MUNGU HAKOSEI
Hili swala sio la
kusikia tu ukaishia hapo bali ni hali halisi ya moyo wako kukwambia kuwa Mungu
hakosei kwa uthibitisho wa Roho mtakatifu ndani yako. Japo ni kweli kukosea ni
sifa ya binadamu lakini sio sifa ya Mungu na pindi utakapo amua kwa dhati kumbeba
Mungu itakuwa si rahisi kwa wewe kukosea kwani uwezo wa Mungu utakuwa
umekufunika katika hali ya kukuwezesha.
Ni rahisi kumshukuru
Mungu katika jambo jema alilokutendea na pia ni rahisi kunung’unika katika
jambo baya ambalo litakalo kupata! Katika maisha yako ya kila siku ni vizuri
utambue kwamba kosa lako sio kosa la Mungu na pia kushindwa kwako sio kushindwa
kwa Mungu.
Ni kweli kama binadamu
mabaya yanaweza kukukabili lakini hapo sio fursa ya kuona kuwa Mungu amekosea
kwa wewe kupitia hali ngumu japo wakati mwingine unaweza kuona mambo
yamekuandama ukaanza kufikiri na kusema Mungu anioni.
Hili ni neno kwa namna
ya uhalisia wake unaweza sema AMEN kweli Mungu ajawai kukosea na kamwe
hatakosea kwakua kazi zake ni kamilifu, na kunakipindi unaweza kuwa njia panda
kujua huyu ni kweli Mungu wa huruma kweli au ! na wakati mwingine unaweza
kusema katika jambo hili Mungu ajakutendea haki kwa maana nyingine amekuonea!
Ukweli uponyaji wa
hatua hii unahitaji sana ufahamu wako kuweza kumwelewa Mungu kwa namna ya
kimungu tu! Zaidi ya hapo ukweli hautaweza kuona ukamilifu wa Mungu katika kila
jambo linalokutokea kwani unaweza kuyumbishwa kama upepo huku na huko.
Ni maisha mengine
utaanza kuishi pindi utakapoweka kwenye ufahamu wako kuwa Mungu ajawai kukosea
na hata kosea hata kama jambo lolote likikukuta haijarishi jambo hilo ni baya
kiasi gani? Niseme tu kuna maisha watu wengi wanaishi katika mateso na dhiki na
kugandamizwa pasipo kujua kuwa uwa Mungu hakoseibali wanaishia kulalamika, wako
watu wanaishi maisha yasiyo ya kwao kutokana mioyo yao imejaa lawama kuhusu
Mungu kwa kuona anaruhusu mabaya katika maisha yake siku zote.
Matokeo ya watu kuona
Mungu anakosea matunda yake kama ifuatavyo,wako watu hawana tena imani ya
ukristo walionao wamekuwa hawaoni maana ya kwenda kanisani, hata thamani ya
mchungaji na kuona nafasi yake haipo katika kanisa, mtu huyu amejawa na lawama
maisha yake yote…….mtu huyu hana maombi zaidi ya malalamiko, hana maneno mazuri
ya Mungu zaidi ya kulaumu. Zaburi 36:3 “Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na
akili na kutenda mema.”
Ni kweli hauwezi kuwa
mtu wa tofauti kama tu ufahamu wako umejawa na hali ya kuona Mungu anakosea
itakuwa ni kizingiti kitachoshika maisha yako na mbaya zaidi kitasambazaa hata
kwa watoto wako huzuni yako haitakuwa
kwako tu bali hata kwa wale watakao kufuata wata beba msalaba wako.
Waebrania
11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.
Napindi utakapo tambua
kuwa Mungu hakosei hapo itakuhakikishia ushindi wa kimungu katika yale
yanayokukabili kwakua katika dogo utakapo ona uweza wa Mungu bila shaka Mungu
naye atakushangaza kukufanyia makubwa zaidi ……….hii tunaiona pale yesu walipo
pewa mikate mitano na samaki wawili yesu alishukuru kwa kile kilichopo na Mungu
akaanza kukizidisha sawa na uhitaji uliokuwepo,
Mathayo
14:19 “Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na
wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate,
akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano”
Napenda kusema kwa
kiasi kikubwa utendaji wa Mungu utegemea sana na vile unavyomuona au mwamini,
imani yako ndio kigezo kikubwa katika kuhakikisha kunautendaji wa kimbingu ndo
mana biblia inasema kuwa pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu…( waebrania
11:6).
Luka
17:6 “Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali,
mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii”
Hivyo ufahamu wako
unaweza kuleta giza katika maisha yako au nuru katika maisha yako kutokana
mtazamo wako usio sahihi kuhusu Mungu, ukomboe ufahamu wako katika kuimarisha
kumjua
Mungu katika njia iliyo sahihi nasio ya kujifariji tu! Pasipokuwa
na muelekeo ulio sawa.
Japo kweli kila jambo
linalotokea linakuwa na sababu yake mengine nikutaka kujua ubora wa imani yako
ulionayo kwa Mungu,mengine ni kukumbusha katika utumishi ulio sahihi, kurejea
kwa toba mbele za Mungu na mengine mengi ambayo Mungu anaweza kukupa tafsiri yake.
Kuna aina mbili ya
maisha kati ya maisha ya kumuona Mungu anakosea na kuona Mungu hakosei kila
maisha yana namna yake ya kuishi na matokeo yake, hivyo usikubali kuishi maisha
ya kuona Mungu anakosea kwani utaweza kuwa na imani potofu, ugumu wa moyo na
kutokuwa tayari katika kumtumikia Mungu kwa ukamilifu.
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson………………………………………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni