Jumanne, 30 Agosti 2016

DUNIA HAIWEZI KUKUPA PUMZIKO!



DUNIA HAIWEZI KUKUPA PUMZIKO


Moja ya vitu ambavyo DUNIA haiwezi kutoa ni PUMZIKO, japo watu wengi wanategemea sana na kungoja kuona DUNIA ikitoa PUMZIKO kwao, ili nao waweze kupata ahueni. Naweza kusema PUMZIKO ni rafiki wa kila mtu kwakua tuna amini kuwa katika pumziko basi hapo kuna raha, tulizo na amani kutokana na vitu hivyo basi watu upenda sana kuwa na PUMZIKO lakini wasiojue kuwa wapi ni sehemu sahihi ya kupata PUMZIKO.

Wako watu wanafikiri wakipata gari basi watapata pumziko lakini anaweza pata gari bado asilione pumziko na wakati mwingine akaona kero na gharama zimeongezeka, wengine wanasema wakisoma sana basi watapata pumziko na hatimae matarajio yao yatatimia lakini bado anakuwa anaona kama kitu alichofikiri atakipata hakipati, pia wako watu wengine wanafikiri wakijenga nyumba basi watapata pumziko lakini bado anajiona kama kuna kitu amekikosa na walio wengi inawezekana walifikiri au wanafikiri wakipa mchumba hapo atapata pumziko lakini ata baada ya kumpata na hata kufunga ndoa lakini mwisho anajiona bado ajapata kile anachokitaka.

Pumziko limekuwa ni swali lililokosa jibu! Kwani watu wengi wamejitahidi kwa uwezo wote kupata pumziko imekua kama zaidi ya tanzanite kutokana na uadimu wake mpaka imepelekea watu kuizoea hali iliyopo hata kama haipendi na kupoteza bidii yake ya kutafuta pumziko katika maisha yake kwakua anaona kutafuta pumziko imekuwa ni sawa na kutafuta chozi la samaki baharini.

Pumziko lingekuwa lina uzwa basi nafikiri hata masikini angejitahidi kwa hali na mali hata hauze mali zake ili mradi naye apate hilo PUMZIKO kwakua ana amini katika hilo anaweza pata usingizi wa furaha na amani, na hata akili yake kufanya kazi kiufasaha pasipo buguza yoyote, napengine ingeisha kutokana na wenye uwezo kuinunua na kuisha kabisa na wengine kukosa.

Lakini ashukuriwe Mungu PUMZIKO lipo ambalo hauhitaji uwe na kiasi cha fedha kikubwa ili uweze kununua kwani ni yeye mwenyewe anatoa, ila inakuwa ngumu sana kwakua yeye utoa kwa namna yake inje yake hakuna PUMZIKO lake.

Lakini dunia ya sasa tumekuwa tukitafuta sana pumziko katika njia isiyo sahihi uku tukimtupilimbali yeye mtoa pumziko ( Mungu), wako watu wamekuwa wakionga ili wapate pumziko, wakisema uongo ili wapate pumziko pasipo kujua pumziko alitokani na matamanio ya mwili bali ujazo waroho katika Mungu.

Pumziko imekuwa adimu sana katika dunia hii kutokana na kuitegemea dunia kwakua itatoa pumziko lakini imekuwa sivyo, imekuwa kama mtu anategemea kumuona mamba katika bahari na sio mtoni bila shaka unaweza kukesha hapo pasipo kuona dalili ya hata ya mkia wa mamba, japo unaweza kujifariji lakini sio kweli kila subira itavuta heri, ndo mana tumeona watu wakitumia njia zao zenye mwisho unaongeza msongo na mateso katika mwili mathalani mtu anakunywa pombe au kucheza mziki sana akitumai baada ya kucheza sana basi hata pata pumziko.

Na wengine wamekwenda mbali kidogo wakitumia muda mwingi wa kufikiria sana namna ya kutoka katika hali Fulani na hatimae kupata pumziko na kuleta furaha katika maisha yake lakini wakati mwingi imekuwa bado changamoto ikiisha hili linakuja hili unaweza kuitumia njia hiyo mwisho itakapo feli utashindwa kupata njia sahihi ya wewe kutoka hapo, usipo kuwa makini unaweza kusema kuwa hapa Mungu ayupo.

PUMZIKO!
Hili swala jepesi sana, kwanza niseme kwanza katika hali ya kawaida tu unafikiri pumziko la mtoto halisi atalipata wapi je! Kwa jirani  hama ndugu jamaa au rafiki wa wazazi ? na fikiri utakuwa umeshanielewa bila shaka mzazi ndie ajuaye tahamani ya mtoto na yeye ndie mwenye kuwajibika kuhakikisha kuwa mtoto anakuwa na furaha sana wakati wote na kama kile alichokuwa na uwezo nacho na anaona kuwa ni kitu chema kwa mtoto wake kamwe hawezi kumnyima,

Mathayo 7:11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa   vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?

Naamini umenielewa sana muache Mungu mwenyewe akupe PUMZIKO maana yeye anaijua KESHO KABLA YA LEO!

Niseme tu hakuna aliye tegemea pumziko kwa Mungu na Mungu asimpatie kama alivyosema basi atatekeleza, UKIMPATA MUNGU BASI UMEPATA PUMZIKO!

Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson…………………………………………..……………………0764 018535
INAITWA SIKU! BARIKIWA

Jumanne, 23 Agosti 2016

KINACHONIZUNGUKA KIMENITENGENEZA!



KINACHONIZUNGUKA KIMENITENGENEZA


Uwa atushangai sana kuona mmasai kuuza dawa za asili! Hama akivaa mashuka yake na kutembea barabarani hilo linakuwa ni swala la kawaida tu! Na pengine  japo mtu anaweza kutembea na rungu unaweza kumshangaa sana lakini pindi utakapo waona wamasai wengi wakitembea na rungu na huku wakicheka hauta shangaa sana kama ulivyo muona mtu asie mmasai ………….kwa nini? Na pindi unapomuona mmasai akila nyama ya ng’ombe uwezi kushangaa sana lakini pindi utakapo muona mmasai anakula samaki bila shaka hapo utaanza kuwa na maswali kichwani…………unafikiri ni kwa nini?

Tukiachana na wamasai maana hawa ni watu wazuri………..pindi unaweza kutoka na rafiki kwenda hotelini, aliyetokea kanda ya ziwa ukaona anaagiza samaki hasa aina sato bila shaka hauta shangaa…………hivi ni kwa nini? Ila unaweza kushangaa kidogo kuona muhaya pindi akiona senene anasikia kichefuchefu na kuhisi kutapika…..hivi ni kwa nini utashangaa!

Ukiwa mtafiti wa watu walifanikiwa/mashuhuri japo sio wote ila kwa asilimia kubwa utakuta familia zao zilikuwa namna yake mathalani wana muziki, wachoraji, wana michezo kwa ujumla wao ukiwafatilia vizuri kama sio tu juhudi zake binafsi basi ata mazingira yaliyo mzunguka yalipa nafasi nzuri katika kujifunza hicho kitu na hatimae akawa mahiri na kuwa kielelezo katika jamii yake na hata ulimwengu mzima.

Ndomana uwezi kushangaa watu waliotoka sehemu fulani kuwa wataalam katika jambo husika kwakua utakuta mtu amezaliwa na kukua katika mazingira hayo na hatimae akaona hayo kuwa ndio maisha yake mathalani uwezi kushangaa kuona watu wa kanda ya ziwa ni wazuri/mahiri katika uvuvi na upande wa muziki kuona watu wana uwezo mzuri kutoka baadhi ya maeneo uwa mahiri sana kuliko maeneo mengine mathalani unaweza usishangae ukisikia mtu toka MBEYA/KIGOMA anaimba lakini unaweza kuongeza umakini kidogo pindi ukiona MCHAGA anaimba sisemi watu hawa hawajui kuimba bali ni nadra kusikia.

Biblia inasema ushirika mbaya uharibu tabia njema! Kwa maana kile kinachokuzunguka na ulichokipa nafasi kina nafasi kubwa ya kukuathiri katika maisha yako na kukutengeneza kiasi kwamba mtu akikuona wewe atatambua CHIMBUKO LAKO! 

KARIBU!

Wako watu wamekuwa wakibadilika sana kutokana na mtu aliyekutana nae au hali fulani katika maisha yake inawezekana katika faida au hasara…….wako walikuwa watu wema sana ila baada ya kukutana na watu wengine wenye roho ya ukatiri ikamvika na hatimae ukatiri ukawa ni maisha yake na wako watu walikuwa wabaya na baada ya kukutana na watu wazuri wakawa watu wa maana sana wenye faida katika katika jamii,taifa na katika mataifa.

Hivyo ni muhimu kabla ujamhukumu mtu ni muhimu ni muhimu kutambua maamuzi yake ya leo yametengezwa na JANA yake ni muhimu kutambua jana ilikuaje na ndipo utafute namna ya kumsaidia katika ufasaha zaidi.

Ndomana mtu uliye muacha kwa kitambo kidogo na pindi unapokutana nae tena unaweza kukuta ana mabadiliko makubwa sana, inategemea amekutana na nani? Ambaye amemtengenezea muonekano mpya  ambao una uona sasa, usishangai kumkuta sasa pombe amekuwa rafiki yake, chumba chake kimekuwa fensi yake ya kutembea atoki tena kama zamani.

Unaweza kushangaa kuona mtu amekuwa na UPENDO, FURAHA NA KICHEKO ukaona mbona amekuwa tofauti na mwanzo hakuwa hivyo, jua kuna kitu amekutana nacho na hatimae kime mbadilisha

Nakubalina kwa asilimia kubwa ili mtu abadilike inategemea nani ameungamanisha nae na mala chache sana kuona mtu anabaidilika yeye mwenyewe tu labda NENO LA MUNGU na Mungu kwa namna yake!

Lakini kuna sababu zinazo wafanya watu wabadilike japo matawi ni mengi lakini kubwa ni moja tu ni USHIRIKA! Unaweza:

i.                    Urafiki

ii.                  Ndoa n.k

Unawa za kukuta mtu amebailika sana ni tofauti alivyokuwa kabla ya kuoa/ kuoelewa au ajakuwa na rafiki na mtu fulani ambaye akaingia katika maisha yake na kumtengeneza katika muonekano mwingine unaweza kuwa uliutegemea au usioutegemea.

Hivyo ni muhimu sana kuwa makini  katika muungamaniko ulionao unaweza kukutengeneza kuwa mbaya sana au kuwa mtu wa maana sana!

NIKUTAKIE KILA LA KHERI!
Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson…………………………………………………………………0764 018535



Jumanne, 16 Agosti 2016

SIJIONI!



SIJIONI



Wako watu wamekuwa waki wasumbua mafundi hasa wachereani kwakutaka mshono ambao utakuwa ni moja ya mtu fulani ambaye anampenda anavyo vaa pasipo kujua kwanini yule mtu alivaa vile? Ila wewe kwakua unampenda basi utamsumbua fundi utafikiri umemuajiri wewe ili mradi tu ufanane na mtu ambaye yeye mwenyewe hata ataki kukujua! Sio hao tu bali kuna watu wanaenda salon wakita minyoo/ kutengeneza nywele zinazofanana na watu waliokichwani mwao nao wanatumia muda mwingi kumuelekeza mwenye saloon kama yeye amelipia saloon siku nzima! 

Ni jambo ambalo mtu ulitegemea pindi anapojiangalia katika kioo ajione yeye maana hiyo ndio kazi moja wapo ya kioo kumuonyesha mtu jinsi anavyoonekana ili kumrahisishia katika kujirekebisha mahali penye upungufu ili kuwa bora zaidi au kughara zaidi au kuwa na muonekano ulio bora zaidi.
Sijui utajisikiaje pindi utakapoamua kujiangalia katika kioo ukawa UJIONI wewe ila unamuona mtu mwingine je! Utachukia au utaamua kubadilisha kioo ili kupata utofauti ili uone kama kuna mabadiliko yoyote! Au utajisikia sasa uko bomba!

Lakini katika dunia ya sasa watu wengi wamekuwa wakitamani pindi wakijiona wasiojione wao bali waone mfanano wa mtu mmoja mashuhuri katika ulimwengu! Na hata kuibuka mitindo mbalimbali ya nywele, nguo, muonekano na hata ongea ya mtu imebebwa na mtu mwingine! 

Siongelei wale wanaofanya vichekesho au maigizo bali nazungumzia mtu husika akiwa na akili timamu katika kukubali mtu mwingine aishi kupitia yeye azidi kumtambulisha mtu mmoja kwasababu yeye anampenda pasipo kujali wewe unamtambulisha je! Wewe nani atakutambulisha? Wako watu wanaita swaga………..!

Ukiangalia watu wanamna hii unaweza kusema wanaweza kumuuliza Mungu kwanini umeniumba hivi ukiniumba vile hama kwanini mimi sikuzaliwa marekani ni kazaliwa bara la giza! Ukimuangalia jinsi mtu anavyojiangalia namna anavyoenda ni vitu fulani hivi ambavyo haviendani kabisa,

Kweli katika ulimwengu wa sasa watu wengi wamepoteza utambulisho wao,utaweza kuona mtu sio kwamba anatamani kufanikiwa kama mtu mashuhuri alivyo fanikiwa bali uanza kuishi kivuli cha mtu katika muonekano usiofanana bali unaolazimishwa kufanana mathalani mtu anampenda mchezaji messi basi utakuta mtu anataka kuvaa kaptura kama anayo vaa messi pasipo kujua yeye anavaa vile kwa sababu ya nini sio hilo tu hadi kutembea, kushangilia ili mradi yeye aonekane kuwa yeye ana mapenzi ya dhati na mchezaji huyo.

Sio mfanano katika hilo bali hali uoenekana katika fani mbalimbali muziki, mitindo na hata filamu mtu utaka kuenenda katika muonekano wa mtu fulani, pasipo kujua kwa kiasi kikubwa katika kufanya hivyo unapoteza utambulisho wako ambao Mungu ameweka  ndani yako ili kuleta msaada kwa jamii fulani ambayo Mungu amekupa neema ya wewe kuwepo.

Maisha haya upelekea kutoishi wewe bali yeye kuishi kupitia wewe inakuwa kama wewe ukupaswa kuwepo kwakua pacha wako ameshatokea kwakua yote anayo  yafanya yeye ndiyo wewe unayafanya baada ya kuona yeye anafanya, bila shaka unakandamiza ile hazina ambayo Mungu ameiweka ndani yako kwa kua unaiona haina thamani ila ya wengine ndio iliyo bora kwakua imeshatambulika na kupata kibali mioyoni mwa watu! Pasipo jua kuwa hata wewe ukiamua kukipenda kilicho chako watu wengine watakipenda tu na hata wasipo kipenda wewe unamalizana na Mungu kwa kutumia kile ulichopewa na Mungu.

Kupenda au kumkubali mtu katika kitu kizuri anachokifanya sio vibaya ila sio vyema kupoteza au kutotumia hazina ambayo Mungu ameweka ndani yako! Maana utakuta mtu anavyompenda mtu hadi unashanga……..utakuata anataka apige mswaki kama yule, acheke kama yule, alale kama yule na hata kulia kama yule basi hapakuwa sababu ya wewe kuwepo, tambua Mungu kumuumba yule na WEWE  kuna sababu na wala haikuwa kwa bahati.

Kupenda kitu kizuri anachokifanya mwingine ni vizuri kwani Mungu amesema TUPENDANE ni sawa na ni vizuri lakini sio watu wakikuona wewe wamuone mtu mwingine kabisa ambaye anaushirikiano na wewe kabisa.

Ni vizuri kujifunza mambo mazuri kwakua ni jambo jema litakuongeza katika lile ambalo unalolifanya ili liwe bora zaidi zaidi, kwani kila utendaji wa mtu una mapungufu yake hivyo utakapo kuwa pale utajifunza vyema ili usifanye makosa tena bali uendelee mbele katika ubora mpya.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………………0764 018535

JITHAMINI UTATHAMINIKA-------JIONE MWENYEWE MAANA WEWE NI BORA!

Jumanne, 2 Agosti 2016

USIIPENDE KESHO KAMA UJAIMALIZA LEO!



USIIPENDE KESHO KAMA UJAIMALIZA LEO


Hata paa likiwa linathamani kiasi gani lakini kamwe hauwezi  kulisimika kwanza alafu ukafuata msingi wa nyumba! KARIBU
 
Ni muhimu tuanze na MOJA na kisha twende kwenye MBILI, sio vizuri tu! ila pia inaleta maana! Ni vyema kuijenga vizuri msingi ili ikurahisishie kujenga nyumba imara na paa iweze kuwa na maana kuwepo maana dhuruba itakapo kuja haita iangusha maana usalama wa msingi utakuwa umeishikilia paa basi nawe utakaa salama na sio salama tu bali utayafurahia maisha yako! Karibu sana

Ni kawaida ya binadamu kupenda jambo jema na kuchukia jambo baya ni kawaida sana! Na katika muonekano wa jinsi hii utaitwa binadamu wa kawaida, kwa watu wenye akili zao watasema hasa huu ndio ubinadamu kuchukia lililobaya na kupenda kitu kizuri! 

Ni jambo jema sana kupenda kitu kizuri kwa kuwa kitu hicho kimekuwa kizuri kwa ajili ya kupendwa na sio kuchukiwa maana hilo silo lengo lake! Changamoto inakuja katika katika kukipata kitu kizuri maana kina vutia na wakati mwingine kinaweza kuwa na ushindani katika kukipata maana ni kitu kizuri hivyo kila mmoja anakihitaji japo inawezekana kwa lengo tofauti.

Sio kila jambo zuri utafikiria linafaa maadam umelifahamu kuwa ni jambo nzuri kila jambo zuri linakuwa la maana sana pindi utakapolitambua wakati wake sahihi! Niseme tu jambo sahihi linapofanywa katika hali sahihi basi kunakuwa na uwezesho uliobeba usahihi katika kukustawisha (mwenye akili njema).

Nikubaliane sana katika dunia ya sasa watu wamekuwa waki harakia mambo ya kesho kabla yakuimaliza leo wakiwa wanasababu nyingi mathalani nataka niwe wa kwanza mimi niitwe mvumbuzi au nisiwe boya, nikichelewa kitakuwa kimeisha, uwa mimi sipendi kujuta nataka niwai mapema ili nisijute!

Niseme kweli kuna mambo yanahitaji uwe na haraka ili kufanikisha mambo yaende sawa mathalani ajari lazima ufanyike uwezekano wa kuhakikisha usalama wa maisha yao waliojeruhiwa na mengine mengi lakini kamwe sio mambo yote au mengine yenye kivutio cha macho ya kakupa msukumo mkali pasipo kujua huu ni wakati wake wa mimi kuingia huku au kufanya hili.

*** Ni muhimu kujua kwamba kama ujaitendea haki leo basi jua hata kesho hautaitendea haki maana itakusumbua : usione watu wanakula basi nawe ukaingia kwenye kula lazima uangalia kweli wewe una njaa na ni kweli hicho chakula ni salama kwa kula! Na kweli ukila chakula hicho utashiba?

Ni muhimu kuwa na maswali yenye manufaa kwako ili kujiweka katika nafasi ya kutofanya makosa yasiyo ya lazima pindi utapoingia katika ulimwengu wowote mathalani URAFIKI, NDOA! Sio dhambi kuangalia katika ushirika huo mambo gani yanaendelea na majukumu gani yanaongezeka ila sio kwa kupa hofu bali katika kukupa kujipanga ili ufanye kitu kwa ubora pasipo KUMSINGIZIA SHETANI MAHALI AMBAPO YEYE AHUSIKI.

Alafu sio ujinga kuikamilisha LEO ikawa ni msingi wako mzuri wa kufanya KESHO kuwa yenye maana zaidi kwako, mathalani unaweza mtu anaweza kuwa mikakati mizuri ya biashara yake lakini baada ya kuona mwingine anauza zaidi kuliko yeye basi anafungua na yeye biashara kama ya yule jirani yake na baada ya muda yule akaacha ile biashara na yeye akaendelea hata baada ya mwingine kuacha pasipo kujua mwenzake ameacha kwa sababu msimu umeisha, au kunamtindo mpya umeingia unaanza kusema mimi nimerogwa au hapa sio bure alivyoondoka kaniachia uchawi ona sasa biashara inadoda.

Ishi maisha ya leo vizuri sana ili hata ikifika kesho usihitamani JANA, kwakua ulitendea ipasavyo na hivyo imekupa msingi mzuri wa wewe kufika hatua hiyo kwa ushindi.

Lazima uelewe kuwa Mungu aliiweka LEO na KESHO alikuwa na maana kubwa sana basi heshimu hilo na hakikisha huna haraka ya KESHO kama UJAIMALIZA LEO, kesho hipo tu hauhitaji kuikimbilia maana itakuja tu!

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….0764 018535

KESHO YAKO IKO MIKONONI MWA MUNGU! IKO SALAMA