Jumanne, 29 Desemba 2015

SWALI LISILO NA JIBU!



SWALI LISILO NA JIBU

 Mwanzo 41:8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na   watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.

KARIBU……………………….!!
Kwa mwalimu mwenye mapenzi mema na wanafunzi wake pindi inapotokea ametunga mtihani na baadhi ya maswali au swali pakatokea makosa kwa kutumia busara weza kutoa alama za bure katika hilo swali au maswali!

Na tukiingia katika maisha ya kila siku kuna mambo mengine yanakutokea katika maisha yako yanaweza kuwa magumu sana lakini pindi huo  ugumu utakapokuwa sio wakudumu/baada ya kupata jibu basi tunaita ni changamoto ya kitambo lakini pindi jambo hilo litakaposababisha akili yako kukosa mwelekeo mwingine tunaita jambo lilikosa jibu na hatimae uweza kupelekea akili kufika mwisho! Sikatai katika hali ya kisomi na hata ya kikawaida(kijamii)  katika maswali yako yenye majibu na yako yasiyo na majibu na maswali haya kwa jina lingine uweza kuitwa maswali yenye utata!au yaliyoshindikana.

►Hivi kwanini niko hapa na wala sio kule?Hivi kwa nini nilizaliwa huku na sikuzaliwa kule? Hivi kwanini nilikutana na huyu na wala sikukutana na Yule? kwanini napenda hiki na sipendi kile kile? Na hivi kwanini sikuwaza vile ni kawaza hivi? Hivi ni kwanini nilitamani vile wala sikutamani hivi?………………………………!!!

Hivi kwanini niliishia pale sikuishia hapa? Hivi kwanini niliomba hivi sikuomba vile? Hivi kwanini naomba hivi na wala siombi vile? Hivi kwanini nachoka hivi na wala sichoki vile?.............................................!!!

Haya yote ni aina ya maswali ambayo mwanadamu mwenye akili timam lazima ajiiulize na wakati mwingine uweza kuijiuliza hivi mimi nimemkosea Mungu kitu gani mpaka ni kawa hivi nilivyo leo au nilivyoleo mimi binafsi nilifanya jambo gani? Lakini wengi uweza kujijibu majibu yaliyo kawaida ya wanadamu na mengine kukosa majibu kabisa lakini wengi watasema ni neema ya Mungu! Hasa katika hali njema.

Ni wazi tu kuwa jibu la kujipa mwenyewe kutokana na ukawaida wa wengi unakuwa na nguvu pale tu utakapoona jibu ulilolipata ni sawa na ulivyofikiria lakini pindi itakapo kuwa kinyume na vile ulivyokusudia ndipo hapo akili inakosa mwegemeo na kuanza kuyumbayumba kwakukosa mwelekeo uliothabiti katika kushikiria.

Japo na kubaliana kabisa jambo lolote zuri uzaliwa katika wazo na baadae kupelekea utekelezaji na pindi utakapokuwa ukiwaza kuna maswali yatakuwa yakiibuka na yote ni katika kukusaidia namna ya kuteleza lile wazo ulilokuwa nalo katika mkakati wako uliokuwa nao. Katika hilo unaweza kuwa na maswali yakapata jibu na mengine yakakosa jibu kutokana na  imani iliyondani yako au kutokana na mawazo ya watu yaliyo katika hali ya kusikika au kuandikikwa.

Na pindi utakapo fikia kipindi cha swali kukosa jibu hapo uwezekano wakufanya jambo lisilopaswa ni mkubwa sana au kufanya jambo nje ya matarajio yako au katika mipango yako kuwa kufanyika kuwa tofauti, kuna wakati unaweza fikiri kuwa unalo jibu sahihi lakini pindi utakaposhindwa kufanikiwa basi litakuwa swali lisilo na jibu mathalani mtu anaweza kuhisi kuwa anaumwa ugonjwa wakichwa na bila wasiwasi akaenda duka la dawa na kununua dawa lakini pindi hiyo dawa ikashindwa kutibu kichwa chake ndipo hapo ataanza kuona ugumu wa swala linalo mkabili na kuanza kutumia muda wake na fedha zake katika kushughulikia tatizo linalo mkabali katika kila kona na pindi jitihada zake zitakapofika mwisho pasipo mwelekeo wa kupata nafuu hapo bila shaka itazaliwa swali lililokosa jibu!

Ni jambo linaloleta huzuni sana pindi unapotambua swali ulilonalo limekosa jibu kwa maana nyingine kama ni mwanafunzi basi hapo kosa ni haki yako na kama ni maisha basi yanaweza kuwa na mwelekeo mwingine na anaweza asiupende au upande mbaya.

Kunakuwa ni wakati mgumu sana kwa mtu pindi anapokuwa na wakati ambao haoni jibu sahihi, wako watu wajiingiza katika ulevi uliopitiliza, wengine wanakuwa makahaba, wengine wanakuwa na maisha ya upweke na hata mwingine kufikia hatua ya kujiua.

Katika kipindi hiki hata profesa/ata watu wenye  uweza mkubwa la kusaidia jamii lakini unaweza kuta  kufanya jambo ambalo kwa hakika ukilisikia hutaweza kuamini kama ndiyo yeye amefanya jambo hilo na hata kushindwa kujua kwa nini amefikia hatua hii, wako watu wanafika hatua ya kuuana kwa sababu amefikiria sana lakini bado amekosa jibu hasa la kujibu moyo wake na moyo wake ukatulia.

Unaweza kuwa na mtu mwenye heshima katika kijiji/mtaa wako lakini baada ya maswali yako kukosa jibu unaweza ukakuta kafanya jambo ambalo hata chizi hawezi kufanya jambo hilo na watu wote kubaki kushangaa lakini yote ni matokeo ya swali lako kukosa jibu!

►Swali lililokosa jibu ni mateso ya akili na ni usumbufu wa moyo na zaidi sana adhabu katika maisha yako!

*Mwisho wa swali hili ni mpaka pale utakapotambua Mungu ni mkubwa na mpana sana katika maisha yako na hapo akili yako itakapoelewa kuwa kweli uwezo wa Mungu hauna kipimo chake anaweza fanya jambo lolote wakati wowote na katika mazingira yoyote!

*Hapa ndipo sehemu sahihi ya kusema acha Mungu aitwe Mungu kwakua unakuwa umemuona katika maisha yako na sio habari ya kusikia kwa mtu na ni mahali ambapo akili yako inapata funzo jingine na kupata hatua nyingine!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni