika kuhakikisha kunautendaji wa kimbingu ndo
mana biblia inasema kuwa pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu…( waebrania
11:6).
Luka
17:6 “Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali,
mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii”
Hivyo ufahamu wako
unaweza kuleta giza katika maisha yako au nuru katika maisha yako kutokana
mtazamo wako usio sahihi kuhusu Mungu, ukomboe ufahamu wako katika kuimarisha
kumjua
Mungu katika njia iliyo sahihi nasio ya kujifariji tu! Pasipokuwa
na muelekeo ulio sawa.
Japo kweli kila jambo
linalotokea linakuwa na sababu yake mengine nikutaka kujua ubora wa imani yako
ulionayo kwa Mungu,mengine ni kukumbusha katika utumishi ulio sahihi, kurejea
kwa toba mbele za Mungu na mengine mengi ambayo Mungu anaweza kukupa tafsiri yake.
Kuna aina mbili ya
maisha kati ya maisha ya kumuona Mungu anakosea na kuona Mungu hakosei kila
maisha yana namna yake ya kuishi na matokeo yake, hivyo usikubali kuishi maisha
ya kuona Mungu anakosea kwani utaweza kuwa na imani potofu, ugumu wa moyo na
kutokuwa tayari katika kumtumikia Mungu kwa ukamilifu.
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson………………………………………………………………0764 018535
Jumanne, 8 Desemba 2015
HAIJUI KESHO YAKO
HAIJUI KESHO YAKO
Yako maneno ambayo
hayasauliki wala kufutika katika maisha ya mtu kirahisi hata kama hayo maneno
ajayahifadhi katika moyo wake mathalani HAUTA FIKA, UTANIKUMBUKA, UTAIONA
DUNIA, UTAKUJA KWA MAGOTI, HAUTA PONA, UMEFIKA MWISHO, UTAJUTA,
SINILISEMA,UMEKWISHA.
Pia yako matendo ambayo
mtu akikufanyia uwezi kusahau na hasa yakiwa yana ashiria mwisho wa hatua
katika maisha yako yanaweza kuweka alama katika maisha yake na kutia hofu
katika maisha yako, lakini.pindi unapotambua kuwa hakuna mtu anaijua kesho yako
hii ni siraha kubwa sana kwa wewe kushinda kwakua utatumia muda mzuri katika
kufanikisha lile kusudi ambalo Mungu amelikwa ndani yako kuliko kuangalia
mwitikio wa kile unachokifanya au kile unachokiangalia kukifanya.
Hakuna kitu kizuri kama mtu unayepigana nawe
kutojua chanzo cha nguvu zako…..tukimwangalia daudi alipokuwa akimkabili
goliati, goliati alimdharau daudi kutokana na kutojua chanzo,asili ya nguvu
zake au kujiamini kwake na hapo ndipo chanzo cha kushindwa kwa goliati na laiti
goliati angelijua chanzo cha nguvu zake daudi asinge thubutu kupambana nae.
Nikutoe tu hofu katika
kila jambo unalolikabili jua kwamba kama mtu ajui kesho yako tambua kuwa kufika
ni lazima kwakua njia yako ni upofu kwa wengine hivyo kamwe hawawezi kuzuia kwa
ukamilifu japo anaweza kuzani kuwa anaziba njia lakini ukweli unabaki njia yako
inakuwa iko wazi kwa ajili ya Mungu kukufikisha.
Unapoona ukombozi wa
mwanadamu, yesu alipokuja duniani katika kuleta ukombozi kwa mwanadamu ambaye
yeye aliwapenda sana…….. lakini shetani alijua kwa kuhakikisha yesu anapotea
ulimwenguni kwa haraka ili aendelee katika kutawala dunia lakini akujua kuwa
haraka yake katika kumpoteza yesu kumbe ndio hatarisha maisha yake katika
utawala wake duniani.
Unahaja ya kuweka
kisirani kwa mtu wala kisasi kwa lolote linalo kukabili kwakua yeye Mungu
alianza kukupa nuru katika duniani atakufikisha kule unakotakiwa kufika kwakua
yeye ndio anajua njia ya kukufikisha kule unakotakiwa kufika, lakini sumu kwako
inaweza kutokea pindi ukaona katika mwisho wako ni sawa na neno la mtu na ukaanza kujipanga katika kukabiliana
na ushindani na mtu huyu pasipo kuweka
mwelekeo wako kwa Mungu tu hapa kushindwa au kuchelewa ni haki yako.
Niseme tu kuwa
kushindwa kufika kesho yako ni wewe mwenyewe na sio kitu kingine japo vikwazo
vinatokea ni kawaida tu na sio uone kuwa Mungu hana upendo na wewe kutokana na yale yanayokukabili, lazima ujifunze kitu
kimoja kukaa mahali ambapo unaonekana hauna kibali kwa wote lakini namna ya
kuishi hapo ndio msingi mzuri wa kuinuka kwako au wakishindwa kwako.
Usiwe
mwepesi wa kukimbia katika kila mazingira yanayokukabili………mwangalia daudi
alipokaa na Esau wakati akiwa hana kibali kwa mfalme Esau lakini alitambua
namna ya kukaa nae.
Na hali ya mtu kutojua
kesho yako haina maana sasa kuanza kudharau wenzako na kuona hawana mchango
wowote katika maisha yako jua hili litakuwa kikwazo kwako na sio tumaini kwako
na inaweza kusababisha kushindwa kule unakotakiwa kufika, sikuzote unyenyekevu
na upole pamoja mshikamano wa wewe na Mungu na kuthamini kwa wengine kuliko
wewe binafsi uwe dira ya maisha yako.
Nikukumbushe kuwa
thamani yako inategemea sana na namna ya unavyowathamini wengine kwakua Mungu
anataka KUMPENDA JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO fanya jambo kwa uelewa na katika
hali ya uelewa uliosahihi na sio kwa hofu isiyotokana na Mungu.
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson…………………………..0764 018535
BARIKIWA NDUGU!!!
Jumanne, 1 Desemba 2015
MAPENZI YA MUNGU
MAPENZI YA MUNGU
Hili neno MAPENZI sio
jambo la kushangaza katika ulimwengu wa leo lakini kubwa zaidi ni namna
linavyopewa nafasi katika dunia ya leo, kimekuwa kama kitu cha mpito tu kwani
leo unaweza kuwa na mapenzi na huyu na bila wasiwasi kesho ukawa na mapenzi na
mwingine na huku moyo wako ukiwa umejaa ujasiri wote pasipo uwoga wowote na
mbaya zaidi unaweza kujisifia kuwa hali hiyo ndio ukisasa wenyewe imekuwa hivyo
kwa muda……mathalani ya mlo asubui utakunywa chai na maandazi na jioni unaweza
kuamua kula wali na dagaa sawa sawa na uwezo wa uchumi wa mtu na maamuzi ya
mtu.
Niseme tu kuwa chezea
mapenzi yoyote kati yako na wanyama, jirani na hata rafiki lakini sio mapenzi
ya Mungu katika maisha yako, niseme haya mapenzi hayabadilishwi
kirahisikirahisi leo utaamua kuwa na mapenzi na Mungu kesho utaki tena kuwa na
mapenzi alafu baadae kidogo ukaamua kurudi tena kuwa na mapenzi na Mungu.
MAPENZI YA MUNGU!
Hiki ni kitu kingine
kwani kinausisha maumivu ya mwili na mateso ya nafsi katika kutimiza matakwa au
mapenzi ya Mungu, ni wazi pindi utakapo amua kuanza kuyaishi haya mapenzi ya
Mungu kwa ukamilifu bila shaka utaanza kuliona penzi la Mungu likiidhihirika
kwa upya katika maisha yako likitofautisha maisha yako na watu wengine.
Penzi la Mungu kuliishi
sio jambo la kufikirika tu kumbuka yesu katika kutimiza matakwa ya baba yake
ili mgharim mateso ya mwili wake ndomana nafsi yake iliteseka sana kwa kuona
kile kitakachompata katika kutimiza lile neno ambalo Mungu mwenyewe alilo liongea
pale bustanini eden kuwa uzao wa mwanamke utakuponda kichwa nyoka.
Ni wazi pindi
utakapoanza kutekeleza mapenzi ya Mungu lazima yako yavunjike kama ilivyo kawaida
unapotaka kutekeleza mapenzi ya mtu lazima yako ya teketee ili utoe fursa
katika kutekeleza mapenzi ya mwingine, na kamwe hauwezi kutekeleza mapenzi yako
huku unatekeleza mapenzi ya mwingine kwa ufasaha zaidi.
Moja ya sumu kubwa
katika ushirika wa watu wowote ni hali ya kushindwa kuteleza matakwa ya
mwingine, watu wengi wanaachana kuona kwamba huyu mchumba,rafiki,ndugu niliye
naye amejaa maslai binafsi yeye anajali maisha yake zaidi kuliko maisha ya
mwingine hivyo sioni sababu ya mimi kuendelea nae.
Hata katika biblia amri
ngumu ambayo watu wengi watakayoshindwa ni KUMPENDA JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO
hii inaweza kubaki katika maandiko tu na wala neno hili lisitoke na kuwa na
athari au kuwa halisi katika maisha tunayoishi.
Niseme pindi unaposikia
MAPENZI YA MUNGU huu ni jumla ya mambo ya Mungu ambayo yamebebwa au yanabebwa
na mtu mwenye ufahamu kamili ambao unajua unafanya kitu gani? Na kamwe hajali
hasara zake kuwa ni kikwazo katika kufanikisha kile kitu ambacho Mungu
anakitaka toka kwake, kwa maana nyingine mtu huyu hayuko tayari kumfurahisha
MTU au YEYE mwenyewe zaidi ya kukamilisha kile ambacho Mungu anataka
akikamilishe kwa ufasaha zaidi.
Furaha yake ni kuona
lile lililokuwa penzi la Mungu kwake linakamilika tena katika mafanikio makubwa
pasipo hata kuacha chembe ya kitu chochote kutotimia, na kwa maana hiyo
usingizi wake unakuja baada ya kuona la Mungu limesha timia.
Niseme tu wazi hauwezi
kujiita kuwa unafanya mapenzi ya Mungu kwakua unafahamika kanisani vizuri na
mchungaji au waumini wenzako bali ni vile nafsi yako inavyo kushuhudia na sio
lazima uwe mtakatifu sana bali kuwa halisi mbele za Mungu kuwa ndio wewe hakuna
mbadala hali hii inabidi ujifahamu wewe binafsi.
Pia kutembea katika
karama au huduma yoyote ambayo Mungu amekupa hichi sio kigenzo cha kuonyesha
sasa wewe unatembea katika mapenzi ya Mungu, kwani unaweza kufanya ubadhilifu
na bado ukatembea katika karama za rohoni kwani Mungu ameziachilia kwa kusudi
lake kwa ajili ya kufanyika baraka kwa watu wengine lakini sio kwako.
Kuna hasara kubwa
kufanya mambo ya kimungu pasipo kutembea katika mapenzi ya Mungu unaweza
kupoteza uzima wa Mungu ndani yako na kule unakotarajia kwenda yaani mbinguni,
jali sana utendaji wako katika mapenzi ya Mungu kuliko sifa za watu katika
maisha yako.
Imeandaliwa
na ;
Cothey
Nelson……………………………………………………………….0764 018535
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)