ASANTE KWA HILI
Naweza sema ni neno
tamu na lenye mvuto wa kipekee na hasa kwa mtu uliyetegemea aseme ASANTE! Naye
akakubaliana na sauti ya moyo wako na hatimae akasema ASANTE! Na amini utaona
kama unaota na hatimae moyo wako utakuwa na furaha itakayokosa kificho katika
muonekano wanje!
Na kubaliana kuwa neno
ASANTE linafuata baada ya tendo jema mtu alilotendewa, japo kuna wakati unaweza
kutendewa jambo jema lenye maana baadae ila pasipo kujua ni jambo jema kwako
unakosa kuwa na moyo wa shukrani kwa wakati huo……….mathalani mwanafunzi
anapoaandaliwa kuwa mtu fulani katika jamii yake hasa kutokana na kipawa chake
bila shaka katika matengenezo ya kuwa mtu bora sio rahisi kusema ASANTE.
Changamoto kubwa
katika kushukuru kwa jambo unalotendewa ni wazi inakuwa vile watu wote hamjui mnalopaswa
kufanya kwa kuwa inakuwa ni mission ya Mungu katika kumwandaa mtu kuwa MTU
hivyo mnakuta huyu ampendi huyu na huyu anamchukia huyu kumbe hiyo hali
inasababishwa na jambo linaendelea ndani ya Mungu ila hapo kunakuwa na
udhihirishi tu.
Niseme kuna siri kubwa
sana katika kusema asante (shukrani) kuna minyororo inavunjika, kuna kuta
zinabomoka na thamani yake kamwe huwezi kulinganisha na chochote kwani liko vile
kama lilivyo hakika hili neno limebeba utoshelevu na mbaraka wake usio kuwa wa kawaida
ni wewe kuutambua tu.
Nimeona mtu akikatisha
kumsaidia mtu kisa kilikuwa huyu mtu ajui neno ASANTE kinywani mwake hivyo
haoni kile ninachokifanya kama ni cha maana katika maisha yake hivyo sijisikii
kuendelea kumsaidia maana yeye haoni jinsi ninavyojinyima juu yake hivyo ni
bora niangalie kitu kingine ambako Moyo wangu unasukumwa kuwa huko.
Katika yote ni bora
uone hivyo katika upande wa wanadamu wenzako kuwa awanashukrani lakini wanadamu
sasa hivi imekwenda mbali sana kiasi cha kuona hata Mungu pia amewekwa katika
kuchunguzwa kana kwamba ni binadamu kwani nini anitendei mimi au haoni juhudi
zangu kwa ajili yake! Watu wamekuwa na kisasi sio kwa wanadamu bali wamevuka
mpaka hata kwa upande wa Mungu kana kwamba na yeye walishirikiana hama
kushauriana ili kwamba yeye atokee dunia na kujichagulia maisha hayatakayo na
sio aliopangiwa kuishi.
ASANTE KWA
HILI……….usipo ona kuwa Mungu mwema kwa yale yana yofanyika yaliyo nje ya uwezo
wako basi hakuna jambo ukampa thamani yako Mungu katika hali stahiki na katika
mwendelezo unaotakiwa!
Imekuwa kama mtu
ukamfanyia mema mengi pindi anapoona pungufu lake moja basi uweza kusahau yote
basi linakuwa na nguvu zaidi ya mema yake yote , hivi ndivyo watu wanavyoona
kwa Mungu laiti ukikaa chini na kutafakari na kuona jinsi Mungu alivyo mwema
katika maisha yako kamwe usinge fungua mlango mwingine wa kuona upendeleo wa
Mungu kwa wengine kuliko kwako.
Samahi kwa mfano huu japo
sio wote, usiwe na hasira kama mama mjamzito katika miezi ya awali kwani
unaweza ukamfurahisha katika mambo mengi ukimuuzi kitu kimoja tu basi anaweza
akasusa na kuona kila kitu kibaya kwake.
Lazima ujifunze kuona
pamoja na yote lakini katika hili Mungu ni mwema sana ASANTE KWA HILI kwa kuwa hakuna kipimo cha
kupima wema Mungu katika maisha yako na laiti pangekuwa na mizani kati ya Mungu
kwa yale apasayo kukutendea na kwako kwa yale upasayo kutenda kwake kamwe
pasingekuwa na hata kushamiliana hata chembe na amini utajiona kuwa wewe ni
mkosaji sana japo Mungu haoni yale unayo yawaza
na kujihukimu basi upaswi kuona kuwa Mungu sio mwema kwako.
Ni vizuri utambue unapo
mzungumzia MUNGU sio kitu fulani ambacho unaweza ukakiweka unavyotaka nacho
kikawa kwa namna unavyofikiria, ni vizuri utambue kwa sababu yake ndomana wewe
uko japo upaswi kumuogopa zaidi sana PENZI lake likuongoze naamini utakuwa
salama.
Jifunze kumshukuru
Mungu hata kwa madogo maana ndio mapenzi ya Mungu kwetu, maana Mungu yeye ndie
awezae kuamuru jambo jema kukufuata popote ulipo pasipo kuangalia umbali gani
uliopo kati yako na mbaraka wako.
Usiruhusu kufikia
maamuzi ya kuona Mungu ameniacha sasa naweza fanya chochote tambua sio kila
mawazo yanayokuja kwako yamebeba usahihi hivyo usiruhusu kuwa hayo ndio maisha
yako ya kuona Mungu ahusiki katika maisha yako.
Ni kweli mawazo mazuri
ni kitu kimoja lakini bila neema yake uwezi kukamilisha tambua upana wa Mungu
na Upendo katika kila hali inayokuzunguka na hapo ndipo uone NJIA YA KUTOKA!!
NA SIO LAWAMA,
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson……………………………………………0764
018535
FURAHA YA MUNGU IWE NCUVU YAKO