MAPENZI YA MUNGU
Hili neno MAPENZI sio
jambo la kushangaza katika ulimwengu wa leo lakini kubwa zaidi ni namna
linavyopewa nafasi katika dunia ya leo, kimekuwa kama kitu cha mpito tu kwani
leo unaweza kuwa na mapenzi na huyu na bila wasiwasi kesho ukawa na mapenzi na
mwingine na huku moyo wako ukiwa umejaa ujasiri wote pasipo uwoga wowote na
mbaya zaidi unaweza kujisifia kuwa hali hiyo ndio ukisasa wenyewe imekuwa hivyo
kwa muda……mathalani ya mlo asubui utakunywa chai na maandazi na jioni unaweza
kuamua kula wali na dagaa sawa sawa na uwezo wa uchumi wa mtu na maamuzi ya
mtu.
Niseme tu kuwa chezea
mapenzi yoyote kati yako na wanyama, jirani na hata rafiki lakini sio mapenzi
ya Mungu katika maisha yako, niseme haya mapenzi hayabadilishwi
kirahisikirahisi leo utaamua kuwa na mapenzi na Mungu kesho utaki tena kuwa na
mapenzi alafu baadae kidogo ukaamua kurudi tena kuwa na mapenzi na Mungu.
MAPENZI YA MUNGU!
Hiki ni kitu kingine
kwani kinausisha maumivu ya mwili na mateso ya nafsi katika kutimiza matakwa au
mapenzi ya Mungu, ni wazi pindi utakapo amua kuanza kuyaishi haya mapenzi ya
Mungu kwa ukamilifu bila shaka utaanza kuliona penzi la Mungu likiidhihirika
kwa upya katika maisha yako likitofautisha maisha yako na watu wengine.
Penzi la Mungu kuliishi
sio jambo la kufikirika tu kumbuka yesu katika kutimiza matakwa ya baba yake
ili mgharim mateso ya mwili wake ndomana nafsi yake iliteseka sana kwa kuona
kile kitakachompata katika kutimiza lile neno ambalo Mungu mwenyewe alilo liongea
pale bustanini eden kuwa uzao wa mwanamke utakuponda kichwa nyoka.
Ni wazi pindi
utakapoanza kutekeleza mapenzi ya Mungu lazima yako yavunjike kama ilivyo kawaida
unapotaka kutekeleza mapenzi ya mtu lazima yako ya teketee ili utoe fursa
katika kutekeleza mapenzi ya mwingine, na kamwe hauwezi kutekeleza mapenzi yako
huku unatekeleza mapenzi ya mwingine kwa ufasaha zaidi.
Moja ya sumu kubwa
katika ushirika wa watu wowote ni hali ya kushindwa kuteleza matakwa ya
mwingine, watu wengi wanaachana kuona kwamba huyu mchumba,rafiki,ndugu niliye
naye amejaa maslai binafsi yeye anajali maisha yake zaidi kuliko maisha ya
mwingine hivyo sioni sababu ya mimi kuendelea nae.
Hata katika biblia amri
ngumu ambayo watu wengi watakayoshindwa ni KUMPENDA JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO
hii inaweza kubaki katika maandiko tu na wala neno hili lisitoke na kuwa na
athari au kuwa halisi katika maisha tunayoishi.
Niseme pindi unaposikia
MAPENZI YA MUNGU huu ni jumla ya mambo ya Mungu ambayo yamebebwa au yanabebwa
na mtu mwenye ufahamu kamili ambao unajua unafanya kitu gani? Na kamwe hajali
hasara zake kuwa ni kikwazo katika kufanikisha kile kitu ambacho Mungu
anakitaka toka kwake, kwa maana nyingine mtu huyu hayuko tayari kumfurahisha
MTU au YEYE mwenyewe zaidi ya kukamilisha kile ambacho Mungu anataka
akikamilishe kwa ufasaha zaidi.
Furaha yake ni kuona
lile lililokuwa penzi la Mungu kwake linakamilika tena katika mafanikio makubwa
pasipo hata kuacha chembe ya kitu chochote kutotimia, na kwa maana hiyo
usingizi wake unakuja baada ya kuona la Mungu limesha timia.
Niseme tu wazi hauwezi
kujiita kuwa unafanya mapenzi ya Mungu kwakua unafahamika kanisani vizuri na
mchungaji au waumini wenzako bali ni vile nafsi yako inavyo kushuhudia na sio
lazima uwe mtakatifu sana bali kuwa halisi mbele za Mungu kuwa ndio wewe hakuna
mbadala hali hii inabidi ujifahamu wewe binafsi.
Pia kutembea katika
karama au huduma yoyote ambayo Mungu amekupa hichi sio kigenzo cha kuonyesha
sasa wewe unatembea katika mapenzi ya Mungu, kwani unaweza kufanya ubadhilifu
na bado ukatembea katika karama za rohoni kwani Mungu ameziachilia kwa kusudi
lake kwa ajili ya kufanyika baraka kwa watu wengine lakini sio kwako.
Kuna hasara kubwa
kufanya mambo ya kimungu pasipo kutembea katika mapenzi ya Mungu unaweza
kupoteza uzima wa Mungu ndani yako na kule unakotarajia kwenda yaani mbinguni,
jali sana utendaji wako katika mapenzi ya Mungu kuliko sifa za watu katika
maisha yako.
Imeandaliwa
na ;
Cothey
Nelson……………………………………………………………….0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni